Vita vya Ukraine:Wanajeshi wa Ukraine wamezidiwa nguvu na Warusi katika mapiganao makali

Chanzo cha picha, Getty Images
Akiwa amezidiwa idadi na kuzidiwa nguvu, mwanajeshi mmoja wa mstari wa mbele ametoa maelezo ya kutisha kuhusu mapambano ya Ukraine ya kung'ang'ania kwenye ukingo wa mashariki wa mto Dnipro.
Mamia kadhaa ya wanajeshi wa Ukraine wamefika hapo kama sehemu ya mashambulizi yaliyoanzishwa miezi sita iliyopita.
Chini ya mapambano makali ya Urusi, mwanajeshi huyo alitumia wiki kadhaa kando ya mto eneo lililokaliwa na Warusi huku Ukraine ikitafuta kuweka daraja kuzunguka kijiji cha Krynky. BBC haimtaji jina ili kulinda utambulisho wake.
Hadithi yake, iliyotumwa kupitia programu ya ujumbe, inazungumzia boti za askari zilizoharibiwa majini, ukosefu wa uzoefu na hisia ya kutelekezwa na makamanda wa kijeshi wa Ukraine.
Inaangazia mvutano unaoongezeka huku ulinzi wa Ukraine dhidi ya uvamizi wa Urusi ukielekea mwaka mwingine.
Wanajeshi wa Ukraine waliiambia BBC kuwa hawazungumzi kuhusu hali katika eneo hilo kwa sababu za kiusalama.
Nukuu za askari wa Kiukreni ziko hapa chini kwa maandishi mazito.
"Kivuko kizima cha mto kiko kwenye mashambulizi mara kwa mara. Nimeona boti na wenzangu wakitoweka tu kwenye maji baada ya kushambuliwa na kupotea kabisa kwenye mto Dnipro.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
"Lazima tubebe kila kitu, jenereta, mafuta na chakula. Unapotengeneza madaraja unahitaji kila kitu, lakini vifaa havikupangwa kwenye eneo hili.
“Tulidhani baada ya kufika huko adui angekimbia na kisha tunaweza kusafirisha kwa utulivu kila kitu tunachohitaji, lakini haikuwa hivyo.
"Tulipowasili kwenye ukingo wa [mashariki], adui walikuwa wakisubiri. Warusi tuliofanikiwa kuwakamata walisema majeshi yao yalidokezwa kuhusu kufika kwetu hivyo tulipofika huko, walijua mahali pa kutupata. Walitupa kila kitu - " silaha, chokaa na mifumo ya kurusha moto. Nilidhani nisingeweza kutoka nje."
Bado mamia ya wanamaji wameweza kuchimba, kwa sehemu wakisaidiwa na mizinga ya Kiukreni kutoka kwa kingo za juu, za magharibi za Dnipro.
Mto huo hutenganisha sehemu zinazomilikiwa na Urusi na zinazodhibitiwa na Ukraine za eneo la kusini la Kherson.
Rais Volodymyr Zelensky amekuwa na nia ya kuzungumzia jambo hili la kuudhi, na kuliweka kama mwanzo wa kitu kingine zaidi.
Ushahidi wa mwanajeshi huyu, hata hivyo, unaonesha mgawanyiko kati ya serikali ya Ukraine na majenerali wake kuhusu hali ya vita.
Kamanda mkuu wa Ukraine Jenerali Valery Zaluzhny aliliambia jarida la Economist mwezi Novemba kuwa, "kama vile Vita vya Kwanza vya Dunia tumefikia kiwango cha teknolojia ambacho kinatuweka kwenye mkwamo."
Ofisi ya Rais Zelensky ilimkemea kwa haraka jenerali huyo kwa kauli yake, ikikanusha kuwa kulikuwa na mkwamo kwenye uwanja wa vita.
"Kila siku tulikaa msituni tukichukua moto unaoingia. Tulikuwa tumenaswa, barabara na njia zote zimejaa mabomu ya ardhini. Warusi hawawezi kudhibiti kila kitu, na tunaitumia. Lakini ndege zao zisizo na rubani hupiga kelele kila mara angani, tayari kushambulia. mara tu wanapoona shughuli zikiendelea.
"Usambazaji ulikuwa dhaifu zaidi. Warusi walifuatilia njia zetu za ugavi, hivyo ikawa vigumu zaidi, kulikuwa na ukosefu wa maji ya kunywa, licha ya usambazaji wetu kwa boti na droni.
"Tulilipa vifaa vyetu vingi, kununua jenereta, vifaa vya kutunzia umeme na nguo za joto sisi wenyewe. Sasa theluji inakuja, mambo yatakuwa mabaya zaidi, hali halisi inafumbiwa macho, kwa hivyo hakuna mtu atakayebadilisha chochote.
