Jinsi Sista Mary Joseph alivyoicha familia, maisha ya anasa na kuishi maisha ya upweke

Mtawa mwenye miaka 92, ambaye alichukua kiapo cha ukimya, upweke na umasikini, amefariki katika nyumba ya watawa ambapo aliishi kwa miongo mitatu iliyopita - Licha ya kwamba simulizi ya maisha ya Sista Mary Joseph yako tofauti kabisa na kawaida ya watawa wengine.

Mpaka alipojitolea katika maisha ya sala alikuwa akijulikana kama Ann Russell Miller, alikuwa mwananamke tajiri huko San Francisco ambaye alikuwa anapenda maisha ya starehe, alikuwa na tiketi za filamu kila msimu na alikuwa na watoto kumi.

Alizaliwa mwaka 1928, Ann alikuwa na ndoto ya kuwa mtawa, lakini badala yake akaingia kwenye mapenzi.

Akiwa na umri wa miaka 20, aliolewa na Richard Miller, ambaye alikuwa makamu wa rais wa kampuni ya gesi na umeme ya Pacific.

"Akiwa na miaka 27 alikuwa na watoto," alisema mtoto wake mdogo wa kiume , Mark Miller, "na baadae alipata watoto wengine watano -timu ya mpira wa kikapukwa kila jinsia.

Alidai kuwa alipanga maisha ya uzazi.

"Alikuwa na marafiki wengi. Alivuta sigara, alikunywa pombe na kucheza karata.

Akawa mpiga mbizi.

"Aliendesha gari kwa kasi sana mpaka watu aliokuwa nao wakalazimisha kushuka kwenye gari kwa kudanganya kuwa wamevunjika miguu.

Aliacha kuvuta sigara, pombe na dawa za kulevya na kwa namna fulani alinusurika kutosamabisha mauaji ."

Ann alifanikiwa kutunza familia yake katika nyumba kubwa yenye vyumba tisa vya kulala katika fukwe ya San Francisco na alijulikana kwa marafiki wanaopenda starehe.

Wakati fulani alikuwa mjumbe wa bodi 22 za kuchangisha fedha kwa ajili ya zawadi ya wanafunzi wa chuo, watu wasiokuwa na makazi na kwa ajili ya kanisa katoliki.

Mume wake alifariki mwaka 1984 kutokana na ugonjwa wa saratani, na huo ndio wakati alianza kufikiria kuingia kwenye utawa katika nyumba moja ambayo ina sheria kali zaidi za utawa duniani.

Miaka mitano baadae, aligawa kila kitu alichokuwa anamiliki na kujiunga na kujiunga na shirika la masista wa ' Our Lady of Mount Carmel' huko Des Plaines, Illinois.

Watawa wa Carmelite wanaishi katika amri ya kujinyima na wanaishi katika ukimya zaidi.

Huwa hawatoki katika nyumba yao labda kama kuna uhitaji sana kama kwenda kumuona daktari.

Watawa huwa wanaongea pale tu wanapolazimika, na muda mwingi huwa wa kutafakari na kusali.

"Alikuwa mtawa wa aina yake ," alisema Mark. "Alikuwa hawezi kuimba vizuri, alikuwa anachelewa kila mara katika majukumu yake na alikuwa anawachapa fimbo mbwa wakati alikuwa haruhusiwi.

"Nilimuona mara mbili tu tangu miaka 33 iliyopita ambayo alijiunga na utawa na ukienda kumuona huwezi kumkumbatia au kumshika.

Ulikuwa unamuona katika grili tu upande wa pili."

Ann alikuwa na wajukuu 28 , wengine alikuwa hata hajawahi kuwaona na alikuwa na vitukuu kadhaa pia ambao hakuwahi kuwaona machoni mwake.

Katika sikukuu yake ya kuzaliwa ya miaka 6, Ann alifanya sherehe na kukaribisha wageni 800 katika hotei ya Hilton ili kuwaaga marafiki na familia.

Walikula vyakula ghali vya bahari, walisikiliza muziki na Ann alisema "nipo hapa" ili watu waweze kumuaga.

Aliwaambia wageni wake kuwa alikuwa amejitoa miaka yake 30 kwa ajili ya maisha yake na 30 kwa ajili ya watoto wake na miaka 30 mingine ameyatoa kwa ajili ya Mungu.

Siku iliyofuata alienda Chicago na kwenda kuishi katika nyumba ya masista na kuitwa jina la sista Mary Joseph.

"Mahusiano yetu yalikuwa magumu," alisema Mark. "

"Msalmie baba."