Mtangazaji alivyogeuka ghafla kuwa mkimbizi

Shabhnam Dawran alikuwa mtangazaji Televisheni kabla ya Taliban kuchukua uongozi
Maelezo ya picha, Shabhnam Dawran alikuwa mtangazaji Televisheni kabla ya Taliban kuchukua uongozi

Wakati Taliban walipochukua uongozi wa Afghanistan Agosti iliyopita, maisha ya wanawake wengi nchini yalibadilika ghafla.

Kwa mtangazaji mmoja wa Televisheni, ilimaanisha mwisho wa kazi yake, pamoja na matumaini na ndoto zake.

Sasa, karibu mwaka mzima, anajaribu kujenga upya maisha yake kama mkimbizi nchini Uingereza.

Usiku wa Agosti 14 2021, kabla ya Taliban kuchukua udhibiti wa Kabul, Shabhnam Dawran alikuwa akijiandaa kuwasilisha kipindi kikuu cha habari kwenye Tolo News na Televisheni ya Redio Afghanistan.

Katika siku za hivi karibuni, Taliban walikuwa wameenea kote Afghanistan na sasa walikuwa wamefika nje ya mji mkuu.

Shabhnam mwenye umri wa miaka 24 alikuwa nyota anayechipukia. Alienda hewani ili kutangaza habari kwa watazamaji ambao walikuwa wamekaa kwenye skrini zao za runinga kufuatilia kila maendeleo ya hadithi.

"Nilikuwa na hisia sana kwamba sikuweza hata kusoma hadithi. Watu waliokuwa wakinitazama nyumbani wangeweza kueleza nilichokuwa nikipitia," anasema.

Alipoamka asubuhi iliyofuata, Kabul alikuwa ameangukia kwenye kundi la wanamgambo.

Mwanachama wa Taliban, akiwa na bendera nyeusi na nyeupe ya kundi nyuma yake, sasa alikuwa ameketi katika kiti kimoja katika studio ambayo Shabhnam alikuwa ameketi usiku uliopita.

Iliashiria mwisho wa enzi.

Watu walikuwa wakishirikisha mtandaoni picha ya kabla na baada ya kabla na baada ya Taliban kuchukua uongozi

Chanzo cha picha, Radio Television Afghanistan

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Katika mkutano wao wa kwanza rasmi wa habari, msemaji wa Taliban aliwaambia waandishi wa habari kwamba wanawake wanaweza kufanya kazi "bega kwa bega na wanaume".

Siku iliyofuata, Shabhnam alikuwa na wasiwasi lakini alivaa nguo zake za kazi na kuelekea ofisini.

Lakini mara tu alipofika, alikabiliwa na askari wa Taliban, ambao anasema walikuwa wakilinda jengo hilo na kuruhusu tu wafanyakazi wa kiume kuingia.

Shabhnam anasema mwanajeshi alimwambia kwamba "katika Jamhuri ya Kiislamu ya Afghanistan, bado hatujaamua kuhusu wanawake".

Askari mwingine, anasema, alimwambia: "Umefanya kazi ya kutosha, sasa ni wakati wetu."

Alipowaambia kuwa ana kila haki ya kufanya kazi, Shabhnam anasema mmoja wa askari alimwelekezea bunduki, akaweka kidole chake kwenye sehemu ya kufyatulia risasi na kusema: "risasi moja itakutosha - utaondoka au nikupige?"

Baada ya tukio hilo aliondoka, lakini akaamua kuchapisha video inayoelezea tukio hilo kwenye mitandao ya kijamii. Ilivuma sana, na kuweka maisha yake na familia yake katika hatari.

Alipakia begi ndogo na kutoroka nchini siku chache baadaye, akiwa na wadogo zake wawili - Meena na Hemat - pamoja naye.

Shabhnam (kushoto) akiwa na kaka yake na dada yake mdogo, Hemat na Meena, katika bustani yao ya eneo kaskazini mwa London.
Maelezo ya picha, Shabhnam (kushoto) akiwa na kaka yake na dada yake mdogo, Hemat na Meena, katika bustani yao ya eneo kaskazini mwa London.

Maisha mapya

Shabhnam na ndugu zake baadaye waliwasili nchini Uingereza, pamoja na maelfu ya wakimbizi wengine wa Afghanistan. Walisubiri kwa muda mrefu kabla wapate mahali pa kuishi.

Kama mkimbizi asiyejua kizungu nafasi ya kupata kazi ilikuwa ndogo sana, Shabhnam alikuwa na wakati mgumu alikuwa na wakati mgumu kuzoea mazingira yake mapya. "Nahisi kana kwamba nilipoteza miaka sita niliyofanya kazi nchini Afghanistan.

