'Ninapowaona wavulana wakienda shule, ninaumia'

Tamana

"Kila siku ninaamka nikiwa na matumaini ya kurejea shuleni. Wao [Wataliban] wanaendelea kusema watafungua shule. Lakini imekuwa karibu miaka miwili sasa. Siwaamini. Inavunja moyo wangu," anasema Habiba mwenye umri wa miaka17.

Anapepesa macho na kuuma midomo akijaribu sana kutolia.

Habiba na wanafunzi wenzake wa zamani Mahtab na Tamana ni miongoni mwa mamia ya maelfu ya wasichana ambao wamezuiwa kwenda shule ya sekondari katika sehemu kubwa ya Afghanistan na Taliban ikiwa ni nchi pekee kuchukua hatua hiyo.

Mwaka mmoja na nusu tangu maisha yao yasitishwe, huzuni yao bado mbichi.

Muda wa shule unaanza

Wasichana hao wanasema wanahofia kwamba ghadhabu ya kimataifa kuhusu kile kilichowapata inafifia, ingawa wanaishi na maumivu kila siku huku huzuni ikiongezeka wiki hii wakati muhula mwingine wa shule ulipoanza bila wao.

“Ninapoona watoto wa kiume wanakwenda shule na kufanya chochote wanachotaka, inaniuma sana, ninajisikia vibaya sana, ninapomuona kaka yangu akitoka kwenda shule najisikia kuvunjika moyo,” anasema Tamana. Sauti yake inatetemeka na machozi yanatiririka mashavuni mwake lakini anaendelea.

“Hapo awali kaka yangu alikuwa akisema siendi shule bila wewe, nilimkumbatia na kumwambia nenda, nitaungana nawe baadaye.

"Watu wanawaambia wazazi wangu usijali, una watoto wa kiume. Laiti tungekuwa na haki sawa."

Habiba

Matumaini yoyote ambayo wangeweza kuwa nayo ya kufunguliwa kwa shule yamepunguzwa na vikwazo vinavyoongezeka ambavyo serikali ya Taliban imeweka kwa wanawake.

"Kulikuwa na uhuru kidogo mwanzoni, lakini hatua kwa hatua hiyo ilibadilika," Habiba anasema.

Kizuizi cha kwanza kufuatia marufuku ya shule za sekondari kilikuja mnamo Desemba 2021, wakati Taliban walipoamuru kwamba wanawake watalazimika kuandamana na jamaa wa kiume ikiwa watasafiri zaidi ya kilomita 72 (maili 48).

Mnamo Machi 2022, serikali ya Taliban ilitangaza kuwa shule za sekondari zitafunguliwa kwa wasichana, na kuzifunga ndani ya saa chache.

Masharti ya mavazi

Chini ya miezi miwili baadaye, amri ilipitishwa kwamba wanawake wangelazimika kuvaa nguo zinazowafunika kuanzia kichwani hadi miguuni, ikiwemo vazi la kufunika uso.

Mnamo Novemba, wanawake na wasichana walizuiliwa kutoka kwenda kwenye bustani za Umma, ukumbi wa michezo na mabwawa ya kuogelea. Wasichana hawakuruhusiwa tena kuchagua masomo kama vile uchumi, uhandisi na uandishi wa habari katika chuo kikuu.

Mwezi mmoja baadaye, pigo kubwa lilitolewa wakati vyuo vikuu vilifungwa kwa wanafunzi wa kike, na wanawake walipigwa marufuku kufanya kazi katika Mashirika yasiyo ya kiserikali ya ndani na ya kimataifa isipokuwa zile za sekta ya afya.

Mahtab's photo, with her quoted as, saying: "Life has no meaning without education. I think death is better tthan a life like this.

"Mapungufu haya yakiongezeka, sidhani kama maisha haya yatafaa tena kwa wanawake, hatuna haki yetu ya msingi kama binadamu, maisha hayana maana bila elimu, nadhani kifo ni bora kuliko maisha kama haya." Mahtab anasema.

Mahtab alijeruhiwa katika shambulio la bomu katika shule ya Sayed Ul-Shuhada mnamo Mei 2021, wakati Taliban walipokuwa wakipigana na vikosi vya serikali iliyopita ya Afghanistan.

