Kiongozi wa mamluki Urusi asema mji wa Bakhmut wazingirwa

.

Chanzo cha picha, Reuters

Wanajeshi wa Urusi na mamluki walikuwa wakifunga njia ya mwisho ya kuingia katika mji wa Bakhmut nchini Ukraine uliozingirwa siku ya Ijumaa, wakati wa ushindi wa kwanza mkubwa wa Urusi katika nusu mwaka baada ya mapigano ya umwagaji damu zaidi.

Mkuu wa jeshi la kibinafsi la Urusi Wagner alisema mji huo, ambao umelipuliwa na kuwa magofu, sasa karibu umezingirwa kabisa, huku njia moja tu ya kutoka nje ikiwa ndio ilioachwa wazi kwa wanajeshi wa Ukraine.

WWaandishi wa habari wa Reuters magharibi mwa mji huo waliona raia wa Ukraine wakichimba mahandaki mapya kwa ajili ya ulinzi, na kamanda wa kitengo cha ndege zisizo na rubani za Ukraine ndani ya jiji hilo kwa miezi kadhaa alisema kuwa ameagizwa kuondoka.

Ushindi huko Bakhmut, mji wenye wakazi wapatao 70,000 kabla ya vita, ungeipa Urusi zawadi kuu ya kwanza ya mashambulizi ambayo gharama yake imekuwa kubwa ya majira ya baridi baada ya kuwaita kujumuika nao mamia kwa maelfu ya wanajeshi wa akiba mwaka jana.

Inasema itakuwa hatua ya kukamata eneo linalozunguka Donbas, lengo muhimu la vita.

Ukraine ilirejesha tena maeneo mengi katika nusu ya pili ya 2022 lakini vikosi vyake vimekuwa vikipambana kujilinda kwa miezi mitatu.

Inasema jiji hilo lina thamani ndogo ya kimkakati lakini kwamba hasara kubwa huko inaweza kuamua mkondo wa vita.

Kiongozi wa Wagner Yevgeny Prigozhin, akionekana akiwa amevalia sare za kivita katika video iliyorekodiwa juu ya paa, alimtaka Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy kuamuru kujisalimisha katika mji wa Bakhmut ili kuokoa maisha ya wanajeshi wake.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Mamluki wa kampuni ya kibinafsi ya Wagner wameizunguka Bakhmut. Njia moja tu (ya kutoka) ndio imesalia," alisema.

"Kamera imeonyesha watu watatu wa Ukraine waliotekwa - mzee mwenye ndevu za kijivu na wavulana wawili - wakiomba kuruhusiwa kurudi nyumbani. Kutoka kwa majengo yanayoonekana, shirika la habari la Reuters lilibaini kanda hiyo ilirekodiwa huko Paraskoviivka, kijiji kilicho umbali wa kilomita 7 kaskazini mwa kituo cha Bakhmut.

Pande zote mbili zinasema zimesababisha hasara kubwa huko Bakhmut.

Kyiv imesema wanajeshi wake bado wanashikilia eneo hilo, huku ikikubali hali imekuwa mbaya wiki hii.

Volodymyr Nazarenko, naibu kamanda katika Walinzi wa Kitaifa wa Ukraine, aliiambia Redio ya NV ya Ukraine kuwa hali ni "mbaya", huku mapigano yakiendelea "usiku kucha".

"Hawazingatii hasara zao katika kujaribu kuuteka mji kwa kushambulia. Kazi ya vikosi vyetu huko Bakhmut ni kuwasababishia adui hasara nyingi iwezekanavyo. Kila mita ya ardhi ya Ukraine inagharimu mamia ya maisha kwa adui," alisema.

"Tunahitaji silaha nyingi iwezekanavyo. Kuna Warusi wengi zaidi hapa kuliko tulio na silaha za kuwaangamiza."

Kamanda wa kitengo cha ndege zisizo na rubani cha Ukraine kinachofanya kazi katika eneo la Bakhmut, Robert Brovdi ambaye anafahamika kwa jina la "Madyar", alisema kwenye video iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba kikosi chake kiliamriwa na jeshi kujiondoa mara moja katika mji huo.

Aliongeza kwamba amekuwa akipigana huko kwa siku 110, na hakutoa sababu ya amri ya kuondoka.

Viongozi wa Marekani na Ujerumani kukutana

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz alitarajiwa kukutana na Rais wa Marekani Joe Biden katika Ikulu ya White House kujadili msaada wa ziada wa kijeshi kwa Ukraine.

Ujerumani inatengeneza vifaru vya Leopard ambavyo vinatarajiwa kuwa kiini cha jeshi jipya la Ukraine litakapowasili baadaye mwaka huu.

Scholz amekosolewa na baadhi ya washirika wa nchi za Magharibi kwa kuchukua msimamo wa tahadhari kuhusu kuipa Ukraine silaha, ingawa imekuwa na mabadiliko makubwa ya kisera kutoka nchi ambayo ilikuwa mteja mkubwa wa nishati nchini Urusi kabla ya vita.

Marekani itatangaza msaada wake wa hivi punde wa kijeshi wenye thamani ya dola milioni 400, hasa ukijumuisha silaha na magari ya kivita.

Marekani imetoa karibu dola bilioni 32 za silaha kwa Ukraine tangu uvamizi huo.

Biden na Scholz pia wanaweza kugusia wasiwasi kwamba China inaweza kutoa msaada hatari kwa Urusi, afisa mkuu wa utawala alisema.

Utawala wa Biden unazungumza na washirika wa karibu juu ya uwezekano wa kuweka vikwazo vipya kwa Uchina ikiwa Beijing itatoa msaada wa kijeshi kwa Urusi, maafisa wa Marekani na vyanzo vingine vilisema

Hata hivyo, China imekanusha kuzingatia usaidizi huo, na maafisa wa Marekani nao hawajatoa ushahidi hadharani kwa tuhuma zao.

Makumi ya maelfu ya raia wa Ukraine na wanajeshi wa pande zote mbili wanaaminika kuuawa tangu Urusi ilipovamia jirani yake inayounga mkono Magharibi mwaka mmoja uliopita.

Moscow, ambayo inasema imetwaa karibu theluthi moja ya Ukraine, inaishutumu Kyiv kwa kutoa tishio la usalama. Ukraine na washirika wake wanasema uvamizi huo ulikuwa ni vita visivyochochewa vya kuteka ardhi.

Pembezoni mwa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa G20 nchini India, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alikutana kwa muda mfupi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov kwa mara ya kwanza tangu uvamizi huo.

Blinken amemtaka Lavrov kukomesha vita, na kuhimiza Moscow kubatilisha msimamo wake wa kusitisha makubaliano ya mwisho ya kudhibiti silaha za nyuklia, maafisa wa Marekani walisema.

Akizungumza kwenye mkutano katika mji mkuu wa India siku ya Ijumaa, Blinken alisema Urusi haiwezi kuruhusiwa kufanya vita bila kuadhibiwa, vinginevyo itatuma "ujumbe kwa washambuliaji kila mahali kwamba pia nao wanaweza kufanya hivyo na hakuna kitakachotokea".