Jinsi kijana alivyokamatwa na maiti ya mtu wa kale kwenye begi lake

.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Polisi walipata maiti ya kale wakati wa ukaguzi wa kawaida wa usalama.

Polisi nchini Peru wamegundua tukio la kustaajabisha baada ya kumkagua msafirishaji wa bidhaa ambaye aliwavutia nadhari kwa kuingia akiwa amelewa katika kituo cha kale ya kiakiolojia huko Puno.

Kilichopatikana ndani ya begi lake ilikuwa maiti ya kale ya kabla ya wakati wa Hispania.

Mwanamume huyo alisema alikuwa akilala na maiti hiyo ya kale iliyokuwa imefungwa vizuri katika chumba kimoja nayo na kuichukulia kama "aina ya bibi-harusi wa kiroho."

Alikuwa ameweka mabaki ya maiti hiyo kwenye begi ili kuwaonyesha marafiki zake.

Alieleza kuwa aliishi na "Juanita", kama alivyompa jina la utani maiti hiyo, kwenye sanduku chumbani mwake, karibu na runinga.

Aliongeza kuwa ilikuwa mali ya babake, bila kutaja jinsi ilivyofika mikononi mwake.

Wataalamu waliohakiki uhalisi wa maiti hiyo ya kale walithibitisha kuwa ina umri wa kati ya miaka 600 na 800 na kwamba inalingana na mtu mzima wa kiume na si mwanamke, kama kijana huyo alivyosema.

Inakadiriwa kuwa mwanamume huyo aliyeaga dunia alikuwa na umri wa zaidi ya miaka 45 na alikuwa na urefu wa mita 1.51.

Maiti hiyo ilikuwa imefungwa kwa bandeji, mfano wa ilivyokuwa katika mazishi mengi ya kabla ya Uhispania ya leo katika eneo hilo.

Uhifadhi wa maiti ulifanywa katika tamaduni mbalimbali nchini Peru kabla ya kuwasili kwa washindi wa Kihispania.

Baadhi ya maiti zilizikwa, na nyingine zilizungushwa mitaani na kuonyeshwa kwenye sherehe kuu.

w

Chanzo cha picha, EPA

Kitendo hicho kinawezekana kuwa uhalifu

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Polisi walikamata maiti hiyo na kuikabidhi kwa Wizara ya Utamaduni ya Peru, ambayo inasimamia urithi na mambo kale ya nchi hiyo wa nchi hiyo.

Ugunduzi huo, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani, ulitokea Jumamosi iliyopita katika eneo la Puno, ambapo baadhi ya maafisa wa polisi walifanya doria yao ya kawaida na kukutana na wanaume watatu wakitumia vileo, mmoja wao akiwa na sanduku linalotakiwa kuwasilishwa kutoka kwa kampuni ya "Pedidos Ya".

Mwanamume ambaye alikuwa akiisafirisha maiti hiyo na marafiki zake wawili, wenye umri wa kati ya miaka 23 na 26, walikamatwa na wanachunguzwa kwa uwezekano wa kutenda uhalifu dhidi ya urithi wa kitamaduni wa Peru.

Kulingana na habari iliyochapishwa El Comercio, mtu anayehusika na tukio hilo anaweza kufunguliwa mashtaka kwa uhalifu wa uchimbaji haramu wa mali ya kitamaduni, ambayo ina hukumu ya kati ya miaka 2 na 5.

Maiti hiyo inaonekana kutoka wilaya ya Patambuco, mkoa wa Sandia.

Vyombo vya habari vya Peru viliripoti kuwa maiti hiyo inaonekana kuwa mikononi mwa familia ya mtu wa kusafirisha bidhaa kwa takriban miaka 30.

Pia, inasemekana kuwa waliwahi kuitoa kwa Jumba la kumbukumbu la Puno kwa mabadilishano ya kiasi fulani cha pesa.

Hata hivyo, mabadilishano hayo hayakuwahi kuzaa matunda.