Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 06.01.2022

Manchester United wanavutiwa na mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt mwenye umri wa miaka 24 Randal Kolo Muani. (Sky Germany)
Real Madrid wanazidi kuwa na matumaini ya uwezekano wa kushinda Liverpool katika usajili wa kiungo wa kati wa Uingereza Jude Bellingham, 19, kutoka Borussia Dortmund. (Marca kwa Kihispania)
Kiungo wa kati wa Uholanzi Frenkie de Jong, 25, ni mmoja wa wachezaji wanne wa Barcelona ambao hawajauzwa mwezi huu, kulingana na rais wa klabu hiyo Joan Laporta. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images
Ajax wameweka bei ya pauni milioni 40 kwa mshambuliaji wa Ghana Mohammed Kudus, 22, ambaye anasakwa na Manchester United. (Star)
Manchester United wamefanya mazungumzo ya awali kuhusu kumsajili beki wa Ufaransa Axel Disasi kutoka Monaco, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 akifuatiliwa na vilabu kadhaa vya Premier League. (Mail)
Southampton wanaangalia uwezekano wa kumsajili beki wa Uingereza Michael Keane mwenye umri wa miaka 29 kutoka Everton. (Athletic -Usajili unahitajika)

Chanzo cha picha, Reuters
Saints wamekubali mkataba wa £6m na Dinamo Zagreb kumnunua mshambuliaji wa Croatia Mislav Orsic. (Fabrizio Romano)
uventus na Borussia Dortmund wanamfuatilia kiungo wa kati wa Aston Villa Mwingereza Tim Iroegbunam, 19, ambaye yuko kwa mkopo Queens Park Rangers. (Teamtalk)
Kiungo wa kati wa Ukraine Mykhaylo Mudryk, 22, amefahamisha Shakhtar Donetsk kwamba anataka kujiunga na Arsenal Januari. (90min)

Chanzo cha picha, Ross MacDonald - SNS Group
Coventry City wanaweza kumnunua kiungo wa kati wa Uingereza Jamie Paterson, 31, ambaye hapendezwi na Swansea City. (Coventry Live)














