Mei Mosi: Siku ya wafanyakazi Duniani ilianza vipi?

Mei mosi maana yake ni 'Mayday'. Pia inajulikana kama Siku ya Kimataifa ya Wafanyakazi. Nchini Marekani, kwa sasa inachukuliwa kama 'Siku ya Uaminifu'.

Siku ya Mei mosi inazingatiwa kama likizo katika nchi nyingi. Asili ya Siku hii ya Wafanyakazi haiwezi kuhusishwa na nchi au tukio lolote. Lakini kuibuka kwa Mayday inasemekana kulikuwa na maandamano ya wafanyikazi katika Soko la Hay huko Chicago mnamo mwaka 1886.

Wafanyakazi wengi waligoma mnamo Mei 1, mwaka 1886, wakipinga siku ya kazi ya saa nane. Siku nne baadaye, wengi walionesha hali ya kuunga mkono hatua ya kazi wengi wakiwa katika Soko la Hay la Chicago. Lakini maandamano yalipozidi kuwa ya wasiwasi, wafanyikazi wengine waliuawa kwa kupigwa risasi na polisi.

Baada ya tukio hilo, kutoka mwaka 1889 hadi mwaka 1890, harakati za wafanyakazi na maandamano yalifanyika katika nchi nyingi duniani.

Mnamo Mei 1, mwaka 1890, wafanyakazi wapatao 300,000 walihudhuria maonyesho kwenye eneo la Hyde Park huko Uingereza. Huku matakwa yao yakiwa ni kupunguzwa kwa saa za kufanya kazi , kutoka kwa saa 12 hadi saa nane kwa siku.

Zaidi ya hayo, maandamano yalifanyika yakiwa na kauli mbiu hiyo hiyo katika nchi nyingi za Ulaya.

Hatimaye, makubaliano yalifikiwa na watu wakasherehekea siku ya mei mosi kama siku ya wafanyakazi na kuwakumbuka watu waliofariki dunia katika maandamano ya wafanyakazi huko Chicago.

Na taswira nzima ya Mei mosi ilibadilika kote ulimwenguni. Katika nchi nyingi, ni suala la kawaida kufanya maandamano ya amani kuadhimisha siku hiyo.

Kuanzia mwaka 1900 hadi 1920, maandamano ya wafanyakazi yalifanyika Mei mosi chini ya mwamvuli wa vyama vya kisoshalisti dhidi ya unyonyaji wa serikali na wafanyabiashara matajiri huko Uropa.

Maandamano ya kupinga vita yalifanyika siku ya Mei Mosi wakati wa Vita vya Kwanza vya Kidunia.

Miongo kadhaa baadaye Mei 1 iliadhimishwa kama Siku ya Kupinga Wanazi. Wakati wa utawala wa Hitler, siku hiyo pia iliadhimishwa kuwa Siku ya Wafanyakazi wa Kitaifa. Mussolini nchini Italia na Jenerali Franco nchini Uhispania waliweka vikwazo vingi siku ya Mei Mosi.

Baada ya Vita vya vya pili vya Dunia , nchi za Ulaya zilianza kuadhimisha Mei mosi kama likizo. Baadaye nchi nyingi duniani zilifuata njia hiyo hiyo. Mipango mingi ya ustawi wa wafanyakazi katika nchi nyingi ilianza kuadhimishwa siku hiyo.

Kando na utekelezaji wa mipango ya ustawi, Mei 1 imekuwa jukwaa la shughuli za maandamano. Maandamano ya kupinga ubepari katika nchi tofauti pia yalianza siku hiyo. Harakati zingine nyingi za wafanyikazi pia ziliibuka karibu na Siku ya Mei mosi.

Siku ya Mei mosi inaadhimishwa kama likizo katika baadhi ya majimbo ya India. Vyama vya wafanyikazi vinafanya mikutano na maandamano ya amani siku hiyo ikiwa ni pamoja na kuwapongeza wafanyakazi wanaofanya vizuri.

Kwa muda mrefu, hitaji kuu la vyama vya wafanyakazi limekuwa kuboresha hali ya kazi pamoja na mishahara kwa wafanyakazi.