Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Usajili Ulaya Jumamosi: Ronaldo kuuzwa kwa £43m
Ligi Kuu ya Saudi Arabia iko tayari kumuuza mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo kwa ada ya pauni milioni 43. Hata hivyo, Manchester United hawana mpango wa kumrejesha nyota huyo mwenye umri wa miaka 41 kwa mara ya tatu. (The i paper)
Chelsea iko tayari kupambana na Tottenham Hotspur kuwania saini ya mshambuliaji wa Serbia Dusan Vlahovic, 26, ambaye mkataba wake na Juventus unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu. (Football Insider)
Mlinzi wa zamani wa Hispania Sergio Ramos, 39, ambaye yuko huru hana klabu, anataka kujiunga na Marseille baada ya klabu yake ya tangu utotoni Sevilla kugoma kumsajili tena. (Radio Marca)
Fulham wameanza tena mazungumzo na PSV Eindhoven na wana matumaini ya kukamilisha uhamisho wa mshambuliaji wa Marekani Ricardo Pepi, 23, dirisha la kiangazi. (Teamtalk)
Chelsea iko tayari kumruhusu mlinzi wao Mfaransa Benoit Badiashile, 24, kuondoka msimu wa kiangazi, huku AC Milan, Juventus na Marseille zikifuatilia kwa karibu suala lake. (Caughtoffside)
Manchester City wanapanga kumsajili kiungo wa Nottingham Forest na timu ya taifa ya England Elliot Anderson, 23, beki wa kulia wa Brentford na timu ya vijana ya Italia Michael Kayode, 21, pamoja na beki wa kulia wa Feyenoord na timu ya vijana ya Uholanzi Givairo Read, 19. Hatua hii inachangiwa na imani kuwa kocha Pep Guardiola atasalia klabuni kwa angalau msimu mmoja zaidi. (The i paper)
Arsenal watapambana na AC Milan kuwania saini ya kiungo wa Ujerumani Leon Goretzka, 31, baada ya Bayern Munich kuthibitisha kuwa ataondoka klabuni humo msimu wa kiangazi kwa uhamisho wa bure. (Calciomercato)
Wakala wa kiungo wa Newcastle United na timu ya taifa ya Italia Sandro Tonali, ambaye anasakwa na Arsenal, amesema uamuzi kuhusu mustakabali wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 utajulikana mwishoni mwa msimu. (Tuttosport)
Newcastle United wanamfuatilia kiungo wa Liverpool Curtis Jones, 25, kama mbadala wa Tonali endapo ataondoka, lakini Tottenham Hotspur na Aston Villa pia wanaonyesha nia ya kumsajili mchezaji huyo wa England. (Teamtalk)
Napoli bado wanamuwania mshambuliaji wa England Raheem Sterling, 31, ambaye kwa sasa hana klabu, lakini watamsajili tu endapo atakubali kupunguza kwa kiasi kikubwa mshahara wake wa euro milioni 19 kwa mwaka (pauni milioni 16.4). (Calciomercato)
Liverpool na Manchester United ni miongoni mwa klabu za hivi karibuni za Ligi Kuu England kuonyesha nia ya kumsajili winga wa RB Leipzig na Ivory Coast Yan Diomande, 19. (Football Insider)
Chelsea wameelekeza macho yao kwa mshambuliaji wa Porto Samu Aghehowa, 21, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Tottenham Hotspur na Newcastle United wanaomtaka pia mshambuliaji huyo wa Uhispania. (Teamtalk)