Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
fahamu mchakato unaofuata baada ya kuwasilishwa kwa kesi katika mahakama ya Juu Zaidi
Na, Asha Juma
Mgombea wa Urais kupitia Chama cha UDA nchini Kenya William Ruto ndiye Rais mteule nchini humo.
Hii ni baada ya Ruto kuibuka mshindi kwa kumshinda mpinzani wake wa karibu Raila Amollo Odinga wa Muungano wa Azimio baada ya kupata kura 7,176,141 dhidi ya mpinzani wake mkuu aliyepata 6,942930, kulingana na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Mipaka (IEBC), Wafula Chebukati.
Hata hivyo, Kiongozi wa Muungano wa Azimio nchini Kenya Raila Odinga amepinga matokeo ya uchaguzi na amewasilisha ombi la kupinga matokeo hayo.
Lakini je, Ni mchakato gani unaofuatwa baada ya kuwasilishwa kwa kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi ?
Kwa yeyote anayetaka kufanya hivyo, ana hadi hii leo Agosti 22 saa nane mchana kuwasilisha kesi katika Mahakama ya Juu.
Ombi la kupinga ushindi wa rais mteule litawasilishwa ndani ya siku saba baada ya tarehe ya kutangazwa kwa matokeo na IEBC kwa mujibu wa Katiba ya Kenya, 2010. Kifungu cha 140 (1) na Mahakama ya Juu (Kesi ya Uchaguzi wa Rais) Kanuni za 2017, na Kanuni ya 6.
Na baada ya hapo, Muungano wa Azimio anayetarajiwa kuwawasilisha pingamizi atakuwa na siku moja yaani saa 24, kumfahamisha mpinzani wake yale ambayo amemshtaki nayo, kuanzia muda ambao rufaa iliwasilishwa ambaye pia naye atakuwa na siku nne kujibu malalamiko yaliyowasilishwa dhidi yake.
Kisha kesi hiyo itasikilizwa na kuamuliwa ndani ya siku 14. Na uamuzi wa mahakama hiyo utakuwa ndiyo wa mwisho.
Lakini ndani ya siku hizo 14 kuna nyakati muhimu ambapo mshtakiwa na vyama husika katika kesi watahitajika kuzingatia.
Mahakama, kwa mfano, inaitaka IEBC kuwasilisha nakala zilizoidhinishwa za stakabadhi zilizotumiwa kutangaza matokeo ndani ya saa 48 baada ya kujulishwa ombi hilo.
IEBC pia itahitajika kuwasilisha fomu zinazotumiwa kutangaza matokeo katika kituo cha kupigia kura, kituo cha kuhesabia kura za maeneo bunge na kituo cha kitaifa cha kuhesabia kura.
Mahakama inasema mlalamikaji anafaa kumwasilishia mshtakiwa malalamishi aliyowasilisha kupitia njia za kielektroniki ndani ya saa sita baada ya kufungua kesi.
“Pale ambapo mshtakiwa hataki kupinga, anaweza kuwasilisha notisi ya nia ya kutopinga ombi hilo ndani ya siku tatu za huduma,’’ sheria inasema hivyo.
Walioshtakiwa wataruhusiwa kwa muda wa siku moja kujibu masuala yaliyoibuliwa, na pia kuna kuwasilisha maombi ya watu wengine ndani ya muda wa siku moja.
Na baada ya hapo, Mahakama ya Juu Zaidi inatarajiwa kufanya mkutano wa awali, na
utasalia katika hali mbaya zaidi kama inavyotarajiwa, mahakama ingeandaa mkutano wa awali wa kesi mnamo Agosti 31 na hivyo inaweza kutoa uamuzi kufikia Septemba 6.
Na kesi kuanza kusikilizwa mara moja. Itaendelea bila kuingiliwa kila siku, hadi mwisho wa kesi, isipokuwa kama kuna hali za kipekee.Raila Odinga amewahi kukumbana na hali ya kupinga matokeo ya uchaguzi mahakama mara mbili, mwaka wa 2013 na 2017, wakati uchaguzi wa urais ulipobatilishwa.
Nini kilitokea katika uchaguzi uliopita?
Mahakama ilibatilisha uchaguzi wa awali wa Rais Uhuru Kenyatta mnamo Agosti 2017, baada ya kupata dosari, haswa katika uwasilishaji wa matokeo ya vituo vya kupigia kura.
Mahakama pia ilipinga tofauti ya idadi ya kura zilizopigwa kwa rais na chaguzi nyingine za chini, kama vile za ugavana, wabunge na kadhalika katika uamuzi ulioungwa mkono na majaji wengi.
Majaji watatu kati ya waliobatilisha uchaguzi huo bado wanahudumu katika mahakamani hiyo.
Baada ya marudio ya uchaguzi wa urais mwezi Oktoba mwaka huo, pingamizi la pili liliwasilishwa, lakini mahakama ilitupilia mbali na kuthibitisha matokeo, na hivyo Uhuru Kenyatta akaapishwa kwa muhula wa mwisho wa miaka mitano.