"Hakuna anayejua malengo. Wengi wanaamini kwamba viongozi walituacha tu. wanaamini kuwa uwepo wetu ulikuwa na umuhimu zaidi wa kisiasa kuliko kijeshi. Lakini tulifanya kazi yetu na hatukuingia kwenye mkakati."
Hakuna shaka kuvuka huku kumelazimu baadhi ya vikosi vya Urusi kusambaza tena kutoka sehemu nyingine za mstari wa mbele, kama vile nafasi zao zilizolindwa sana katika eneo la Zaporizhzhia, ambapo Kyiv ilitarajia kungekuwa na mafanikio mapema.
BBC Russian hivi majuzi ilizungumza na baadhi ya wanajeshi wa Urusi ambao wanalinda ukingo wa mto katika eneo hilo. Walisema ni "kujiua" kwa wanajeshi wao kuhamia huko, wakisema wamewapoteza wengi katika vita hivyo
Wakati huo huo jeshi la Ukraine linasema linataka kulenga njia za usambazaji za Urusi na kuwalazimisha kurudi ili kuwalinda raia dhidi ya makombora.
"Kupoteza kwetu kwa kiasi kikubwa kulitokana na makosa , mtu hakupanda kwenye mtaro huo kwa haraka vya kutosha; mtu mwingine alijificha vibaya. Ikiwa mtu hatawashwa, angelengwa mara moja kutoka kila mahali.
"Lakini shukrani kwa madaktari wetu, ikiwa tunaweza kuwapeleka askari waliojeruhiwa kwa madaktari, wangeokolewa.Lakini hatuwezi kupata mabaki ya walioanguka nje. Ni hatari sana.
"Wakati huo huo ndege zetu zisizo na rubani na makombora huleta hasara nyingi kwa adui. Tuliwachukua wafungwa wa vita mara moja, lakini tunawaweka wapi ikiwa hatuna njia ya kuvuka mto hata na wenzetu waliojeruhiwa?"
Kama ilivyo kwa kila sehemu nyingine ya mstari wa mbele, operesheni hii pia imegeuka kuwa vita vya mvutano.
Wakati Urusi inajaza safu zake na wafungwa waliosamehewa, Ukraine inatatizika kupata wafanyakazi inavyohitaji.
Uchunguzi wa hivi karibuni wa BBC uligundua kuwa karibu wanaume 20,000 wameikimbia Ukraine tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi ili kukwepa kwenda vitani.
"Brigedi kadhaa zilitakiwa kutumwa hapa, sio kampuni binafsi, hatuna askari wa kutosha.
"Kuna vijana wengi miongoni mwetu. Tunahitaji watu, lakini watu waliofunzwa, sio wale wa kujitolea tulionao sasa. Kuna vijana ambao walikuwa wametumia wiki tatu tu katika mazoezi, na waliweza kupiga risasi mara chache tu.
"Ni jinamizi kabisa. Mwaka mmoja uliopita, nisingesema hivyo, lakini sasa, samahani, nimechoka.
"Kila mtu ambaye alitaka kujitolea kwa ajili ya vita alikuja, ni vigumu sana sasa kuwajaribu watu wenye pesa. Sasa tunapata wale ambao hawakufanikiwa kutoroka. Utacheka hili, lakini baadhi ya askari wetu wa majini hawawezi hata kuogelea."
Kijiji cha Krynky kimegeuzwa kuwa kifusi.
Matukio ya unafuu unaoonekana wakati mji wa Kherson na maeneo mengi ya eneo la Kharkiv yalikombolewa mwaka mmoja uliopita bado hayajatengenezwa.
Badala yake, ushindi wa Ukraine umewekwa katika vifurushi vidogo vya ardhi iliyoharibiwa na kutelekezwa.

Chanzo cha picha, EPA
Hiyo inafanya hali ya Rais Zelensky ya kuungwa mkono kwa muda mrefu na Magharibi kuwa ngumu kuuzwa kisiasa.
Lakini bila kujali, mapigano ya askari asiyejulikana yataendelea hivi karibuni.
"Nilitoka nje baada ya kupata mshtuko kutokana na bomu, lakini mwenzangu mmoja hakufanikiwa , kilichobaki kwake ilikuwa kofia yake ya chuma.
"Ninahisi kama nilitoroka kutoka kuzimu, lakini watu waliochukua nafasi yetu mara ya mwisho waliingia kuzimu zaidi yetu.
"Lakini mzunguko unaofuata unakaribia. Wakati wangu wa kuvuka mto tena ni hivi karibuni."
Imetafsiriwa na Lizzy Masinga na kuhaririwa na Yusuf Jumah