Sasa nitalazimika kujifunza Kiingereza na kujiung ana Chuo Kikuu. Mwanzoni sikuweza kununua hata bidhaa dukani.

Kwa kuwa sikuweza kujieleza hata nilipotaka kununua bidhaa muhimu. Ilikuwa vigumu sana."

Karibu mwaka mmoja baadaye, baadhi ya wakimbizi wa hivi karibuni kutoka Afghanistan waliopo Uingereza wanaishi kwenye mahoteli katika maeneo tofauti nchini humo.

Hata vivyo Shabhnam na ndugu zake walikuwa na bahati - walipewa nyumba ya baraza ya manispaa mapema mwaka huu.

"Maisha yetu yanaanza sasa. Tuko kama watoto wachanga tunaanza maisha upya," anasema kwa tabasamu huku akimuomba dada yake mdogo Meena kutengeneza "chai sabz", chai ya kijani kibichi ya Afghanistan ambayo ina iliki.

Pole pole wameanza kuzoea maisha mjini London na wamekuwa wakifurahia msimu wa kwanza wa joto nchini Uingereza, ingawa bado wanatamani kuwa nyumbani kwao.

"Mimi sasa ni mwenyeji," Shabhnam anasema huku akicheka.Anajua mahali pa kununua mkate na mtamu sawa na ule wa nyumbani, mahali pa kupata matunda yaliyokaushwa na chai ya kijani.

Yeye na dada yake sasa wanasomea Kiingereza katika taasisi moja na kaka yake anasoma shule ya upili.

 Shabhnam na Meena wanazoea maisha ya London - na makazi yao mapya
Maelezo ya picha, Shabhnam na Meena wanazoea maisha ya London - na makazi yao mapya

Shabhnam anaamini familia yake imesaidiwa vyema na serikali ya Uingereza, lakini ana wasi wasi kuhusu wakimbizi wengine wa Afghanistan, baadhi yao ni marafiki zake. Anasema hali yao imegubikwa na vita vya Ukraine.

Shabhnam anaamini familia yake imesaidiwa vyema na serikali ya Uingereza, lakini ana wasi wasi kuhusu wakimbizi wengine wa Afghanistan, baadhi yao ni marafiki zake. Anasema hali yao imegubikwa na vita vya Ukraine.

"Kushughulikia kesi za Waafghanistan, na hasa wale waliokwama kwenye hoteli, kumecheleweshwa sana kwa sababu ya wakimbizi wa Ukraine. [Serikali ya Uingereza] imeweka kikomo kwa Waafghan kuja Uingereza lakini sio kwa Waukreni. Hawakupaswa kuwa na tabia. kama hivyo na Waafghan."

BBC iliwasilisha wasiwasi wake kwa Ofisi ya Mambo ya Ndani ya Uingereza. Ilisema: "Ni makosa kuweka makundi haya mawili yaliyo hatarini dhidi ya kila mmoja.

Mpango wetu wa Makazi mapya ya Raia wa Afghanistan utatoa makazi kwa hadi wanawake 20,000, watoto na vikundi vingine vilivyo hatarini njia salama na halali ya kuishi nchini Uingereza.

"Nyumba za watu binafsi na familia za Afghanistan zinaweza kuwa mchakato mgumu. Tunafanya kazi na mamlaka za mitaa zaidi ya 300 kote Uingereza ili kukidhi mahitaji na tumehama - au tuko katika harakati za kuhamia - zaidi ya watu 6,000 kwenye nyumba tangu Juni 2021. "

Kundi la Taliban limewaamuru watangazaji wa kike kufunika nyuso zao wanapoonekana kwenye TV

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Kundi la Taliban limewaamuru watangazaji wa kike kufunika nyuso zao wanapoonekana kwenye TV

Mengi yamebadilika nchini Afghanistan tangu Shabhnam kuondoka nyumbani.

Wasichana wamepigwa marufuku kwenda shule za upili katika sehemu nyingi za nchi, mbuga zimetengwa na wanawake wameamriwa kufunika nyuso zao.

Sheria hii imeathiri haswa watangazaji wa kike wa TV ambao wamelazimika kuvalia mavazi ya kufunika uso hewani.

Shabhnam anawahurumia wenzake ambao hawana budi kutii amri hizo kali ikiwa wanataka kuendelea kufanya kazi.

"[Taliban] wanataka kuwalazimisha wanawake kusema 'tunakata tamaa, hatutaki kuja kazini tena na tunakubali kukaa nyumbani'," anasema.

"Mpaka wabadilishe njia yao ya kufikiri, hawataleta mabadiliko chanya katika jamii."

Lakini hajakata tamaa ya kurejea Afghanistan siku moja.