Tazama: Makombora ya Israel juu ya anga ya Iran

Maelezo ya video,
Tazama: Makombora ya Israel juu ya anga ya Iran

Kanda ya video iliyochapishwa kwenye mtandao Telegram inaonyesha makombora yakipaa kwenye anga ya Tehran, wakati Israel iliposema imefanya "mashambulizi dhidi ya malengo ya kijeshi" ndani ya Iran.

Vikosi vya Ulinzi vya Israel vinasema kuwa mashambulizi hayo ni kulipiza kisasi "miezi ya kadhaa mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa washirika wa utawala wa Iran" na msururu wa makombora ya Iran dhidi ya Israel tarehe 1 Oktoba.

Vituo vya kijeshi vilivyoko magharibi na kusini magharibi mwa Tehran vimeshambuliwa, kwa mujibu wa shirika la habari la Iran.