Sajil-2: Kombora hatari la Iran linalofika Israel kwa 'dakika 7'

a

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jaribio la kwanza la mafanikio la kombora hili lilifanyika mwaka 2008
Muda wa kusoma: Dakika 4

Mzozo wa hivi karibuni wa kijeshi kati ya Israel na Iran umekuwa jaribio la uwezo wa mapigano wa nchi zote mbili, pamoja na silaha zao.

Wakati Iran ilipoishambulia tena Israel wiki moja na nusu iliyopita, ilidai kwa mara ya kwanza kwamba kombora la Sajil-2 la Iran lilitumika katika shambulio hilo. Hata hivyo, Israel inadai kuwa jeshi lake lilizuia shambulio la kombora la Sajil na kulinasua kwa mafanikio kwa msaada wa mfumo wa ulinzi.

Ingawa mapigano yamesimama kwa muda, kombora hili linaonekana kuwa sehemu muhimu ya nguvu ya Iran.

Walinda Mapinduzi wa Iran wamesema kuwa mashambulizi ya Jumatano ya wiki iliypita yalifanywa kama sehemu ya "Operesheni Ahadi ya Kweli 3." Taarifa iliyotolewa na Walinda Mapinduzi ilisema kwamba "operesheni ya 12 ya kulipiza kisasi ya Operesheni Ahadi ya Kweli 3 imezinduliwa kwa kombora zito sana la masafa marefu la Sajil la hatua mbili." Taarifa hiyo, ikielezea sifa za kombora hili, inadai kwamba Sajil ni mojawapo ya silaha zenye nguvu na sahihi zaidi za kimkakati za Iran, zenye uwezo wa kuharibu malengo muhimu ya adui.

Nguvu ya Kombora la Sajil

a

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kombora la Sajil lina urefu wa takriban mita 18 nalinalotumia mafuta, jambo linalolifanya kuwa hatari

Sajil ni kombora la balistiki la masafa ya kati lenye uwezo wa kufikia maeneo lengwa hadi kilomita 2,000. Kwa masafa haya, kombora hili linaweza kulenga Mashariki yote ya Kati, ikiwemo Israel, kusini mashariki mwa Ulaya, na sehemu za Asia ya Kati, likirushwa kutoka Iran. Ikiwa litarushwa kutoka mji wa Natanz nchini Iran, linaweza kufika jiji la Tel Aviv nchini Israel kwa dakika saba tu.

Kombora la Sajil lina urefu wa takriban mita 18 linatumia mafuta imara, jambo linalolipa faida dhidi ya makombora yanayotumia aina nyingine za mafuta ya kawaida. Kutokana na matumizi yake ya mafuta imara, linaweza kuandaliwa kurushwa haraka zaidi, lina uwezo bora wa kuhifadhi vilipuzi, na linaweza kuwa na ufanisi zaidi wakati wa mapigano.

Kombora hili linaweza kubeba kichwa cha kivita chenye uzito wa takriban kilogramu 700 na, kutokana na hili, lina uwezo mkubwa wa uharibifu dhidi ya maeneo lengwa. Jaribio la kwanza la mafanikio la kombora hili lilifanyika mwaka 2008 na katika jaribio hilo lilifunika umbali wa kilomita 800. Jaribio lake la pili lilifanyika Mei 2009, likijaribu teknolojia ya hali ya juu na mifumo ya ulipuaji.

Kwa mujibu wa Taasisi ya Kimkakati na Mafunzo ya Kimataifa ya Marekani (Center for Strategic and International Studies), "Kunaweza kuwa na aina kadhaa za kombora la Sajil. Mwaka 2009, Iran ilijaribu kombora lililoitwa Sajil 2. Ripoti isiyothibitishwa inasema kwamba Sajil 3 inaweza kuwa bora zaidi. Sajil 3 ni kombora la hatua tatu lenye masafa ya juu ya kilomita 4,000 na uzito wa kilogramu 38,000."

Iran haijajaribu kombora la Sajil hadharani tangu mwaka 2012, lakini lilijaribiwa wakati wa mazoezi ya kijeshi mwaka 2021, karibu muongo mmoja baadaye.

Mpango wa makombora wa Iran unaendelea kukua licha ya vikwazo

a

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Iran imetumia makombora ya hypersonic ya Al-Fath pamoja na Sajjil katika mashambulizi ya hivi karibuni dhidi ya Israel.
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kwa mujibu wa Taasisi ya Amani yenye makao yake Marekani (Peace Institute), Iran ina hifadhi kubwa na yenye aina nyingi za makombora ya balistiki katika Mashariki ya Kati. Wakati huo huo, Iran ndiyo nchi pekee katika eneo hilo isiyo na silaha za nyuklia, lakini makombora yake ya balistiki yanaweza kufikia umbali wa kilomita 2,000.

Teknolojia ya balistiki ilitengenezwa wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia, lakini ni nchi chache tu duniani zenye uwezo wa kutengeneza makombora ya balistiki zenyewe kwa kutumia teknolojia hii. Iran imepata teknolojia hii na kutengeneza makombora ya balistiki katika miongo miwili iliyopita licha ya vikwazo vikali vya kimataifa.

Kiongozi Mkuu wa Iran Khamenei alisema katika hotuba kwamba mipango ya kijeshi na makombora ambazo nchi za Magharibi zina wasiwasi nazo zote zilitengenezwa chini ya vikwazo.

Hivi sasa Iran inazalisha zaidi ya aina 50 za roketi, makombora ya balistiki na cruise, pamoja na ndege zisizo na rubani za kijeshi, ambazo baadhi zimetumika katika migogoro ya kimataifa kama vile vita kati ya Urusi na Ukraine.

Iran imedai kuwa kizazi chake kipya cha makombora ni silaha ya hypersonic, ambayo ni aina ya silaha inayokwenda kwa kasi mara tano hadi ishirini na tano ya kasi ya sauti. Iran ilianzisha kombora la 'Fatah' kwa mara ya kwanza kama kombora la hypersonic katika makundi ya balistiki na cruise.

Kombora la hypersonic la 'Al-Fath' lina masafa ya kilomita 1,400 na IRGC imedai kuwa lina uwezo wa kukwepa na kuharibu mifumo yote ya ulinzi wa makombora. 'Al-Fath' ni kizazi cha makombora yanayotumia mafuta imara ambayo hufikia kasi ya Mach 13 hadi 15 kabla ya kufika kwenye lengo lao. Mach 15 inamaanisha kasi ya kilomita tano kwa sekunde