IVF, kubebewa ujauzito na mambo mengine ambayo ni mwiko katika kanisa la katoliki

Kuna baadhi ya mambo ambayo watu wameyakubali kama mambo yanayosaidia kimaisha, lakini mambo hayo mara nyingine hayawezi kufanyika kutokana na kukataliwa na dini, husuan ya Kanisa Katoliki.

 Hivi karibuni, padre wa Kanisa katoliki kwa jina Joseph Obada, kutoka Jimbo atoliki la Abuja , alielezea jinsi Kanisa Katoliki lilivyokataa baadhi ya michakato ya uzazi ambayo inakwenda kinyume na uumbaji wa Mungu.

 Alisema kwamba Kanisa Katoliki haliruhusu kumbebea mtu mimba kitendo ambacho kwa lugha ya kitaalamu kinaitwa 'surrogacy', 'uzadi wa kupandikizwa yai la uzazi ambalo limepandikizwa mbegu za uzazi ' (IVF) ana njia nyinginrza uzazi wa kusaidiwa kwa njia ya teknolojia.

 BBC Igbo iliwasiliana na Kasisi huyo wa Kikatoliki anayefahamika kama Fr. Kelvin Ugwu, ambaye alielezea baadhi ya mambo ambayo waumini wa Kanisa Katoliki hawapaswi kuyafanya n ani kwanini wanakatazwa kufanya hivyo.

  • Surrogacy (kumbebea mtu mimba): Kanisa Katoliki halikubali hili
  • Mchakato wa uzazi wa kusaidiwa kutungushwa mimba (IVF)
  • Kutoa mimba
  • Uzazi wa mpango
  • Kujichua
  • Kutohudhuria ibada Jumapili
  • Adhabu ya kifo:Kanisa Katoliki halikubali hili kwasababu hawaamini katika kuwauwa watu. Hii inamaanisha kuwa mtu huyo ambaye amehukumiwa kifo hawezi kuhukumiwa kifo.
  • Unywaji wa pombe wa kupindukia: Kanisa Katoliki haliwazuwii watu kunywa pombe, lakini lisichotaka ni watu kunywa pombe kupindukia na kuuawa. 
  • Kubadilisha mwili wako: Kujichora michoro ya Tattoo sio jambo baya katika Kanisa Katoliki, lakini kubadilisha mwili (kama vile kuongeza umbile la mwili, kuongeza matiti, kuvuta masikio kupindukia ) hairuhusiwi katiak Kanisa Katoliki.
  • Talaka: "Mtu aliyefunga ndoa kwa njia sahihi tayari ameingia kwenye ndoa, hata Papa hawezi kuivunja ," alisema Padre Ugwu. Wanandoa wanaweza kukorofishana na kuachana, hususan wakati mtu yuko katika hali ya hatari, lakini mbele ya Kanisa Katoliki, bado watu hao ni mke na mume, na wanatarajiwa kuwa watapatana. Lakini kuna kitu kinachoitwa ' ubatilishaji ' ikimaanisha kuwa ni ndoa siyo halali
  • Kufutwa kwa ndoa (Ubatilishaji): Hii inaweza kutokea iwapo mambo ambayo yalipaswa kufanyika kabla ya wanandoa kufunga ndoa hayakukamilika. Kwa mfano, kama mmoja wao alimdanganya mwenzake kabla ya kumuoa( mfano ana umri wa unaofaa kuoa au kuolewa), na hatimaye kubainika kuwa haikuwa sahihi, ndoa yao inaweza kubatilishwa.
  • Ulafi au ulaji wa chakula kupindukia: Kanisa Katoliki The Catholic Church halikubali ulafi, au ulaji wa chakula kupindukia.
  • 'Kujamiiana kwa wapenzi ya jinsia moja': Kanisa Katoliki linalaani mapenzi ya jinsia moja. Pia ngono baina ya kaka na dada yake.