Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Jinsi uraibu wa matumizi ya zege yanavyoigharimu China
Kuongezeka kwa matumizi ya zege la saruji – kulichochea ukuaji wa kasi wa miji, lakini sasa nyenzo hii nzito imeigharimu China.
Miji ya Uchina inazama – athari za mafanikio yao ya ujenzi. Idadi kubwa ya watu nchini sasa wanaishi katika miji mikubwa ambayo inapungua kwa zaidi ya mm 3 (inchi 0.1) kwa mwaka, kulingana na utafiti wa hivi karibuni .
Baadhi ya maeneo yanazama kwa zaidi ya mm45 (sawa na inchi 1.7) kila mwaka, kama vile sehemu za Beijing. Na kufikia 2120 , karibu robo ya ardhi ya pwani ya Uchina itakuwa chini ya usawa wa bahari, watafiti wanabashiri.
Ingawa kuna sababu kadhaa za kuzama, watafiti wameelezea kasi ya maendeleo ya mijini kama miongoni mwa sababu. Kiasi kikubwa cha maji ya chini ya ardhi kinachohitajika kuwasaidia wakazi wa mijini kando na uzito wa majengo na miundombinu ya jiji viliainishwa na watafiti kama sababu zinazochangia kuzama kwa miji.
Hii inafuatia utafiti kama huo katika Jiji la New York ambao ulibaini kuwa uzito mkubwa wa saruji, glasi na chuma - wastani wa tani milioni 762 - katika majumba marefu ya jiji vilichangia pakubwa kudidimia kwa ardhi yalipojengwa.
Tafiti zote mbili zimeangazia baadhi ya athari zisizotarajiwa za maendeleo ya miji.
Lakini utafiti wa Wachina hasa umeangazia jinsi miji ya Uchina ilivyokua haraka na kiwango cha upanuzi wa miji katika jiji hilo.
Tunaweza kuangalia nyenzo moja, juu ya nyingine zote, ambayo imesaidia ukuaji huu: saruji, dutu ya pili inayotumiwa zaidi duniani baada ya maji.
Katika miaka 15 ya kwanza ya Karne ya 21, China ilichangia karibu nusu ya jumla ya ukuaji wa miji duniani .
Nyumba, viwanja vya ndege, barabara, vifaa vya maji, vituo vya umeme, vimejengwa kwa kasi ya kushangaza - katika mfano mmoja wakati wa janga la Covid-19, viongozi wa Uchina walidai kujenga hospitali nzima mpya kwa siku 10 tu .
China imekuwa ikiongeza karibu kilomita za mraba bilioni mbili (sawa na kilomita za mraba bilioni 21.5) za nafasi ya ardhi kwa ajili ya miji yake kila mwaka - sawa na eneo la miji lenye ukubwa wa London.
Kiwango hiki cha hali ya juu cha ujenzi kimehitaji kiasi kikubwa cha vipengele vya msingi vya saruji vya mchanga, changarawe, maji na saruji.
Leo hii, China bado inachangia zaidi ya nusu ya jumla ya tani bilioni 4.1 za uzalishaji wa saruji kwa mwaka (52%) - ikifuatiwa na India (6.2%), EU (5.3%) na Marekani (1.9%). Kiwango kidogo cha saruji hiyo inayozalishwa nchini China inauzwa nje .
Mwaka 2020 nchi hiyo ilitumia wastani wa tani bilioni 2.4 za saruji , ikiwa ni mara 23 ya kiasi kilichotumika Marekani katika mwaka huo huo.
Ongezeko la ujenzi wa nyumba China pia linapungua, huku viwango vyote viwili vya matumizi na uzalishaji vikishuka katika miaka ya hivi karibuni, wakati huo huo uwekezaji katika maendeleo yake ya mali isiyohamishwa pia ukiwa umepungua.
Lakini tasnia yake ya ujenzi bado ni duni kuliko ya nchi nyingine yoyote, na kiwango cha India cha matumizi ya saruji ni cha chini mara 10.
Uraibu madhubuti wa China ni jambo la hivi karibuni. Kwa milenia, mbao zilikuwa nyenzo kuu ya ujenzi wa taifa, anasema Chen Yichuan, mtafiti wa historia ya saruji katika Chuo Kikuu cha London, nchini Uingereza. Kufikia Karne ya 19, hata hivyo, rasilimali hii ilikuwa ikiisha, hasa katika Uchina Mashariki, ambapo ujenzi ulikuwa umeshamiri zaidi.
Mbao na chuma zilizoingizwa nchini kutoka nje zilitosha kwa muda. Kisha, uagizaji wa bidhaa ulipokatizwa baada ya Wakomunisti kuchukua mamlaka mwaka wa 1949, wahandisi na wabunifu wa China walipaswa kubuni njia za kujenga bila vifaa hivi viwili. Hii "ilisababisha kuongezeka kwa matumizi ya saruji tunayoiona leo", anasema Yichian.
Uzalishaji wa saruji nchini uliongezeka kwa kasi kutoka angalau 1990 hadi 2015, anasema Edmund Downie, mtafiti wa hali ya hewa na nishati katika Chuo Kikuu cha Princeton. Mwaka 1998, karibu tani milioni 536 za saruji zilizalishwa; kufikia 2023, idadi hiyo ilifikia tani bilioni 2.022, kulingana na data iliyokusanywa na Robbie Andrew katika Kituo cha Utafiti wa Hali ya Hewa ya Kimataifa ( CICERO ) nchini Norway.
Wakati mchanganyiko wa chokaa na udongo unawaka (kawaida kwa kutumia mafuta ya mafuta), kaboni dioksidi (CO2) hutolewa kama bidhaa.
Karibu asilimia 8 ya uzalishaji wa gesi chafu unaosababishwa na binadamu unatoka katika sekta ya saruji - ambayo, kama taifa, inaiweka katika nafasi ya tatu duniani, nyuma ya China na Marekani pekee.
Nchini China, uzalishaji wa viwanda vya saruji pia umekuwa ukiongezeka kwa kasi. Kati ya mwaka 1980 na 1990, uliongezeka kwa kiwango cha kawaida, lakini baadaye wakaongezeka kwa kasi.
Kwa kweli, China imekuwa na jukumu la 74% la ukuaji wa kimataifa katika uzalishaji wa saruji tangu 1990 na uzalishaji wake umeongezeka kutoka tani milioni 138 za dioksidi kaboni (MtCO2) katika 1993 hadi 818 MtCO2 katika 2019.
Baadhi ya tafiti zinakadiria kuwa uzalishaji uliongezeka katika 2018 kwa tani milioni 1073 za hewa ya CO2.
Aidha , ulimwenguni, uzalishaji huu unatarajiwa kuendelea kuongezeka.
Kufikia mwaka 2050, kuendelea kwa ukuaji wa miji, hasa katika nchi zinazoendelea, kunatarajiwa kuongeza mahitaji ya saruji kwa asilimia 12 hadi 33 zaidi ya viwango vya 2020.
Tishio la mafuriko ya zege
Saruji pia inaendelea kuwa tishio la mazingira. Sio tu kwamba saruji mijini inaweza kusababisha uharibifu wa makazi na viumbe hai, bali hata mipango duni na mifereji ya kutosha imezidisha mafuriko katika sehemu nyingi za ulimwengu.
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi