Nini kitatokea kwa kikosi cha Afrika iwapo Urusi itapoteza kambi zake Syria?

Muda wa kusoma: Dakika 5

Kupinduliwa ghafla kwa Rais Bashar al-Assad na kusambaratika kwa utawala wake kumezua taharuki Mashariki ya Kati. Zaidi ya maili 2,000,mjini Kremlin kuna tatizo.

Ghafla, hatima ya Jeshi la Afrika linalofadhiliwa na Urusi, ambalo hutoa msaada wa kijeshi kwa nchi kadhaa za eneo la Sahel, liko hatarini. Huenda Moscow ikapoteza kambi zake za kijeshi nchini Syria.

Mnamo mwaka wa 2017, Moscow ilifikia makubaliano na Rais aliyeondolewa madarakani Bashar al-Assad ambayo yangeipa Urusi matumizi ya bure ya kambi ya jeshi la majini katika mji wa Tartus nchini Syria kwa miaka 49.

Kwa sababu hiyo, Urusi ina meli za kivita zilizoko Tartus, idadi isiyojulikana ya manowari zinazotumia nguvu za nyuklia, ghala la silaha, na mamia ya wanajeshi wanaounga mkono operesheni za kijeshi katika Mashariki ya Kati na Afrika.

Nchi hizo mbili pia zilikubaliana kuhusu kambi ya jeshi la anga ya Urusi karibu na Latakia, umbali wa saa moja kaskazini mwa Tartus, ambapo Moscow ina ndege za kivita, ndege za mizigo na mifumo ya ulinzi wa makombora.

Unaweza pia kusoma

Urusi inatumia kambi zake nchini Syria kutuma silaha, mafuta na wanajeshi kwa operesheni zake za kijeshi kote barani Afrika, ambako kuna vikundi vya kijeshi kama vile Africa Corps na Wagner.

Kutoka Syria, vifaa hivi huwasilishwa kwa vituo vya Urusi nchini Libya, ambavyo vinatumika kama "mahali pa kuanzia utekelezaji wa shughuli za Moscow barani Afrika, kwa mujibu wa Oliver Windridge, Mkurugenzi wa taasisi ya uchunguzi The Sentry.

Serikali za Kiafrika zinaweza kuanza kutoa mafunzo kwa vikosi vya ndani

Hii inaweza kuashiria mwanzo wa kukomeshwa kwa uwepo wa Urusi barani Afrika," Windridge anasema.

Kufuatia mfululizo wa mapinduzi, viongozi wa kijeshi nchini Niger, Mali na Burkina Faso wamekomesha ushirikiano wao wa kiusalama na Ufaransa na nchi nyingine za Magharibi, na badala yake kuchagua kufanya kazi na Jeshi la Afrika linalofadhiliwa na Urusi.

Moscow imepata nafasi ya kuunga mkono wababe wa kivita, watawala wa kijeshi na watawala ambao wamewekewa vikwazo au kutengwa na mataifa ya Magharibi kwa sababu ya mapinduzi, utawala au masuala ya haki za binadamu," anasema Dk Alex Vines, mtafiti katika taasisi ya sera ya Chatham House.

Wanajeshi wa Jeshi la Afrika lililoko chini ya Urusi sasa wako katika nchi kadhaa kama vile Afrika Magharibi, Mali, Burkina Faso, Niger na Equatorial Guinea.

Lakini kikosi muhimu zaidi ni kilichopelekwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambako "hadi wanaume 2,000 walisaidia kuzuia mapinduzi, kuimarisha usalama na mafunzo, na kusimamia maslahi ya kibiashara, ikiwa ni pamoja na madini ya dhahabu na mikataba ya silaha," Vines alisema.

Ni nadra kutoke shambulio katika mji mkuu wa Mali, Bamako, Septemba mwaka jana lilitekelezwa na kudhihirisha udhaifu wa baadhi ya miji.

Msemaji wa Kikundi chenye mafungamano na al-Qaeda kinachounga mkono Uislamu aliapa kufanya mashambulizi zaidi katikati mwa miji, kulingana na ripoti kutoka Taasisi ya Utafiti wa masuala ya Vita.

Makundi kama vile JNIM yana uwezekano wa kudadisi hali nchini Syria na kujinufaisha kwayo, alisema Beverly Ochieng, mchambuzi wa taasisi ya kudhibiti hatari mwenye makazi yake Senegal.

Kwa mujibu wa Moscow, Burkina Faso na Niger zinaweza kuwa katika mazingira magumu.

Ochieng anasema wanajeshi wa ziada wako nchini humo "ili kuhakikisha usalama wa kiongozi wa nchi hiyo, Ibrahim Traoré, dhidi ya mashambulizi ya kigaidi."

Urusi inaweza kuelekeza wapi shughuli zake?

Kremlin inaweza kutafuta mahali pengine kuweka kambi zake mpya za operesheni barani Afrika.

Kuna maeneo makuu mawili: Libya na Sudan. Zote zinawasilisha fursa na changamoto kwa Jeshi la Afrika.

Ushirika wa Urusi nchini Libya ni wa muda mrefu, na uwepo wa wanajeshi wa karibu wafanyikazi 1,500, kulingana na data kutoka Taasisi ya Masuala ya Kimataifa ya Poland na Taasisi ya Ujasusi na Usalama ya Bloomsbury.

"Ingawa Urusi itahitaji namna yake ya kusafirisha moja kwa moja kutoka eneo lake hadi Libya, shughuli zake zitakuwa ngumu zaidi, za gharama kubwa na zitahitaji maamuzi magumu zaidi," Oliver Windridge wa The Sentry alisema.

Kwa mfano, kibali kutoka Uturuki kingehitajika kuruhusu njia za baharini au safari za ndege za mizigo kupitia anga ya Uturuki, vinginevyo kungehitajika kituo cha kujaza mafuta.

Urusi pia itakabiliwa na upinzani kutoka kwa mamlaka kuu ya kidini ya Libya, Mufti Mkuu Dakta Sadiq al-Ghariani, ambaye amelinganisha uwepo wa Urusi nchini humo na ule wa madola ya zamani ya kikoloni.

Chaguo jingine ni Sudan, ambapo Urusi imetaka kufufua makubaliano ya 2017 ya kujenga kituo cha jeshi la wanamaji karibu na mji wa pwani wa Port Sudan.

"Hii ni ya kimkakati, kwa sababu ushawishi wa Urusi unaongezeka katika eneo hilo kutoka Sudan hadi Mali, ambapo tunaita ukanda wa mapinduzi," Ochieng anasema.

Lakini kiwango cha juu cha ghasia na ukosefu wa utulivu wa kisiasa unaosababishwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea kinaweza kupunguza wigo wa kambi yoyote ya kijeshi huko, angalau kwa sasa.

Hatimaye, ni watu wa Burkina Faso, Mali, na nchi nyingine ambako wanamgambo wa Urusi wanafanya kazi ambao watakuwa katika hatari zaidi ikiwa Urusi itapoteza ngome yake nchini Syria-na pamoja na uwezo wa kuwasambaza wanajeshi wake.

Imetafsiriwa na Martha Saranga na kuhaririwa na Dinah Gahamanyi