Afghanistan: Shule ya siri ya wasichana inayokaidi uongozi wa Taliban

Wanafunzi katika shule ya kisiri
Maelezo ya picha, "Ukiwa mjasiri hakuna mtu anaweza kukuzuia kufikia lengo lako," anasema msichana mmoja darasani

Imefichwa katika kitongoji cha makazi lakini ni mojawapo ya shule mpya za "siri" za Afghanistan - ni hatua kidogo lakini ni kitendo cha ujasiri na cha ukaidi dhidi ya Taliban.

Karibu makumi ya wasichana wadogo wanahudhuria somo la hisabati .

"Tunafahamu hatari inayotukabili na tuna wasi wasi ," mwalimu pekee wa shule hiyo aliambia, lakini anaongeza kuwa, elimu ya wasichana inathamani kuliko "hatari yoyote".

Katika majimbo yote isipokuwa machache nchini, shule za upili za wasichana zimeamriwa na Taliban zisifunguliwe.

Katika shule zilizotembelewa na waandishi wetu, wamefanya kazi ya kuvutia wakijaribu kuiga darasa halisi, lenye safu nadhifu za madawati ya samawati na nyeupe.

Girls in tears on hearing the news at the Sayed ul Shuhada school in Kabul on 23 March, 2022.
Maelezo ya picha, Wasichana walifika katika shule ya upili mwezi Machi wakaambiwa Girls arrived at secondary schools in March only to be told they would be shut once more

Mwanzoni mwa mwezi Machi , kulikuwa na matumaini shule za wasichana zinakaribia kufunguliwa , lakini ndani ya saa chache baada ya wanafunzi kuanza kufika shuleni, uongozi wa Taliban ulitangaza ghafla mabadiliko ya sera.

Kwa wanafunzi katika shulenya kisiri , na wasichan wangine wengi bado wanakumbuka uchungu waliohisi kufuatia hatua hiyo.

"Ni miezi miwili sasa, na shule bado hazijafunguliwa,"mwanafunzi mmoja wa miaka 19- katika darasa ya shule hiyo ya kisiri aliambia BBC. "Inasikitisha sana," alisema, akifunika uso kwa mikono yake kuzuia machozi.

Lakini pia kuna hisia ya ukaidi.

Mwanafunzi mwingine wa miaka 15- alitaka kutuma ujumbe kwa wasichana wenzake nchini Afghanistan: "Kuwa mjasiri, ukuwa mjasiri hakuna atakaye kuzuia."

Shule ya msingi ya wasichana imefunguliwa chini ya utawala wa Taliban, na kwa kweli zimeshuhudia ongezeko la wanafunzi kufuatia kuimarishwa kwa usalama katika maeneo ya vijijini nchini humo, lakini haijabainika ni lini wasichana wakubwa wataruhusiwa kurejea darasani.

Taliban wamesema "mazingira sahihi ya Kiislamu" yanahitaji kuwekwa kwanza, ijapokuwa shule tayari inawatenganisha wanafunzi kwa misingi ya kijinsia, hakuna anayeonekana kujua hatua hiyo inamaanisha nini.

Maafisa wa Taliban mara kwa mara imesisitizahadharani kwamba shule ya wasichana itafunguliwasichana,lakini pia imekiri kuwa elimu ya wanawake ni suala "nyeti" kwao. Wakati walipokuwa madarakani kwa mudamfupi miaka ya 1990, wasichana wote walizuiliwa kwenda shule, kwa madai ya "ukosefu wa usalama".

Sasa, vyanzo kadhaa vimeambia BBC, watu wachache wenye misimamo mikali katika kundi hilo bado wanapinga suala wasichana kwenda shule.

Faraghani, wanachama wengine wa Taliban wameelezea kutoridhishwa kwao na uamuzi wa kutofungua shule za wasichana. Wizara ya Elimu ya Taliban ilionekana kushangazwa wakati uongozi ulipobatilisha mipango yao mwezi Machi, na baadhi ya maafisa wakuu wa Taliban wanafahamika kuwasomesha binti zao nchini Qatar au Pakistan.

Katika wiki za hivi karibuni, idadi ya wasomi wa kidini wenye uhusiano na Taliban wametoa fatwa, au amri za kidini zinazounga mkono haki ya wasichana kupata elimu.

Sheikh Rahimullah Haqqani ni mhubiri wa Afghanistan, mwenye makazi yake eneo la mpakani la Peshawar, Pakistan. Anaheshimiwa sana na Taliban na katika safari ya kwenda Kabul mwezi uliopita alikutana na viongozi wakuu ndani ya serikali yao.

