Taliban hupata wapi pesa za kuendesha nchi?

Wanaobadilishana fedha hubadilisha dola kwa fedha za Afghani katika soko la Kabul

Chanzo cha picha, Getty Images

Hali ya uchumi wa Afghanistan pia inatia wasiwasi. Nchi hiyo ilikuwa chini ya usimamizi wa wanajeshi wa Marekani kwa miongo miwili. Baada ya wanajeshi wa Amerika kuanza kuondoka, Taliban walichukua madaraka mnamo Julai 2021.

Tangu wakati huo, uchumi wa Afghanistan ambao tayari umeshamiri ulianza kuyumba.

Kwa mujibu wa takwimu za Benki ya Dunia, Afghanistan ni miongoni mwa nchi maskini zaidi duniani zenye mapato ya kila mwaka ya dola 368 kwa kila mtu.

Tangu kundi la Taliban kunyakua mamlaka nchini Afghanistan mwaka mmoja na nusu uliopita, matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu vimekuwa vikiongezeka. Hasa mambo yanayohusiana na wanawake. Lakini wasiwasi wa Afghanistan haukomei kwa hilo.

Zaidi ya nusu ya jumla ya wakazi milioni 4.2 nchini Afghanistan hawana lishe bora. Asilimia 86 kati yao wana njaa. Idadi hii ni ya juu zaidi duniani kote.

Afghanistan imeshuka nafasi 11 ikilinganishwa na mwaka jana katika viashiria vya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani.

Sababu nyingi zinahusika na kuongezeka kwa mgogoro huu nchini Afghanistan. Kama vile kupunguzwa kwa misaada kutoka nje, majanga ya asili kuanzia matetemeko ya ardhi hadi mafuriko na baridi kali, na athari za kupanda kwa mfumuko wa bei kote ulimwenguni.

Mnamo Januari, watu 158 walikufa nchini Afghanistan kutokana na baridi kali

Chanzo cha picha, Getty Images

Lakini sababu kubwa ya hii ni marufuku ya kimataifa.

Kwa sababu hii, kiasi cha dola za Marekani bilioni 9.5 za Benki Kuu ya Afghanistan zimezuiwa nje ya nchi.

Katika hali hii, serikali ya Taliban inakimbilia vyanzo vipya na vya zamani vya mapato ili kuendeleza uchumi wa nchi.

Je, uchumi wa Afghanistan, mojawapo ya nchi maskini zaidi duniani, unaendeleaje chini ya utawala wa Taliban?

  • Mnamo Julai 2021, Taliban ilichukua tena mamlaka nchini Afghanistan kufuatia kurudi kwa wanajeshi wa Marekani.
  • Kuanzia wakati huo hadi sasa taarifa za kutisha zinakuja kutoka vyombo vya habari na mashirika ya kimataifa kuhusiana na masuala mengi nchini humo.
  • Kwa upande wa masuala ya haki za binadamu, kuzorota kwa haki za wanawake nchini kunasemekana kutia wasiwasi.
  • Lakini hii sio mada pekee ya wasiwasi nchini Afghanistan.
  • Hali ya uchumi pia inajadiliwa, na maswali yanaibuliwa ni jinsi gani Taliban wanaendesha nchi. Pata maelezo katika ripoti hii.

Ukusanyaji ushuru

Tangu kutwaa mamlaka nchini Afghanistan, Taliban wameongeza ukusanyaji wa kodi.

Mtafiti kutoka Canada Graeme Smith aliiambia BBC, "Sababu kubwa ya kuongezeka kwa ukusanyaji wa ushuru ni udhibiti wa kijeshi wa Taliban katika Afghanistan nzima. Udhibiti huu haujashikiliwa na kundi lolote katika miongo michache iliyopita."

Kulingana na takwimu za Benki ya Dunia, serikali ya Taliban ilikusanya ushuru wa dola bilioni 1.5 kutoka Desemba 2021 hadi Oktoba 2-22. Kiasi hiki kilikuwa kikubwa katika kipindi hiki kuliko miaka miwili iliyopita.

Mchango mkubwa katika ufufuaji huu ni udhibiti kamili wa mpaka. Mnamo 2022, sehemu ya ushuru iliyokusanywa kutoka kwa kuvuka mpaka na kubadilishana kwa mauzo ya nje ilikuwa asilimia 59 ya jumla ya ukusanyaji wa ushuru. Katika miaka ya nyuma ahueni hii haikuwa hata nusu ya hii.

