Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Dawa ya mikojo ya watawa ambayo 'iliwasaidia' wanaume kupata watoto
Watawa wa kike huombea, lakini habari kuhusu tiba iliyotokana nao inaturudisha miaka ya 1940. Katika miaka hiyo, mwanasayansi wa Kitaliano Piero Donini aligundua homoni mbili zinazoitwa ‘LH na FSH,’ zinazowasaidia wanawake kuzalisha mayai kutoka katika ovari na kupelekea ujauzito.
Miaka ya 1940 alipima mikojo ya mamia ya wanawake na kugundua homoni hizo zipo kwa wingi kwa wanawake ambao hedhi yao imekata.
Baada ya hedhi kukata, na ovari inapoacha kuzalisha mayai, LH na FSH huongezeka wakati mwili unapojaribu kuchochea uzalishaji wake. Donini alitambua kupata homoni hizi kutoka kwa wanawake wasiopata tena hedhi kutasaidia wanawake wagumba.
Donini aliita mchanganyiko huo ni ‘pergonal,’ baada ya kuzitenganisha homoni kutoka sampuli ya mikojo. Aliamini Pergonal itasaidia kushika mimba, lakini tatizo likawa ni wapi utazalisha pergonal kwa kiwango kikubwa na wapi atapata kiwango kikubwa cha mikojo ili kuzalisha homoni. Miaka ikakatika bila mafanikio.
“Mwongo mmoja baadaye, wanasayansi wanaotafiti kuhusu ugumba walisikia kuhusu kazi ya Donini,” anaeleza Oliver Stelle. Kwa mujibu wa kitabu, “Haidhti ya Homoni Mbili,” kilichochapishwa 1996 (A Tale of Two Hormones).
Stille anaandika, Donini alitafutwa na Bruno Lunenfeld, mwanafunzi wa udaktari aliyekuwa akifanya kazi Geneva – alikuwa anatafiti kuhusu matumizi ya homoni za binaadamu ili kuwezesha mimba.
Akitokea familia ya kiyahudi kutokea Australia, shauku yake ilikuwa ni kuongeza kuzaliana kwa mayahudi baada ya kupungua kwa kiasi kikubwa kutokana na mauaji ya Holucaust.
'Lonenfeld aliwasilisha kesi yake kwa wakuu wa kampuni ya madawa, ya Serono ili kuzalisha dawa za kutosha kwa ajili ya majaribio. Ila uzalishaji huo ulihitaji maelfu ya madumu ya mikojo ya wanawake wasiopata hedhi.
Kijana mdogo Lunenfeld alikutana na bodi ya wakurugenzi wa Serono. “Nilikuwa kama mtoto tu mbele yao,” Lunenfeld aliliambia gazeti la kiisraeli la Haaretz.
Baada ya kuzungumza kuhusu ugunduzi huu, niliiomba bodi hiyo kunisaidia kupata wanawake wanne wasiopata hedhi ambao watakubali kukusanya mikojo yao kila siku.
Nilimaliza mazungumzo yangu na kila mmoja alinipigia makofi, kisha mwenyekiti wa bodi akasimama, “sawa, ila hiki ni kiwanda cha dawa sio kiwanda cha mikojo.” Nilitoka nje nikiwa nalia.
Awali, wakuu wa Serono walimjuulisha kuhusu Giulio Pacelli, mtalioano wa hadhi ya juu na mpwa wa Papa Pius. Pacelli pia alikuwa ni mwanachama wa bodi ya Cerono. Pacelli alivutiwa na kazi ya Lunenfeld, baada ya vikao vingi – Pacelli alirudi na Lunenfeld kwa bodi ya wakurugenzi.
Alizungumza yaleyale niliyozungumza siku kumi zilizopita, ila mwisho aliongeza sentensi moja: “Mjomba wangu Papa Pius atatusaidia kupata watawa wa kike walio uzeeni ili kukusanya mikojo kila siku kwa lengo hili takatifu.”
Sentensi hii bila shaka iliishawishi bodi ya wakurugenzi papo hapo kuunga mkono mradi wetu wa utafiti, kwa pesa na rasilimali. Baadaye niligundua Vatican inamiliki asilimia 25 ya shughuli za Serono.
Watawa kumi, siku kumi kwa tiba moja
Punde gari la migizo likaanza kusafirisha mikojo ya mamia ya watawa wa kike kutoka makaazi ya wastaafu wa kikatoliki kutoka Italy kote na kupeleka katika makao makuu ya Serono, Roma. Ikichukua watawa kumi, kwa siku kumi kutengeneza dawa ya mtu mmoja.
