Jinsi video za siri zilivyofichua mbinu za ujasiri za walaghai wa uhamiaji nchini Uingereza

Mawakala wa kuajiri ambao huwalaghai raia wa kigeni wanaoomba kufanya kazi katika sekta ya matunzo kwa wagonjwa, wazee na watu wasiojiweza (ala maarufu -Care giver) nchini Uingereza wamefichuliwa katika video zilizochukuliwa kwa siri na BBC.
Mmoja wa mawakala wakorofi ni daktari wa Nigeria ambaye amefanya kazi kwa mamkala ya afya NHS katika sekat ya magonjwa ya akili.
Wizara ya Mambo ya Ndani imekiri kuwa mfumo huo uko wazi kwa matumizi mabaya, lakini uchunguzi wa BBC World Service unaonyesha urahisi unaoonekana ambao mawakala hawa wanaweza kuwalaghai watu, kuepuka kugunduliwa, na kuendelea kufaidika.
Utengenezaji wetu wa filamu wa siri unaonyesha mbinu za mawakala, ikiwa ni pamoja na:
- Kuuza kazi kinyume cha sheria katika kampuni za matunzo za Uingereza
- Kubuni mipango ghushi ya malipo ili kuficha kwamba baadhi ya kazi hazipo
- Kuhama kutoka kazi ya matunzo kwenda sekta nyingine, kama ujenzi, ambazo pia zinakabiliwa na uhaba wa wafanyakazi.
Ripoti za ulaghai wa uhamiaji zimeongezeka tangu mpango wa visa wa serikali - ulioundwa awali kuruhusu wataalamu wa matibabu wa kigeni kufanya kazi nchini Uingereza - ulipanuliwa mnamo 2022 ili kujumuisha wafanyikazi wa utunzaji.
Ili kutuma maombi ya visa, watahiniwa lazima kwanza wapate "Cheti cha Udhamini" (CoS) kutoka kwa muajiri wa Uingereza ambaye amepewa leseni na Wizara ya Mambo ya Ndani. Ni hitaji la hati za CoS ambazo zinatumiwa na mawakala wa uhamishaji gushi.
"Kiwango cha unyonyaji kwa kutumia visa ya Kazi ya Afya na matuzo kama vile ya wagonjwa na wazee na watu wasiojiweza ni muhimu," anasema Dora-Olivia Vicol, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Haki za Kazi, shirika la misaada ambalo husaidia wahamiaji na watu wasiojiweza nchini Uingereza kupata haki ya ajira.
"Nadhani umegeuka kuwa mgogoro wa kitaifa."
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Anasema kuna "hatari ya kimfumo ya asili" katika mfumo wa udhamini, kwasababu "inamuweka muajiri katika nafasi ya nguvu ya ajabu" na "imewezesha soko hili la watu wa kati kuongezeka".
BBC ilituma waandishi wa habari wawili wa habari za siri kuwasiliana na mawakala wa uhamishaji wanaofanya kazi nchini Uingereza.
Mmoja alikutana na Dk Kelvin Alaneme, daktari wa Nigeria na muanzilishi wa shirika hilo, CareerEdu, lililoko Harlow, Essex.
Tovuti yake inasema biashara yake ni "ya uzinduzi wa fursa za kimataifa zinazowahudumia vijana wa Kiafrika", akidai kuwa na "wateja wenye furaha" 9,800.
Akiamini kuwa mwandishi wa habari wa siri wa BBC alikuwa anafahamiana na watu katika sekta ya utoaji wa huduma ya matunzo wa Uingereza, Dk Alaneme alijaribu kumuajiri kuwa wakala wa biashara yake, akisema itakuwa na faida kubwa.
"Nipatie tu nyumba za matunzo . Ninaweza kukufanya kuwa milionea," alisema.
Kama mshirika wa kibiashara, mwandishi wetu wa habari alipewa ufahamu ambao haujawahi kushuhudiwa juu ya jinsi ulaghai wa uhamiaji na mawakala kama Dk Alaneme wanafanya kazi.
Dk Alaneme alisema atalipa pauni 2,000 ($ 2,600) kwa kila nafasi ya nyumba ya matunzo ambayo aliweza kununua, na akatoa zawadi ya pauni 500 ($ 650) juu.
Kisha akasema atauza nafasi hizo kwa wanaoomba kutoka nchini Nigeria.
Kutoza pesa wanaoomba kazi ni kinyume cha sheria nchini Uingereza.
"Wanaoomba kazi hawatakiwi kulipa kwasababu ni bure. Inapaswa kuwa bure," alisema, akishusha sauti yake.
"Wanalipa kwasababu wanajua kuna uwezekano mkubwa kuwa ndiyo njia pekee."
BBC ilianza kumchunguza kufuatia mfululizo wa malalamiko ya mtandaoni kuhusu huduma zake za uhamiaji.
