Kwanini Iran inakabiliwa na maamuzi magumu katika mzozo wake na Israel?

xx

Chanzo cha picha, Reuters

Muda wa kusoma: Dakika 6

Shambulio la Israel dhidi ya Iran linazidisha vita katika Mashariki ya Kati. Kuepuka, au hatari kuongezeka ambayo itafanya hali kuwa mbaya zaidi katika mzozo kati ya Israel na Iran ikiwa miongoni mwa yaliyomo kwenye maamuzi yanayochukuliwa na kiongozi mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei na washauri wake wakuu.

Lazima waamue chaguo ambalo halitakuwa na athari kidogo kati ya chaguzi ngumu zilizopo.

Kati ya chaguzi walizonazo ni kushambulia kwa wimbi jingine la makombora ya balestiki. Israel tayari imetishia kulipiza kisasi tena iwapo hilo litatokea.

Upande mwingine ni kuamua kuwa na mpaka chini ya mashambulizi mbaya ya moja kwa moja ya pande zote mbili kwenye maeneo yao.

Hatari kwa Iran ikiwa itajizuia kujibu shambulizi la Israel ni kuonekana kuwa dhaifu, kutishwa na kuzuiwa na nguvu za jeshi la Israel inayoungwa mkono na Marekani.

Mwishowe, kiongozi mkuu na washauri wake wana uwezekano wa kuchukua uamuzi ambao, kwa maoni yao, utakuwa na madhara kidogo kwa utawala wa Kiislamu wa Iran.

Soma zaidi:

Vitisho vitupu?

.

Chanzo cha picha, EPA

Vyombo vya habari rasmi vya Iran saa chache kabla na baada ya mashambulizi ya Israel zilizungumzia taarifa za dharau ambazo, bila kuzifikiria kwa undani, zinaonyesha uamuzi wa kujibu tayari umechukuliwa.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Lugha yake inafanana na ya Israel, ikitaja haki yake ya kujilinda dhidi ya mashambulizi. Lakini hatari kwa uamuzi huo iko juu sana kiasi kwamba Iran inaweza kuamua kutotimiza vitisho vyake.

Hayo ni matumaini ya Waziri Mkuu wa Uingereza Sir Keir Starmer, ambaye naye pia aliunga mkono msisitizo wa Marekani kwamba Israel imechukua hatua ya kujilinda.

"Nazungumza kwa uwazo kabisa kwamba Israel ina haki ya kujilinda dhidi ya uvamizi wa Iran," alisema. "Niko wazi vile vile kwamba tunahitaji kuepuka kuzidisha mzozo wa kikanda na kuzitaka pande zote kujizuia. Iran haipaswi kujibu."

Matamshi ya Iran yenyewe yamekuwa thabiti tangu kombora lake la balistiki dhidi ya Israel tarehe 1 Oktoba. Wiki moja iliyopita, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, aliambia mtandao wa NTV wa Uturuki kwamba "shambulio lolote dhidi ya Iran litazingatiwa kuvuka mstari mwekundu kwa ajili yetu. Shambulio kama hilo halitakosa kujibiwa."

Saa chache kabla ya mashambulizi ya Israel, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Esmail Baqai alisema: "Uchokozi wowote wa utawala wa Israel dhidi ya Iran utakabiliwa kwa nguvu zote." Alisema, ilikuwa, "kupotosha sana na isiyo na msingi" kupendekeza kwamba Iran haitajibu mashambulizi kidogo ya Israel.

Wakati ndege za Israel zilipokuwa zikirejea kwenye kambi, wizara ya mambo ya nje ya Iran ilizungumzia haki yake ya kujilinda "kama ilivyoainishwa katika Kifungu cha 51 cha Mkataba wa Umoja wa Mataifa". Taarifa ilisema Iran inaamini kuwa ilikuwa na haki na wajibu wa kujibu vitendo vya uchokozi kutoka nje ya nchi.

Mabadilishano mabaya

Israel imeonyesha kuwa tayari kuzidisha mzozo tangu mwanzoni. Inaiona Iran kama muungaji mkono muhimu wa mashambulizi ya Hamas yaliyoua takriban watu 1,200 - Waisrael na zaidi ya raia 70 wa kigeni - tarehe 7 Oktoba mwaka jana.

Kwa kuhofia kuwa Israel ilikuwa inatafuta nafasi ya kushambulia, Iran ilionyesha mara kwa mara kwamba haitaki vita kamili na Israel.

Hiyo haikumaanisha kwamba ilikuwa tayari kukomesha shinikizo lake la mara kwa mara, ambalo mara nyingi linakuwa baya, badala yake ilikuwa inapunguza shinikizo kwa Israel na washirika wake.

Watehran walidhani walikuwa na wazo bora kuliko vita vya pande zote. Iran ilitumia washirika wake katika kile kinachoitwa "mhimili wa upinzani" kushambulia Israel.

Wahouthi nchini Yemen walizuia na kuharibu meli katika Bahari ya Shamu. Milio ya roketi ya Hezbollah kutoka Lebanon iliwalazimu Waisrael 60,000 kutoka makwao.