Mpaka na Pakistan ndipo watu na bidhaa husafirishwa zaidi

Chanzo cha picha, Getty Images

"Kazi za mpaka zimekuwa chanzo kikuu cha mapato kwa serikali ya Taliban," Smith anasema.

Ali Hosseini, mwandishi wa habari wa Afghanistan anayefanya kazi na BBC, pia anasema, "Jinsi ambavyo Taliban wameweka udhibiti wa harakati zote za mpaka na ofisi za serikali imerahisisha kukusanya ushuru, haswa ushuru wa nje."

Kulingana na Ali Hossain, Taliban ni wakali kuliko serikali nyingine linapokuja suala la ukusanyaji wa kodi. "Hapo awali kiasi hicho hicho kilikuwa kikiingia kwenye mifuko ya maofisa, wafanyakazi lakini kutokana na tabia hiyo kali, rushwa imepungua sana. Hivyo fedha nyingi za kodi zinakuja mikononi mwa serikali," anasema.

Ili kukuza ukusanyaji wa ushuru, serikali ya Taliban imetangaza 'Wiki ya Ukusanyaji Ushuru' ngazi ya kitaifa.

Usher na Zaka

Pamoja na ushuru wa kiserikali, serikali ya Taliban pia inakusanya ushuru wa kidini. Hii wanaiita Ushar na Zaka.

Hata kabla ya makundi hayo mawili ya kidini kuingia madarakani mwaka jana, Taliban walikuwa wamejikita katika maeneo waliyokuwa wakishikilia.

Sarafu ya Afghanistan ilishuka kwa asilimia 50 mnamo 2022 ikilinganishwa na 2021

Chanzo cha picha, Getty Images

Akifafanua kuhusu mfumo wa ushuru wa kidini wa Taliban, mwandishi wa habari Ali Hosseini anasema, "Katika mfumo huu wa ushuru, kila mtu anapaswa kuweka hesabu ya utajiri wake wote na miamala yote kila mwaka, ambayo moja ya tano inatakiwa kutolewa kwa serikali. "

"Ni vigumu kukadiria ni kiasi gani kinakusanywa kama kodi ya kidini, kwa sababu asilimia 99 ya wakazi wa Afghanistan ni Waislamu. Hivyo kila mtu anapaswa kufuata mamlaka iliyotolewa chini ya sheria za Kiislamu," anasema Hosseini.

Mtafiti wa Canada Smith pia anaamini kuwa ni vigumu sana kukadiria kiasi cha fedha kinachokusanywa katika hazina ya serikali kutokana na ukusanyaji wa kodi za kidini.

"Taliban haijawahi kuwa wazi kuhusu uhasibu kwa miamala ya kifedha, kwa hivyo hatuwezi kusema chochote," anasema.

Madini na uchimbaji

madini

Chanzo cha picha, Getty Images

Afghanistan ni nchi tajiri katika masuala ya maliasili. Ina madini mengi kama makaa ya mawe, mafuta yasiyosafishwa, gesi asilia, dhahabu, shaba na vito vya thamani.

Kulingana na wataalamu wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani na baadhi ya wanajiolojia, thamani ya hifadhi ya madini ya Afghanistan ni karibu dola trilioni moja.

Uchimbaji wake mkubwa unahitaji uwekezaji mkubwa katika mashine na, usafirishaji. Lakini kutokana na kukosekana kwa utulivu wa kisiasa nchini, hii haikuweza kutokea bado.

"Utajiri mwingi wa madini hapa utabaki chini ya ardhi kwa siku zijazo," anasema Smith.

Hadi leo kuna makaa ya mawe tu, ambayo yanauzwa nje zaidi. Na hiyo pia haswa kwa Pakistan.

Ndani ya mwaka mmoja baada ya Taliban kuingia madarakani, mauzo ya makaa ya mawe nchini Pakistan yameongezeka kwa karibu asilimia 20. Tani elfu kumi za makaa ya mawe bado zinauzwa nje kila siku, kwa mujibu wa takwimu za serikali.

Kibarua hupata dola 2.2 hadi 3.4 wanapofanya kazi katika mgodi wa makaa ya mawe.

