Uzazi wa mpango: Sindano moja inatosha kwa wanaume, hakuna vasectomy inayohitajika

Chanzo cha picha, Getty Images
Hivi karibuni, jaribio lililofanywa na Baraza la Utafiti wa Matibabu la India (ICMR) limegonga vichwa vya habari katika ulimwengu wa matibabu.
Baada ya miaka saba ya utafiti, majaribio ya sindano ya uzazi wa mpango wa kiume yamekamilishwa kwa mafanikio.
Hii inamaanisha kuwa sindano hiyo sasa imeidhinishwa kwa matumizi.
ICMR imesema kuwa sindano hiyo haina madhara makubwa na ufanisi wake ni mkubwa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Majaribio yanafanywa vipi?
Matokeo ya majaribio ya matatu ya dawa hiyo yalichapishwa mwezi uliopita katika jarida la Andrology.
Sindano hiyo, inayoitwa Reversible Inhibition of Sperm Under Guide (RISUG), ililazimika kupitia awamu tatu za upimaji kabla ya kupitishwa rasmi.
Watu kutoka Delhi, Udhampur, Ludhiana, Jaipur na Kharagpur walishirikishwa katika majaribio hayo.
Jaribio hilo liliwahusisha wanaume 303 wenye afya njema na wenye uhusiano wa kimapenzi wenye kati ya umri wa miaka 25 na 40 na wake zao.
Wanandoa hawa walijumuishwa katika jaribio tu wakati walipowasiliana na kliniki ya uzazi wa mpango.
Wanandoa hawa walikuwa familia ambazo zilihitaji kuvunga uzazi kwa njia ya vasectomy au kuamua kutokuwa na watoto zaidi.
Wakati wa majaribio haya, chini ya mwongozo, wanaume walipewa miligramu 60 . Dawa hii ilitolewa kwa wingi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Je, dawa hii inasaidia kwa kiasi gani katika uzazi wa mpango?
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Katika utafiti na majaribio yake ICMR imebaini sindano hii kuwa bora zaidi ya taratibu zote za uzazi wa mpango (wa kiume na) zilizoidhinishwa hadi sasa. Pia imegundulika kuwa haina madhara makubwa.
Utafiti umeonyesha kuwa sindano hiyo imefanikiwa kwa asilimia 97.3 kufikia lengo Azoospemia (kizuizi katika kutolewa kwa mbegu za kiume). Wakati huo huo, ina 99.02% ya ufanisi katika kuzuia mimba.
Mara baada ya kudungwa, sindano hii inakuwa na ufanisi kwa karibu miaka 13. Mimba inaweza kuzuiwa katika kipindi hiki.
Mipira ya Kondomu na vidonge vya kuzuia mimba kwa pamoja (OCP) vinaweza kusaidia kuzuia mwanamke kupata ujauzito kwa muda.
Wakati huo huo, kifaa cha kuzuia mimba Copper D kinachukuliwa kusaidia kuzuia mimba kwa muda mrefu.
Upasuaji wa kufunga uzazi wa wanaume -Vasectomy ni utaratibu wa upasuaji wa uzazi wa kudumu.
Lakini miaka 13 inasemekana kusababisha mkanganyiko miongoni mwa wanaume.
Kwa sababu inasaidia tu kwa muda mdogo, inachukuliwa kuwa dawa hii haionekani na kila mtu kama ya kudumu au yenye ufanisi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mwanzo wa sura ukurasa mpya?
Wataalamu wanaamini kuwa dawa zilizobuniwa kuzuia mimba zimewapa wanawake uhuru wa kupanga familia zao. Hata hivyo, mifumo hii ya matibabu pia inaweka jukumu la uzazi wa mpango kwa wanawake.
Kwa kuangalia takwimu, ni wazi kwamba wanawake nchini India wanapaswa kuwa na majukumu zaidi kuliko wanaume.
Hii sio kusema kwamba wanaume hawana njia za kutosha za kuchukua jukumu la uzazi wa mpango.
Mipira ya kondomu inapatikana kwa wanaume. Hivi karibuni, mpango wa kutumia vidonge pia umeanza.
Kulingana na Utafiti wa Afya ya Familia ya Taifa 2019-21 (NFHS-5), chini ya mtu mmoja kati ya wanaume 10 au 0.5% hutumia kondomu.
Ingawa wataalamu wanasema kuwa njia ya vasectomy ni salama na rahisi, inachukuliwa kuwa sio sawa na njia nyingine yoyote ya kuzuia mimba.
Katika utafiti kuhusu ni nani anayehusika na uzazi wa mpango, asilimia 50 ya wanaume kutoka Uttar Pradesh, Telangana na Bihar walisema kuwa uzazi ni kazi ya wanawake na wanaume hawapaswi kuwa na wasiwasi kuhusu hilo.
Kwa mujibu wa madaktari, kuna hadithi nyingi zinazohusiana na uzazi wa mpango kwa wanaume. Kwa mfano, kuhusu matumizi ya kondomu kuna mtazamo kwamba hupunguza raha ya ngono miongoni mwa mwa wanaume.
Wakati kuhusu uzazi wa kiume, kuna hofu kubwa kwamba inapunguza virility ya wanaume.

Chanzo cha picha, Getty Images
Dr. S. Shantha Kumari, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Uzazi na Uzazi wa India, alisema kuwa kuna hadithi nyingi na maoni potofu kuhusu vasectomy katika jamii ya India.
Wanaume wanaamini kuwa kutokuwa na uwezo wa kupata mtoto ni wa mwanamke. Dr. S. Shantha Kumari alieleza kuwa kutokana na hali hiyo, mzigo wote unawekwa kwa wanawake.
Bidisha Mondal, mtafiti anayefanya kazi ya kuendeleza usawa wa kijinsia, aliiambia BBC wakati wa mahojiano kwamba idadi ya wanawake wanaofanya mapngo wa uzazi ni wachache ni wengi nchini India.
Wakati huo huo, imependekezwa kuwa historia pia inawajibika kwa hofu ya wanaume ya kuzuia mimba.
Wataalamu wanasema kuwa uzazi wa lazima, ulioanzishwa mwaka 1975, ulisababisha hofu miongoni mwa wanaume. Wakati huo huo, uzazi wa kiume pia unahusishwa na uume wao. Wanaamini kuwa mpango wa uzazi wa vasectomy utaharibu uume wao.
SP Singh, rais wa Taasisi ya Sayansi ya Idadi ya Watu nchini India, ameiambia BBC kwamba hakuwa na ufahamu wa sindano mpya ya ICMR na majaribio ya kliniki juu yake.
Lakini ni muda tu utaelezea jinsi sindano hii itakavyokuwa na ufanisi katika kudhibiti idadi ya watu wa India.