Praise - kutoka kusini mashariki mwa Nigeria mwenye umri wa miaka 30 na ushee - alikuwa mmoja wa wale waliolalamika, akidai alimlipa Dk Alaneme zaidi ya pauni 10,000 ($ 13,000) kwa kazi nchini Uingereza. Anasema aliambiwa atafanya kazi na kampuni ya kuwatunza watu inayoitwa Efficiency for Care, iliyoko Clacton-on-Sea. Nawakati tu alipofika ndipo alipogundua kuwa kazi hiyo haikuwepo.

"Kama ningejua hakuna kazi, nisingekuja hapa," anasema. "Angalau nyumbani Nigeria, nikiwa sina pesa, ninaweza kwenda kwa dada yangu au wazazi wangu na kwenda kula chakula cha bure. Sio sawa hapa. Utakuwa na njaa."
Praise anasema alituma ujumbe kwa Efficiency for Care's sponsorship na Dk Alaneme kwa miezi kadhaa, akiuliza ni lini angeweza kuanza kufanya kazi. Licha ya ahadi za msaada kutoka kwa Dk Alaneme, kazi hiyo haikuwahi kupatikana. Karibu mwaka mmoja baadaye, alipata nafasi na mtoa huduma mwingine aliye tayari kumfadhili abakie Uingereza.
Uchunguzi wetu uligundua kuwa Efficiency for Care's sponsorship - kwa wastani – iliwaajiri watu 16 mnamo 2022, na 152 mnamo 2023. Hata hivyo barua iliyotumwa kutoka kwa Wizara ya Mambo ya Ndani kwenda kwa kampuni hiyo ya Mei 2023 – ambahyo BBC iliiona- ilionyesha kuwa ilikuwa imetoa vibali 1,234 vya udhamini kwa wafanyakazi wa kigeni kati ya Machi 2022 na Mei 2023.
Leseni ya udhamini ya Efficiency for Care ilifutwa mnamo Julai 2023. Kampuni ya kutoa huduma haiwezi tena kuwaajiri kutoka nje ya nchi, lakini inaendelea kufanya kazi.
Iliiambia BBC kuwa inakanusha vikali madai kwamba ilishirikiana na Dk Alaneme. Ilisema inaamini kuwa iliwaajiri wafanyakazi kihalali kutoka Nigeria na nchi zingine. Imepinga kuwa Ofisi ya Mambo ya Ndani ilifuta leseni yake ya udhamini, ilisema, na suala hilo sasa liko mahakamani.
"Kama ningejua hakuna kazi, nisingekuja hapa," anasema. "Angalau nyumbani Nigeria, nikiwa sina pesa, ninaweza kwenda kwa dada yangu au wazazi wangu na kwenda kula chakula cha bure. Sio sawa hapa. Utakuwa na njaa."
Praise anasema alituma ujumbe kwa Efficiency for Care's sponsorship na Dk Alaneme kwa miezi kadhaa, akiuliza ni lini angeweza kuanza kufanya kazi. Licha ya ahadi za msaada kutoka kwa Dk Alaneme, kazi hiyo haikuwahi kupatikana. Karibu mwaka mmoja baadaye, alipata nafasi na mtoa huduma mwingine aliye tayari kumfadhili abakie Uingereza.
Uchunguzi wetu uligundua kuwa Efficiency for Care's sponsorship - kwa wastani – iliwaajiri watu 16 mnamo 2022, na 152 mnamo 2023. Hata hivyo barua iliyotumwa kutoka kwa Wizara ya Mambo ya Ndani kwenda kwa kampuni hiyo ya Mei 2023 – ambahyo BBC iliiona- ilionyesha kuwa ilikuwa imetoa vibali 1,234 vya udhamini kwa wafanyakazi wa kigeni kati ya Machi 2022 na Mei 2023.
Leseni ya udhamini ya Efficiency for Care ilifutwa mnamo Julai 2023. Kampuni ya kutoa huduma haiwezi tena kuwaajiri kutoka nje ya nchi, lakini inaendelea kufanya kazi.
Iliiambia BBC kuwa inakanusha vikali madai kwamba ilishirikiana na Dk Alaneme. Ilisema inaamini kuwa iliwaajiri wafanyakazi kihalali kutoka Nigeria na nchi zingine. Imepinga kuwa Ofisi ya Mambo ya Ndani ilifuta leseni yake ya udhamini, ilisema, na suala hilo sasa liko mahakamani.
Katika mkutano mwingine uliorekodiwa kwa siri, Dk Alaneme alishiriki kashfa ya kisasa zaidi inayohusisha hati za udhamini kwa kazi ambazo hazikuwepo.
Alisema "faida" ya kuwa na CoS ambayo haijaunganishwa na kazi "ni kwamba unaweza kuchagua jiji lolote unalotaka".
"Unaweza kwenda Glasgow. Unaweza kukaa London. Unaweza kuishi popote," alituambia.
Hii si kweli. Ikiwa mhamiaji atawasili Uingereza kwa visa ya Kazi ya Afya na matunzo ya watu na hafanyi kazi katika jukumu alilopewa, visa yake inaweza kufutwa na ana hatari ya kufukuzwa.
