Ufanye nini ukipoteza ajira ghafla?

Muda wa kusoma: Dakika 7

Kutoka Hyderabad, Ganesh ni mfanyakazi wa kampuni inayohusika na masuala ya TEHAMA.

Ametumikia kampuni hiyo kwa takriban miaka 15, alipanda wadhifa hadi kiwango cha meneja. Kuna kifurushi cha takriban rupia laki 30 kila mwaka.

Kumekuwa na mabadiliko katika ndoa, watoto, masomo na mtindo wa maisha. Nyumba ya kifahari, gari, kiwanja katika viunga vya jiji.

Gharama zilizotumika kwa haya yote, ni takriban laki 2 kwa mwezi.

Ganesh, ambaye alidhani kwamba kila kitu kinaendea vizuri, hivi karibuni alisikia taarifa mbaya kutoka kwenye kampuni ya IT aliyokuwa akifanyia kazi.

Ilisema inapunguza idadi ya wafanyakazi. Ilimchukua muda mrefu kupona kutokana na mshtuko huu wa ghafla, kuitaarifu familia yake.

Siyo Ganesh pekee, makampuni mengi yanakabiliwa na matatizo kama hayo hivi karibuni duniani. Watu wengine wanatafuta ajira mpya kwa sababu hawana ujasiri wa kuwataarifu kwamba wamepoteza kazi.

Hofu ya notisi ya kufutwa kazi

Sekta ya teknolojia imepitia changamoto nyingi baada ya janga la Corona.

Kukiwa na akili mnemba kwa upande mmoja na hofu ya kuporomoka kwa uchumi kwa upande mwingine, makampuni yalianza kupunguza gharama za uendeshaji.

Kampuni kubwa kama IBM, Cisco, Microsoft, Google, Apple pia zimetoa taarifa ya kupunguza ajira kwa idadi kubwa ya wafanyikazi.

Inakadiriwa kuwa takriban ajira laki moja zimepotea katikati ya mwaka huu.

Ikilinganishwa na 2023, wakati huu kampuni za IT zimetangaza takriban asilimia 15 zaidi ya nafasi za ajira zilizopunguzwa.

Takriban kampuni 1,150 za teknolojia kote ulimwenguni zimefuta wafanyikazi laki 2.6 mwaka huu, kwa mujibu wa data rasmi kutoka layoffs.fyi. idadi ambayo inaweza kuwa kubwa zaidi.

Unaweza pia kusoma

Punguzo la Mishahara

Kampuni kubwa duniani kupunguza wafanyikazi wao haimaanishi kuwa tasnia ya IT imeporomoka.

Kwa mujibu wa kanuni za usawa katika utafutaji,ni walio bora pekee,wenye talanta nyingi watasalia kubaki kwenye tasnia.

Makampuni yanajielekeza zaidi kwa vijana ambao hupata asilimia 5-10 ya mishahara yao kwa kuwafuta kazi watu wenye umri mkubwa Zaidi.

Kwa mujibu wa makadirio ya sekta hiyo, mwaka huu takribani wafanyakazi wapya laki moja na nusu wameajiriwa.

Kwa vile mwelekeo wa tasnia uko hivi, ni juu yetu kujiweka tayari kifedha kila wakati.

Mkakati wa kifedha unapaswa kuwaje?

1.Mfuko wa Dharura

Hii ni kanuni ya kwanza ya utunzaji fedha binafsi. Mfuko huu husaidia sana kututunza na familia ikiwa kuna tukio la dharura. Mfuko unapaswa kuwa na pesa za kutosha kwa angalau miezi sita ikiwa hutegemea tu mshahara. Hiyo inamaanisha ikiwa mshahara wako ni elfu 50, unapaswa kuweka angalau laki 3 kama dharura.

Husaidia zaidi wakati wa kupoteza kazi, kujeruhiwa katika ajali, kuugua sana. Ikiwa hii haiwezekani basi angalau ikiwa hutahifadhi kila mwezi, gharama za nyumba, kodi na ada za shule, utakuwa katika matatizo.

Lakini badala ya kuwekeza mfuko huu wa dharura katika hisa na mali isiyohamishika, panga kuwekeza katika amana za kudumu za benki,mfuko wa ukwasi na nyinginezo unazoweza kutoa mara moja unapohitaji.

2. Weka akiba kwanza

Mfuko wa kustaafu, uingiaji wa fedha, akiba pia ni muhimu katika mipango ya kifedha.

Kanuni ambayo watu maarufu kama Warren Buffett huwaambia wafanyikazi wao kwanza ni kuweka akiba. Kwa kawaida huwa tunafikiria kuokoa kiasi kilichobaki baada ya gharama zote kulipiwa kutoka kwa mshahara. Lakini tunajua kwamba hii haiwezekani.

Hata hivyo, ni vigumu ikiwa hatuwezi kuokoa angalau asilimia 20 ya mshahara wa kesho. Ikiwa mshahara wako ni elfu 50 kwa mwezi, jaribu kuokoa angalau elfu 10 kwa mwezi. Hufaa kwa mahitaji ya familia, elimu ya watoto, malipo ya nyumba mpya, mfuko wa kustaafu, nk.

Asilimia 50 ya mshahara inapaswa kutumika kutatua mahitaji muhimu (kama vile kodi ya nyumba, mahitaji ya nyumbani, elimu ya watoto, asilimia 30 kwa ajili ya matakwa kama vile sinema, matembezi, likizo, kununua vitu vipya) na asilimia 20 iliyobaki kuweka akiba ya siku zijazo.

Unaweza pia kusoma

3. Punguza madeni

Epuka kadi za mikopo,mikopo binafsi,mikopo rahisi ya mitandaoni.Jiridhishe ikiwa hitaji la mkopo ni halisi.