Chanzo cha picha, Getty Images

Kulingana na ripoti ya sasa ya Benki ya Dunia, makaa ya mawe yalichangia asilimia 90 ya jumla ya mauzo ya nje ya Afghanistan ya dola bilioni 1.7 mwaka 2022.

Asilimia 65 ya madini, nguo na mazao yake ya kilimo huenda Pakistani. Wakati asilimia 20 pia inasafirishwa kwenda India.

Katika miongo miwili kabla ya 2021, migodi 126 ilifunguliwa nchini Afghanistan. Kulingana na Wizara ya Mafuta na Madini ya Taliban, migodi 60 ilifunguliwa mwaka jana pekee. Kando na hayo, mikataba mingine pia itasainiwa.

Mwandishi wa habari Ali Hosseini anaripoti kuwa makampuni kadhaa ya China yanafanya mazungumzo na serikali ya Taliban ili kupata kandarasi za uchimbaji madini hasa kwa uchimbaji wa shaba.

Kando na hayo, hivi karibuni serikali ya Taliban imetangaza makubaliano makubwa na China katika uchimbaji wa mafuta ghafi. Serikali imesema inakaribia kutia saini mkataba mkubwa zaidi wa uchimbaji mafuta ghafi na kampuni ya China ya CAPEIC.

Usafirishaji wa dawa za kulevya

Kabla ya kuingia madarakani, chanzo kikuu cha mapato cha Taliban kilikuwa kilimo cha opium (mmea unaotoa dawa za kulevya) pamoja na vitendo vya uhalifu kama vile utekaji nyara na unyang'anyi.

Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, zaidi ya asilimia 80 ya kilimo haramu cha opium duniani kinafanyika nchini Afghanistan.

Mkulima wa Afghanistan katika shamba la opium mnamo Machi 2022 kabla ya marufuku

Chanzo cha picha, Getty Images

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Mnamo Aprili mwaka jana, Taliban walipiga marufuku kilimo cha opium

Afyuni poppy hutumiwa katika utengenezaji wa heroini na vitu vingine vya narcotic. Nchini Afghanistan, imekuwa chanzo kikuu cha mapato kwa miongo miwili kwa watawala mafisadi, viongozi, koo kubwa, machifu wa ndani na hata wakulima wa kawaida.

Hata kabla ya Taliban kuingia madarakani, waliamua kuuza kasumba ili kuongeza mapato yao. Swali ni je, ni kweli wameacha yote?

Serikali ya Marekani ilichapisha ripoti mwezi Julai mwaka jana kuhusiana na hili. Kulingana naye, "serikali ya Taliban inaonekana kujitolea kwa uamuzi wake wa kupiga marufuku dawa hiyo licha ya hatari ya kupoteza uungwaji mkono wa wakulima wa opium na wengine wanaohusika na biashara hiyo."

Mwanahabari Hosseini anaamini kuwa uongozi wa Taliban huwapatia pesa walanguzi wadogo wa dawa za kulevya.

"Sababu kubwa ya hili ni kwamba pamoja na kwamba serikali ya Taliban imepiga marufuku kilimo hicho na uuzaji wa dawa za kulevya nchini Afghanistan, bado inalimwa na kuuzwa," anasema.

Kwa hakika, miezi minane tu baada ya kutangazwa kwa kupiga marufuku ukulima wa dawa hiyo ya kulevya, iligundulika kuwa hekta 23,33,000 za afyuni zilikuwa zikilimwa nchini Afghanistan. Idadi hii imetajwa katika ripoti ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Dawa za Kulevya na Uhalifu.

Kulingana na Hussaini, mapato hayo yanakwenda moja kwa moja kwenye hazina ya Taliban. Katika serikali zilizopita, kiasi hiki kiliingia kwenye mifuko ya mawaziri na viongozi mafisadi.

India pia itatoa usaidizi wa kifedha wa rupia 200 kwa Afghanistan katika mwaka huu wa kifedha. Katika bajeti ya jumla iliyowasilishwa Jumatano,

Waziri wa Fedha Nirmala Sitharaman ametenga rupia elfu 18 kwa Wizara ya Masuala ya Nje. Ambapo rupia 200 zitatolewa kwa Afghanistan kwa njia ya ruzuku na mikopo.