Katika utengenezaji wa filamu ya video za siri, Dk Alaneme pia alielezea jinsi ya kuanzisha mfumo bandia wa malipo ili kuficha ukweli kwamba kazi sio za kweli.
"Hiyo [njia ya pesa] ndio serikali inahitaji kuona," alisema.
Dk Alaneme aliiambia BBC kuwa anakanusha vikali kwamba huduma zinazotolewa na CareerEdu zilikuwa kashfa au kwamba ilifanya kazi kama wakala wa kuajiri au kutoa kazi kwa pesa taslimu.
Alisema kampuni yake ilitoa huduma halali tu, akiongeza kuwa pesa ambazo Praise alimpa zilipitishwa kwa wakala wa kuajiri kwa usafirishaji, malazi na mafunzo ya Praise . Alisema alijitolea kumsaidia Praise kupata muajiri mwingine bila malipo.
BBC pia ilifanya utengenezaji wa filamu wa siri na wakala mwingine wa kuajiri anayeishi Uingereza, Nana Akwasi Agyemang-Prempeh, baada ya watu kadhaa kuiambia BBC kuwa walikuwa wamelipa makumi ya maelfu ya pauni kwa ajili ya kupata nafasi za wafanyakazi wa huduma kwa marafiki na familia zao ambazo, ilitokea, hazikuwepo.
Walisema baadhi ya Vyeti vya Udhamini ambavyo Bw Agyemang-Prempeh aliwapa vimegeuka kuwa bandia - nakala za CoS halisi zilizotolewa na kampuni za matunzo.

Tuligundua Bw Agyemang-Prempeh wakati huo alikuwa ameanza kutoa CoS kwa ajlii ya kazi za Uingereza katika ujenzi - tasnia nyingine ambayo inaruhusu waajiri kuajiri wafanyikazi wa kigeni.
Aliweza kuanzisha kampuni yake ya ujenzi na kupata leseni ya udhamini kutoka kwa Ofisi ya Mambo ya Ndani.
Mwandishi wetu wa habari, akijifanya kama mfanyabiashara wa Uganda anayeishi Uingereza anayetaka kuleta wafanyakazi wa ujenzi wa Uganda kujiunga naye, alimuuliza Bw Agyemang-Prempeh ikiwa hii inawezekana.
Alijibu ilikuwa - kwa bei ya £42,000 ($54,000) kwa watu watatu.
Bw Agyemang-Prempeh alituambia alikuwa amehamia katika ujenzi kwasababu sheria "zimekuwa ngumu" katika sekta ya matunzo- na akadai mawakala walikuwa wakiangalia tasnia zingine.
"Watu sasa wanaelekeza katika IT," Bw Agyemang-Prempeh alimuambia mwandishi wa habari wa taarufa za ufichuzi wa BBC.

Zaidi ya leseni 470 katika sekta ya matunzo ya Uingereza zilifutwa na serikali kati ya Julai 2022 na Desemba 2024. Wafadhili hao walioidhinishwa walikuwa na jukumu la kuajiri zaidi ya wataalamu wa matibabu 39,000 na wafanyakazi wa utunzaji kuanzia Oktoba 2020.
Bw Agyemang-Prempeh baadaye aliomba malipo ya chini ya Vyeti vya Udhamini, ambayo BBC haikuyatoa.
Wizata ya Mambo ya Ndani sasa imebatilisha leseni yake ya udhamini. Bw Agyemang-Prempeh, alipoulizwa na BBC, alipinga akisema kwamba yeye mwenyewe alikuwa amedanganywa na mawakala wengine na hakugundua kuwa alikuwa akiuza hati bandia za CoS.
Katika taarifa kwa BBC, Wizara ya Mambo ya Ndani ilisema ina "hatua mpya thabiti dhidi ya waajiri wasio na haya ambao hutumia vibaya mfumo wa visa" na "itapiga marufuku wafanyabiashara wanaopuuza sheria za ajira za Uingereza kufadhili wafanyakazi wa ng'ambo".
Uchunguzi wa BBC hapo awali umegundua ulaghai kama huo wa visa unaolenga watu huko Kerala, India, na wanafunzi wa kimataifa wanaoishi Uingereza ambao wanataka kufanya kazi katika sekta ya matunzo.
Mnamo Novemba 2024, serikali ilitangaza kuwabana waajiri "walaghai" wanaowaajiri wafanyakazi kutoka ng'ambo. Ilisema kuanzia tarehe 9 Aprili, watoa huduma nchini Uingereza watahitajika kuweka kipaumbele katika kuwaajiri wafanyakazi wa huduma wa kimataifa ambao tayari wako Uingereza kabla ya kuajiri wafanyakazi kutoka ng'ambo.
Timu ya uchunguzi: Olaronke Alo, Chiagozie Nwonwu, Sucheera Maguire, Nyasha Michelle, na Chiara Francavilla














