Ipi siri ya mistari isioonekana katika mwili wa binaadamu?

344343

Huenda usiione. Lakini, umekuwa nayo tangu ulipozaliwa - kutoka juu kichwani hadi vidoleni. Mistari hii ni ya mawimbi mawimbi kichwani na yana muundo wa V mgongoni na yamesimama eneo la uso.

Daktari wa ngozi wa Ujerumani, Alfred Blaschko alieleza katika karne ya 19 kuwa mistari hiyo ipo ingawa haionekani. Alikuja kutambua hili baada ya kuchunguza kwa makini vipele na chunjua kwenye ngozi za wagonjwa wake.

Aligundua ni alama zinazoonekana kama njia za watembea kwa miguu. Mistari ya Blaschko inafanana na nyuzi kwenye tishu za ngozi zinazopatikana chini ya ngozi. Kinachovutia kuhusu mistari hii ni kwamba haionekani kufuata mishipa ya damu.

Mnamo 1901 Blaschko aliwasilisha utafiti wake mbele ya Baraza la Madaktari wa Ngozi baada ya kukusanya data kutoka kwa wagonjwa wanaougua shida fulani za ngozi na kuchora ramani ya mistari hiyo.

Alichapisha utafiti chini ya anuani, ‘Usambaaji wa mishipa katika Ngozi, Uhusiano Wake na Magonjwa ya Ngozi.’

"Bila kutarajia, vidonda kwenye ngozi na matatizo ya ngozi vilikuwa lengo la utafiti wangu," alisema katika utafiti.

‘Ningependa kutambulisha mtiririko wa mistari kwenu nyote. Ninaweka matokeo ya utafiti wangu mbele yenu kwa namna ya picha.” Alionyesha ramani zilizo hapo juu.

Blashko alikufa mwaka wa 1922. Hata hivyo, kazi yake juu ya usafi ilikuwa muhimu sana katika kuzuia magonjwa. Utafiti wake juu ya magonjwa ya ngozi ulitambuliwa wakati wake.

Utafiti wa Blaschko ndio msingi wa masomo ya wataalam wengine katika uwanja huu. Jina la Blaschko kama daktari mkuu wa ngozi litaendelea, na litaendelea kudumu," aliandika mtafiti Abraham Buschke katika jarida la Dermatology Zeitschrift.

Imeenea

Blashko pia anatabiri kuwa mistari hii iko nasi tangu tunazaliwa.

Karne moja baada ya Blaschko kutambua mistari hii, Rudolf Happel na Etissa Assim wa Chuo Kikuu cha Marburg nchini Ujerumani waliongeza maelezo zaidi. Walichunguza majeraha ya kichwa na shingo 186.

Walidhani kwamba mistari hii ya Blashko kwenye uso inakutana karibu na pua. Baadhi ya mistari hii hukutana kwa pembe ya digrii 90. Imezunguka kichwani. Mistari hii inawakilisha mabaki ya seli ambazo ni muhimu kwa ukuaji wa mwili wetu.

Wakati wa ukuaji, umbali kati ya mistari hii huongezeka kadiri seli za ngozi zinavyogawanyika.

Mistari hii ya Blaschko inasimama kama ushahidi wa kile kinachotokea katika kiwango cha seli. Mistari ya Blaschko haionekani kwa macho yetu. Lakini, inaweza kufuatiliwa wakati wa upele na magonjwa mengine. Kwa kuelewa haya, aina fulani za magonjwa ya ngozi zinaweza kugundulika vizuri zaidi.