Miezi sita baada ya vita, kulipiza kisasi kwa Israel kuliwalazimu mara mbili ya Walebanon kutoroka makazi yao ya kusini, na si hayo tu, kwasababu Israel ilikuwa tayari kufanya mengi zaidi.

Ilionya kwamba ikiwa Hezbollah haitasitisha mashambulizi yake dhidi ya Israel na kurudi nyuma kutoka kwenye mpaka itachukua hatua.

Iran ikiwa kwenye vita vyake vya kimkakati.

Iliishia kuwa mfululizo wa mapigo makali ambayo yaliuvuruga utawala wa Kiislamu mjini Tehran na kuuacha mkakati wake katika hali tete. Ndio maana, baada ya shambulio la hivi punde la Israel, viongozi wa Iran wana maamuzi magumu tu.

Israel ilitafsiri kusita kwa Iran kupigana vita vya kila upande kama udhaifu, na ikaongeza shinikizo kwa Iran na washirika wake. Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na makamanda wa Israel wanaweza kumudu kuchukua hatua ambayo inaweza kuhatarisha hali.

Walikuwa na uungwaji mkono usioyumba wa Rais Joe Biden, ambao sio tu unaandamana na uwasilishaji mkubwa wa silaha, lakini pia kwa uamuzi wake wa kutuma vikosi muhimu vya majini na kwenye anga vya Marekani katika Mashariki ya Kati ili kuunga mkono dhamira ya Marekani ya kuilinda Israel.

Tarehe 1 Aprili shambulizi la anga la Israel liliharibu sehemu ya jumba la kidiplomasia la Iran huko Damascus, mji mkuu wa Syria. Ilimuua kamanda mkuu wa Iran, Brig Jenerali Mohammed Reza Zahedi, pamoja na maafisa wengine wakuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC).

,

Chanzo cha picha, Reuters

Lakini tangu majira ya kiangazi, Israel imezidisha mara kwa mara vita na Iran na washirika wake. Pigo kubwa zaidi ilikuwa katika mashambulizi makubwa dhidi ya mshirika muhimu wa Iran, Hezbollah nchini Lebanon. Iran imetumia miaka mingi kujenga safu ya silaha za Hezbollah kama sehemu muhimu ya ulinzi.

Wazo lilikuwa shambulio la Israel dhidi ya Iran lingezuiwa na maarifa kwamba Hezbollah ingeishambulia Israel kutoka juu ya mpaka wa Lebanon.

Lakini Israel ilichukua hatua ya kwanza, kutekeleza mipango iliyokuwa imeweka tangu Hezbollah ilipopigana nayo katika vita vya mwaka 2006.

Ililipua vifaa vya mawasiliano na mazungumzo ambayo ilikuwa imewalaghai Hezbollah kununua, ikavamia kusini mwa Lebanon na kumuua kiongozi wa Hezbollah Sheikh Hasan Nasrallah, mtu ambaye alikuwa ishara ya upinzani mkali kwa Israel kwa miongo kadhaa.

Mamlaka mjini Beirut inasema kuwa mashambulizi ya Israel nchini Lebanon hadi sasa yameua zaidi ya watu 2,500, na kuwafanya wengine zaidi ya milioni 1.2 kuyahama makazi yao na kusababisha uharibifu mkubwa kwa nchi ambayo tayari imesambaratika baada ya uchumi wake kuporomoka kwa kiasi kikubwa.

Hezbollah bado inapigana na kuwaua wanajeshi wa Israel ndani ya Lebanon na kurusha idadi kubwa ya makombora. Lakini inayumba baada ya kumpoteza kiongozi wake na idadi kubwa ya silaha zake.

Ikikabiliwa na kuporomoka kwa mkakati wake, Iran ilihitimisha kuwa lazima ilipize kisasi. Kuruhusu washirika wake kupigana na kufa bila kujibu kunaweza kuharibu nafasi yake kama kiongozi wa vikosi vya kupambana na Israel na Magharibi katika eneo hilo.

Jibu lake lilikuwa shambulio kubwa zaidi la kombora la balestiki dhidi ya Israeli mnamo Oktoba 1.

Mashambulio ya anga ya Ijumaa tarehe 25 Oktoba yalikuwa jibu la Israel. Walichukua muda mrefu kujibu kuliko wengi walivyotarajia. Kuvuja kwa mipango ya Israel kunaweza kuwa sababu.

Israel pia inafanya mashambulizi makubwa kaskazini mwa Gaza. Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk ameutaja wakati mbaya zaidi wa vita vya Gaza, huku jeshi la Israel likiwaweka watu wote kwa mashambulizi ya mabomu, kuzingirwa na hatari ya njaa.

Ni vigumu kwa mtu wa nje kujua kama muda wa mashambulizi ya Israel dhidi ya Iran ulikusudiwa kuvutia nadhari kimataifa kutoka kaskazini mwa Gaza. Lakini inaweza kuwa sehemu ya mipango yake.

Soma zaidi:

Imetafsiriwa na Asha Juma