'Sayansi ya Pesa': Kuelewa pesa ni nusu ya utatuzi wa shida zako...

Kupata mshahara, kuwekeza au kuweka akiba, gharama, madeni, mali, kujaribu kudumisha utajiri kama upo... maisha ya mwanadamu kawaida yanazunguka haya.
Brian Tracy, mtaalam wa masomo ya kifedha nchini Marekani, anasema kwamba kadiri unavyoelewa pesa vizuri, ndivyo maisha yako yatakavyokuwa bora.
Ameandika kitabu kiitwacho 'Sayansi ya Pesa' akielezea kwa kina kuhusu fedha za kibinafsi.
Kuanzia maisha kama kibarua, Tracy alikua mkuu wa kampuni yenye kampuni nyingi zinazoongoza kama wateja.
Hadi sasa wafanyakazi na maofisa wa mashirika laki mbili na nusu wamehudhuria semina zinazoendeshwa na yeye mwenyewe kuhusu mada mbalimbali.
Alileta mafunzo aliyopata kutokana na matukio mengi aliyoyaona na kujifunza katika safari yake ya maisha katika mfumo wa kitabu kilichoitwa 'Sayansi ya Pesa'.

Chanzo cha picha, Getty Images
Jinsi ya kudhibiti gharama?
Tracy anasema kuwa kuishi bila deni ni nusu ya kushinda vita vya matatizo yanayokukabili maishani mwako.
Akisema kwamba ukipunguza gharama, hautaingia kwenye deni, alipendekeza njia kadhaa kuu za kufanya hivyo.
Muhimu kati yao ni 'kuahirishwa kufanya manunuzi yasiyo ya lazima kwa siku 30'.
Hiyo inamaanisha ikiwa ungependa kununua bidhaa yoyote ya kifahari au isiyo ya lazima, unapaswa kuiahirisha kwa siku 30.
Hata baada ya siku hizo thelathini, ikiwa unahisi haja ya bidhaa hiyo, basi ndio unapaswa kununua.
Mojawapo ya sababu kuu za kuongezeka kwa matumizi bila udhibiti ni kununua vitu ambavyo havihitajiki kwa kukurupuka.
Kulingana na Tracy, njia hii ya siku 30 ya kuahirisha inaweza kuepusha hatari hiyo.
Uwekezaji bora ni upi?
Brian Tracy anasema kuwa uwekezaji bora ni wakati na juhudi tunazoweka katika maendeleo yetu.
Wengi wanahangaikia mapato kutokana na shughuli nyingine zaidi ya kazi na hutumia muda wao mwingi katika shughuli hizo.
Hili si wazo zuri.
Ikiwa wakati huo huo unatumika katika kuboresha ujuzi wetu uliopo au kujifunza ujuzi mpya, mapato yataongezeka mara nyingi.
Kwa mfano, Tracy anaeleza katika kitabu chake kwamba muda ambao wafanyakazi hutumia katika biashara ya ndani unaweza kutumika vyema zaidi katika kazi zinazohusiana na kazi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Maisha ya mwanadamu ni mkusanyiko wa mazoea
Tracy anaamini kuwa mwanadamu sio kiumbe wa kijamii tu bali pia mtumwa wa tabia zake.
Alisema kwa mifano mingi kwamba mazoea hutawala maisha ya mtu.
Fikiria juu ya maendeleo kuwa tabia zako. Tunapaswa kutenga muda fulani kila siku kwa lengo letu la kesho.
Alisema kuwa hata katika safari ya kutafuta fedha za kibinafsi, tunaweza kupata uhuru wa kifedha ikiwa tu tunafanya tabia nzuri kuwa sehemu ya maisha.
Tracy anapendekeza kwamba matumizi yanaweza kudhibitiwa kwa kubadilisha mazoea machache.
Kwa mfano, watu wanaotumia pesa kwa kadi ya mkopo wanaweza kupunguza matumizi yao kwa kubadili tabia hiyo.
Tofauti kati ya mshahara, kipato na mali
Mshahara wetu sio utajiri wetu.
Tracy anahitaji kuelewa hili vizuri zaidi.
Wengi wako chini ya dhana potofu kwamba mshahara mkubwa unamaanisha utajiri zaidi.
Mshahara ukiongezeka, gharama pia zitaongezeka.
Hili ni jambo la kuzingatia.
Baada ya kufanya uwekezaji mwingine katika mshahara tunaopata, kiasi kinachobaki kinapaswa kutumika kwa matumizi tu.
Katika suala hili, Tracy anamtaja Warren Buffett kama aliyeishi katika nyumba moja ndogo kwa miongo kadhaa.
Buffett amekuwa mmoja wa watu tajiri zaidi ulimwenguni kwa miongo kadhaa.
Amekuwa akikaa katika nyumba moja kwa siku nyingi sana. Nyumba hiyo pia ilinunuliwa kama sehemu ya uwekezaji wake.
Mtazamo wa muda mrefu
Kulingana na utafiti wa Chuo Kikuu cha Harvard, asilimia 85 ya wawekezaji ambao wamepata faida kupitia soko la hisa wanawekeza kwa malengo ya muda mrefu.
Mtazamo wa muda mrefu ni kanuni ya msingi ya fedha za kibinafsi.
Vile vile vilithibitishwa katika utafiti hapo juu.
Tracy pia anataja jambo hili mara kadhaa katika kitabu chake 'Sayansi ya Pesa'.
Kushughulika ni muhimu
Kulingana na Tracy, maendeleo hayawezekani bila hatua.
Wale ambao wanataka kufikia utoshelevu wa kifedha wanapaswa kuendelea na shughuli inayofaa.
Hakuna ubaguzi kwa hili. Mmea hauwezi kukua bila mbegu na bila shughuli zetu hakuna mapato.
Jinsi ya kuondokana na deni?

Chanzo cha picha, Getty Images
Kanuni ya msingi ya fedha za kibinafsi ni kulipa madeni madogo kwanza.
Brian Tracy naye alisema vivyo hivyo.
Inasemekana kuwa deni ni kitu kibaya na mara tu unapokwama ndani yake, ni vigumu kutoka.
Sio sahihi kuchagua njia potofu kwa mapato ya haraka haraka.
Kwa mfano, kamari. Tracy anaonya kuwa kucheza kamari kidogo ni sawa, lakini ukizoea kucheza kamari kwa kiwango kikubwa katika miji kama Las Vegas, maisha yatazidi kwenda juu chini.
Wale wanaofuata maendeleo ya kifedha maishani wanapendekeza kwamba ni muhimu kujiepusha na kucheza kamari.

Chanzo cha picha, Getty Images
Soko la Hisa – Mali ya majengo isiyohamishika
Wataalam wa fedha za kibinafsi wanasema kurudia kuelewa tofauti kati ya soko la hisa na mali isiyohamishika kam amajengo na mashamba.
Malengo tofauti ya kifedha yanapaswa kuamuliwa kwa haya mawili.
Wataalamu wanasema kwamba mbinu za uwekezaji zinapaswa kuchaguliwa ipasavyo.
Tracy anapendekeza kufanya maamuzi ya mali isiyohamishika bila hisia.
Wale wanaowekeza kupitia soko la hisa wanashauriwa kupata faida kutoka kwa fedha za faharisi na kuchukua maamuzi katika mwelekeo huo.
Mwandishi wa makala hii ni mtaalamu wa masuala ya fedha.














