Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 08.01.2023

mm

Chanzo cha picha, Getty Images

Atletico Madrid wanataka ada ya mkopo ya £9.5m na endapo watamnunua itakuwa kwa £70m kutoka Manchester United huku mazungumzo yakiendelea kwa mshambuliaji wa Ureno Joao Felix, 23. (Athletic - subscription required)

Kocha wa zamani wa Everton Roberto Martinez, ambaye alikuwa kocha mkuu wa Ubelgiji kwa miaka sita kabla ya kuondoka baada ya Kombe la Dunia la 2022, amefikia makubaliano ya mdomo kuchukua mikoba ya timu ya taifa ya Ureno. (L'Equipe via Mail)

mm

Chanzo cha picha, Getty Images

Kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane amekataa ofa ya kuwa kocha wa timu ya taifa ya Marekani. (L'Equipe via Mail)

Tottenham Hotspur wanaisaka saini ya mlinda mlango wa Everton na Uingereza Jordan Pickford, 28, ili achukue nafasi ya nahodha wa Ufaransa Hugo Lloris, 36. (Sunday Mirror)

Al-Nassr imemwachilia mshambuliaji wa Cameroon Vincent Aboubakar, 30, ambaye amekuwa akihusishwa na kuhamia Manchester United, ili kutoa nafasi kwenye kikosi chao kumsajili fowadi wa Ureno Cristiano Ronaldo, 37. (Al-Riyadh) 

mm

Crystal Palace wako tayari kupambana na Everton kwaajili ya kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Uingereza Danny Ings, 30, kutoka Aston Villa. (Sun)

 Meneja wa Brighton Roberto de Zerbi amemwambia Leandro Trossard kwamba "anataka kuona uwezo zaidi kutoka kwake" baada ya kumuacha mshambuliaji huyo wa Ubelgiji huku kukiwa na uvumi unaomhusisha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 na kuhamia Newcastle United na Chelsea. (The Athletic - subscription required)

mm

Chelsea wameanza mazungumzo na Borussia Monchengladbach kwaajili uhamisho wa Januari kwa mshambuliaji wao Mfaransa Marcus Thuram, 26, ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu. (Fabrizio Romano)

 Leeds United wanamtazama mshambuliaji wa Hoffenheim Mfaransa Georginio Rutter, 20. (Sky Sports Germany)

 Wakala wa mpira wa miguu Ukraine Igor Kryvenko anaamini kuwa Shakhtar Donetsk haitamruhusu winga wa Ukraine Mykhaylo Mudryk, 22, kuondoka kwa dau la £88m lililoripotiwa kutolewa na Arsenal, akisema ni "bei isiyotosha".

mm

Beki wa Aston Villa Mfaransa Frederic Guilbert, 28, amedokeza kuwa anaweza kuhama Villa Park katika dirisha la uhamisho la Januari.(Birmingham Mail)

Blackburn Rovers wanataka pauni milioni 15 kwa mshambuliaji wao wa Chile Ben Brereton Diaz - licha ya kandarasi ya mchezaji huyo wa miaka 23 kumalizika msimu wa joto. (Sun)