"Nilikuwa na majeraha shingoni, usoni na mguuni. Yalikuwa maumivu. Lakini nilidhamiria kuendelea kusoma," anasema. "Hata nilihudhuria mtihani wangu wa katikati ya muhula, lakini mara baada ya Taliban kuja yote yalikuwa yamekwisha."

'Mazingira yanayofaa'

Taliban wamesema kuwa shule na vyuo vikuu vimefungwa kwa muda tu kwa wanawake na wasichana hadi "mazingira yanayofaa" yaweze kuundwa. Ni dhahiri kwamba kuna mgawanyiko ndani ya serikali ya Taliban kuhusu suala hilo, lakini hadi sasa juhudi zozote za wale wanaoamini wasichana wanapaswa kuruhusiwa kusoma hazijazaa matunda.

Kuhusu baadhi ya vikwazo vingine, Taliban wanasema viliwekwa kwa sababu wanawake hawakuwa wamevaa hijabu au kufuata sheria za Kiislamu. Utekelezaji wa sheria za Taliban sio sawa katika majimbo yote, lakini kanuni zinaunda mazingira ya hofu na machafuko.

"Siku zote tunavaa hijabu. Lakini haileti tofauti. Wanamaanisha nini? Sielewi," Tamana anasema.

Katika wakati wetu nchini Afghanistan kabla na baada ya utekaji wa Taliban, hatujawahi kukutana na mwanamke wa Afghanistan ambaye hajavaa hijabu.

Maktaba ya wanawake

Ili kukabiliana na kupungua kwa nafasi za umma kwa wanawake, Laila Basim alikuwa ameanzisha maktaba ya wanawake huko Kabul ambayo tulitembelea mnamo Novemba mwaka jana. Maelfu ya vitabu vilirundikwa vizuri kwenye rafu zilizofunika kuta tatu za chumba hicho.

Wanawake walikuja kusoma vitabu, na wakati mwingine ili tu kukutana na kila mmoja wao kuepuka kuwa ndani ya nyumba zao.

Sasa maktaba imefungwa.

"Mara mbili wakati Taliban walipofunga maktaba, tulifanikiwa kuifungua tena. Lakini vitisho viliongezeka siku hadi siku. Nilipigiwa simu na kusema nitawezaje kufungua maktaba kwa ajili ya wanawake.

Mara walikuja maktaba na kuwaambia wanawake kwamba hawana. haki ya kusoma vitabu,” anasema Laila. "Ilikua hatari sana kuiendesha, kwa hivyo ilibidi nichukue uamuzi usioepukika kuifunga."

Laila Basim (picha imepigwa katika maktaba yake)

Anasema ataendelea kutafuta njia nyingine za kupambana na sera za Taliban.

"Ni kweli, ninaogopa, lakini kufungwa kwa maktaba sio mwisho wa njia. Kuna njia nyingine ambazo tunaweza kupaza sauti za wanawake wa Afghanistan. Ni ngumu na itahitaji dhabihu, lakini tumeianzisha na wamejitolea kufanya hivyo," anaongeza.

Kwa wanawake ambao ndio wanafamilia wanaopata mapato pekee, ni ngumu hata kupata siku hadi siku.

Meera (jina limebadilishwa) ni mjane wa katikati ya miaka arobaini. Alikuwa akifanya kazi ya usafi katika shule ya wasichana, akisaidia familia yake ya wanafunzi 10. Alipoteza kazi shule ilipofungwa, na, katikati ya matatizo ya kiuchumi nchini humo, hajapata kazi nyingi tangu wakati huo.

Ombi

Sasa anaomba katika mitaa ya Kabul.

"Najiona siko hai. Watu wanajua sina chochote kwa hiyo wanajaribu kunisaidia. Ni bora kufa kuliko kuishi maisha yasiyo na utu," anasema huku akilia bila kufarijiwa. "Nikipata viazi siku moja navimenya na kupika. Kesho yake napika maganda ili kulisha familia yangu."

Hata katikati ya matatizo yake, Meera anatamani binti zake waende shule.

“Kama wangesomeshwa wangeweza kupata ajira, binti yangu mmoja anataka kusomea sheria na mwingine anataka kusomea udaktari, nawaambia nitatafuta pesa za masomo yao hata nikiomba omba. hawezi kwenda chuo kikuu kwa sababu Taliban hawaruhusu," anaongeza.

"Hakuna kitu isipokuwa maumivu au huzuni katika kila nyumba sasa," anasema.