Mwaka 1962, mwanamke mmoja huko Tel Aviv, Israel alijifungua mtoto wa kike baada ya kutibiwa na Pergonal. Pergonal hupitishwa kwa sindano. Huyu alikuwa mtoto wa kwanza kuzaliwa kwa matibabu haya. Ndani ya miaka miwili, mimba 20 zilitolewa zikitokana na matibabu hayo.
Oktoba 1, 1964 gazeti la New York Times liliripoti kwamba maabara ya Marekani ambayo ni msambazaji wa Pergonal nchini humo imetoa onyo ikieleza Pergonal ni kwa ajili ya majaribio ya kitafiti tu. Taarifa hiyo pia ikaeleza watoto wanne wamezaliwa kutokana na dawa hiyo huko Queens na Sweden.
Mwanzoni mwa miaka ya 70, wanawake wa Kimarekani walianza kutumia dawa hiyo mara kwa mara. Kwa mujibu wa ripoti nyingine, ya New York Times, katika kipindi kifupi karibia wanawake laki mbili wakitumia dawa za kuzuia mimba kila mwaka. Makadirio ya wanawake 9,000 kati yao walikuwa wakitibiwa kwa Pergonal, kwa gharama ya dola za kimarekani 10,000 ikijumuisha ada ya daktari na gharama za kliniki.
Ruhusa kwa Wanaume
Gazeti la New York Times liliripoti Januari 21, 1982, Pergonal dawa ya homoni inayotumiwa na wanawake wagumba kwa miaka kumi sasa, jana imeruhusiwa kutumiwa na wanaume wagumba na Mamlaka ya Dawa Na Chakula.
Wanaume wenye tatizo hilo, ni pale manii kutozalishwa kwa sababu ya kushindwa kwa tezi kutengeneza homoni ya LH au FSH ama zote mbili.
Dkt. Russell W. Pelham, mkurugenzi wa Serono, anakadiria kati ya wanaume 10,000 hadi 50,000 ni watumiaji wa dawa hii.
Dkt. Richard Sherness, mtafiti mkuu wa taasisi ya taifa ya afya ya mtoto na maendeleo ya binadamu, alitafiti kuhusu mafanikio ya Pergonal kwa wanaume kwa miaka 12.
Gazeti linaandika, “baadhi ya wagonjwa hupata mafanikio ndani ya miezi sita ama nane na wengine hulazimika kupata matibabu kwa miezi kadhaa,” alisema Dkt. Sherness.
Nchi nyingine nane, zimeidhinisha matumizi ya Pergonal kwa wanaume na inatumiwa na wanaume katika nchi nyingine saba.
Kwa mujibu wa Dkt. Pelham, matibabu kwa wanaume hayakuwa na athari zozote. Katikati ya 1980 mahitaji yaliongezeka na Serono ikahitaji lita 30,000 ya mikojo kwa siku ili kuzalisha dawa za kutosha.
Watoto wengi kwa wakati mmoja
Pragunal ilijipatia heshima ya kuzalisha mtoto zaidi ya mmoja. Mei 1985, wapenzi kutoka California walipata watoto saba, na kufunga kesi dhidi ya Serono wakidai kuwa hawakueleza vizuri matumizi ya dawa hiyo.
Kwa mujibu New York Times, baba wa watoto, Samuel Frastasi, alisema, "hatukutaka kuweka rikodi sisi."
Tafiti na matumizi ya dawa yalipo boreshwa, idadi ya watoto machapa au zaidi ikapungua. Mwaka 1991, mapacha walizaliwa na wapenzi wale wale wa California, kwa msaada wa dawa hiyo hiyo. Kuzaliwa kwao kulitangazwa na mwanasheria wao, Brown Greene.
Greene ni mwanasheria aliyewawakilisha na kushinda kesi ya milioni 2.7 wakati wa ile kesi ya kuzaa watoto saba. Baadaye ikagundulika Julai 1990, Patti Frastasi alitumia tena Pergonal ili kupata mimba tena.
Ni watoto watatu tu kati ya watoto hao ambao wanne wa kiume na watatu wa kike, walizaliwa kabla ya muda wao – baba yao alisema hao waliozaliwa kabla ya muda walikuwa na matatizo ya kiafya na ukuaji.
Lakini Greene anasema, mapacha wa sasa wako na afya na mmoja wa kiume amempa jina langu kwa heshima.
Kiwango cha mikojo kilipokuwa kidogo kwa uwiano wa uhitaji wa dawa, kampuni ilianza kutengeneza homoni hizo maabara. Matokeo ya matibabu yao yaliyoitwa Gonal-F yaliruhusiwa 1995.
Serono ilinunuliwa na Merck mwaka 2007. Inaendelea kuzalisha dawa hadi leo, kwa kuwa homoni zinazalishwa maabara, mkojo wa watawa wa kike hauhitajiki tena kutengeneza dawa hiyo.