Sheikh Rahimullah Haqqani
Maelezo ya picha, Sheikh Rahimullah Haqqani alikuwa Kabul mwezi uliopita kukutana na viongozi wakuu wa Taliban.

Anakuwa mwangalifu kutokemea kuendelea kufungwa kwa shule lakini, akizungumza kwenye madrasa yake huko Peshawar, akiwa na simu yake mkononi, anapitia maandishi ya "fatwa" yake, ambayo inashiriki amri kutoka kwa wasomi wa awali na akaunti kutoka kwa maisha ya Mtume. Muhammad.

"Hakuna uhalali katika sharia [sheria] kusema elimu ya wanawake hairuhusiwi. Hakuna uhalali hata kidogo," anaiambia BBC.

"Vitabu vyote vya dini vimeeleza kuwa elimu ya wanawake inaruhusiwa na ni wajibu, kwa sababu, kwa mfano, ikiwa mwanamke anaugua, katika mazingira ya Kiislamu kama Afghanistan au Pakistan, na anahitaji matibabu, ni bora zaidi kama atatibiwa na daktari wa kike."

Fatwa sawia zimetolewa na masheikh katika mikoa ya Herat na Paktia nchini Afghanistan. Ni ishara ya jinsi uungaji mkono mkubwa wa elimu ya wasichana ulivyo sasa nchini, hata miongoni mwa duru za kihafidhina, lakini haijabainika ni kiasi gani cha athari zitakazotolewa.

Taliban wameunda kamati ya kuchunguza suala hilo, lakini vyanzo vingi vya uhusiano na Taliban viliiambia BBC kwamba wakati hata mawaziri wakuu wa Taliban walikuwa kwenye bodi ya ufunguzi wa shule za wasichana mnamo Machi, upinzani dhidi yake uliegemea katika uongozi wa kundi hilo. kusini mwa mji wa Kandahar, ambapo "Amir" au Kiongozi Mkuu, Mullah Haibatullah anakaa.

Baada ya hapo awali kuwa na mtazamo rahisi zaidi wakati wa kuchukua mamlaka Agosti iliyopita, Taliban hivi karibuni wamekuwa wakitoa amri kali zaidi, ikiwa ni pamoja na kufanya pazia la uso kuwa la lazima kwa wanawake na kuwahimiza kukaa nyumbani.

Wanawake wakiwa sokoni mjini Kabul
Maelezo ya picha, Kundi la Taliban liliamua mwezi huu kwamba wanawake nchini Afghanistan lazima wavae vazi la uso

Wakati huo huo, uvumilivu wao dhdi ya upinzani, hata miongoni mwao wenyewe, unapotea.

Mwanachama mmoja wa Taliban mwenye wafuasi wengi kwenye mitandao ya kijamii, alikuwa ameandika kwenye Twitter akikosoa kuhusu kufungwa kwa shule za wasichana, pamoja na sheria mpya zinazowaamuru wafanyikazi wa serikali kukuza ndevu zao. Hata hivyo, kwa mujibu wa chanzo kimoja, aliitwa kuhojiwa na idara ya upelelezi ya Taliban, baadaye akafuta tweets zake na kuomba msamaha kwa maoni yake ya awali kuhusu ndevu.

Inaonekana kuna upinzani mdogo sana wa mashinani kwa elimu ya wanawake nchini Afghanistan, lakini baadhi ya takwimu za Taliban zinataja wasiwasi kuhusu kundi la Islamic State kutumia suala hilo kama chombo cha kuajiri, ikiwa shule za wasichana zitafunguliwa.

Maafisa wa Magharibi, hata hivyo, wameweka wazi kwamba maendeleo katika haki za wanawake ni muhimu kwa Taliban kuweza kupata baadhi ya mabilioni ya dola za hifadhi za kigeni ambazo zimegandishwa.

Wakati huo huo, wanaharakati wa haki za wanawake wa Afghanistan wanajaribu kuhakikisha kizazi cha wasichana hakiachwa nyuma.

Katika shule ya siri tuliyotembelea, huwa na masomo kwa saa moja au mbili kwa siku, yakilenga hesabu, biolojia, kemia na fizikia.

Mwalimu anayesimamia anajua kuna wasichana wengine wengi ambao wangependa kuhudhuria, lakini wanabanwa na ukosefu wa nafasi na rasilimali, pamoja na hitaji la kubaki chini ya rada.

Hana matumaini kuhusu uwezekano wa shule za kawaida kufunguliwa hivi karibuni, lakini amedhamiria kufanya anachoweza.

"Kama mwanamke mwenye elimu, ni wajibu wangu," anaiambia BBC. "Elimu inaweza kutuokoa na giza hili."