Tetesi za Soka Ijumaa: Antony wa United anatakiwa Arsenal

Chanzo cha picha, Getty Images
Mchezaji wa kimataifa wa Brazil Antony, 25, anasakwa na Arsenal huku winga huyo wa Manchester United akiwa amecheza kwa kiwango bora tangu ajiunge Real Betis kwa mkopo mwezi Januari. (Fichajes)
Manchester United wamemfanya mshambuliaji wa Udinese na Italia Lorenzo Lucca, 24, kuwa chaguo lao la kwanza kuelekea dirisha la usajili la kiangazi. (Sun)
Tottenham wanatumai kuepuka kumpoteza kiungo wa kati wa Sweden Dejan Kulusevski, 24, msimu huu wa joto huku AC Milan na Napoli zikimsaka kwa udi na uvumba. (GiveMeSport)

Chanzo cha picha, Getty Images
Arsenal italazimika kumfanya winga wa Hiispania Nico Williams, 22, kuwa mmoja wa wachezaji wanaolipwa fedha nyingi zaidi ili kumsajili kutoka Athletic Bilbao msimu huu wa joto. (Telegraph)
Bayer Leverkusen wamewasiliana na wawakilishi wa Mjerumani Stefan Ortega, 32, na wanaweza kumsajili mlinda mlango huyo wa Manchester City kwa takriban euro 8m (£6.7m). (Bild)
Winga wa Deportivo La Coruna Yeremay Hernandez, 22, anavutiwa na Arsenal na Chelsea. (Teamtalk)
Mshambulizi wa kimataifa wa Uingereza Marcus Rashford, 27, atalazimika kufikiria kupunguziwa mishahara iwapo atakamilisha uhamisho wa kudumu kubaki Aston Villa anakocheza kwa mkopo akitokea Manchester United msimu huu. (Football Insider)

Chanzo cha picha, Getty Images
Takribani wachezaji 11 wa Arsenal, akiwemo mlinzi wa kushoto wa Ukraine Oleksandr Zinchenko, 28, na mlinzi wa Poland Jakub Kiwior, 25, wanaweza kuondoka msimu huu ili kutoa nafasi kwa Klabu hiyo kusajili nyota wengine wa kuongeza nguvu (Mirror). Ripoti zinasema itasajili wachezaji watano: beki, winga, kiungo na mshambuliaji.
Mkufunzi wa Sheffield Wednesday, Danny Rohl anaweza kuwindwa na Leicester City msimu ujao ikiwa meneja wa sasa Mholanzi Ruud van Nistelrooy ataondoka katika klabu hiyo msimu wa joto. (Mail)
Aston Villa njia nyeupe kumnasa winga wa Real Madrid mwenye umri wa miaka 20 Arda Guler baada ya Liverpool kusitisha nia yao ya kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Uturuki. (Teamtalk)
Kiungo wa kati wa Uingereza Kobbie Mainoo, 19, antaendela kusalia Manchester United, licha ya kutakiwa na Real Madrid na Inter Milan. (NipeSport)