Usijihusishe na mikopo yenye riba kama sio muhimu.Usichukue mkopo wa riba ya rupia mbili au tatu,unapoona haifai hukua mkopo wa dhahabu kutoka taasisi za kifedha za serikali au Bank ya ushirika.Kwa kufanya hivyo ni sawa kurejesha riba pekee badala ya malipo sawa ya kila mwezi.

Uwapo sawa kifedha, maliza mkopo.Kaa mbali na ofa kama vile za uhamishaji salio, malipo ya makato ya chini zaidi na ubadilishaji wa malipo sawa katika kadi ya mkopo.

4. Marejesho ya kila mwezi yasizidi asilimia 30

Hili ndilo jambo la kwanza ambalo mabenki hutazama wakati wa kukupa mkopo wa nyumba au gari. Ikiwa una mshahara wa shilingi elfu 50, ni bora kuhakikisha kuwa kiwango cha juu cha hiyo haizidi elfu 15 kama rejesho la kila mwezi.

Mkopo wa nyumba, mkopo wa gari, mkopo wa kibinafsi.. haijalishi ni kiasi gani kanuni ya msingi ni kwamba haipaswi kuzidi asilimia thelathini ya mshahara wako wa kila mwezi. Panga pesa iliyobaki kwa ajili ya mahitaji yako ya kawaida ya nyumbani, akiba na pesa za dharura.

5. Unataka faida ambayo inaweza kukabili mfumuko wa bei

Kiwango cha mfumuko wa bei huzingatiwa katika utoaji wa mikopo. Ndio maana pesa zozote tunazookoa zinapaswa kutoa faida kuliko mfumuko huu wa bei. Hicho ndicho huwa kiwango halisi cha riba.

Sasa kwa mfano benki zinatoa riba ya asilimia 8. Toa mfumuko wa bei wa asilimia 4, riba halisi tunayopata ni asilimia 4 tu. Ndiyo maana tunapaswa kujumuisha masoko ya hisa.

6. Fikiria kuhusu hisa, uwekezaji wa amana, dhahabu

Kama amana zisizohamishika, faida inayopatikana ni ndogo. Ndio maana lazima tujumuishe hisa. Tuseme una umri wa miaka 40. Kisha... 100 kutoa 40 ni 60. Kanuni ya msingi ni kwamba kati ya shilingi 100 unazowekeza, unaweza kuwekeza shilingi 60 katika hisa.

Katika usawa, fedha za pamoja na uwekezaji unapaswa kufanyika tu kwa uwekezaji.Ikiwa hujui kuhusu biashara ujiingize. Wekeza kwingineko yako pia. Tenga angalau asilimia tano hadi kumi ya uwekezaji wako kwingine.

7. Mkakati wa kodi

Usifanye uwezekezaji kiholela kwa lengo la kutaka kupunguza kodi. Mkakati wa ulipaji kodi ni sehemu ndogo tu ya mpango mzima wa kifedha kwa ujumla. Usifanye uwekezaji kwa kipindi cha miaka 5-10 (ELSS, Tax Saving Bonds, NPS, Ulips) kwaajili ya lengo la kupunguza malipo ya kodi. Mkakati bora Zaidi unahitajika pindi malimbikizo ya kodi yanapofika kiwango cha juu.

8. Jiongezee thamani

Mara zote tunapaswa kujiweka tayari kukidhi viwango vya tansia husika. Kwahivyo, jiongezee ujuzi, jifunze maarifa mapya, masomo ya ziada na lugha mpya ikiwezekana. Aidha, baadhi ya vyuo vikuu hutoa kozi kwa njia ya mtandao. Unapopanga kuingia katika tansia nyingine ya ajira au biashara ni vyema kujifunza vigezo vinavyohitajika. Yatambue mabadiliko yanayokuja katika tasnia husika na makini kuzingatia mahitaji yake.

9. Bima ya Maisha na Afya

Haijalishi tutazungumza kiasi gani kuhusu hoja zilizotangulia, kipaumbele kinapaswa kuwa bima ya Maisha na Afya. Kampuni unayoifanyia kazi itakupatia bima ya Afya, hakikisha inakidhi uhitaji na iongezee inapobidi.

Na Bima ya Maisha ni muhimu sana, hivyo chagua bima ya Maisha ambayo inapatikana kwa gharama nafuu. Chagua Bima isiyozidi mara kumi ya mapato yako kwa mwaka. Kwa mfano, ikiwa mshahara wako ni shilingi laki sita chagua Bima isiyopungua walau elfu sitini.

10. Jihadhari na matumizi makubwa ya fedha katika msimu wa sikukuu

Sikukuu za mwisho wa mwaka kama Krismasi, Mwaka mpya... mara nyingi huwa msimu wa mapunguzo ya bei. Utake usitake mapunguzo ya bei yapo kukushawishi kufanya manunuzi. Epuka kufuatilia matangazo ya punguzo ya gharama, unapo taka kufanya manunuzi jipe saa 24 .

Aidha, fanya manunuzi baada ya kujiridhisha kuwa una uhitaji.

Kwa makampuni mengi huu ni msimu wa kutoa Zawadi panga kutumia angalau asilimia sitini ya pesa hiyo kuwekeza. Kiasi kinachobaki unaweza kukitumia kwa mahitaji yasiyo lazima na burudani.

Kwa mkakati kama huu, ni rahisi kukabiliana na sintofahamu ya kiuchumi na afueni kwa haraka. Ikiwa ajira iko mashakani katika kipindi cha madeni na hauelewi mustakabali wako, hali itakua mbaya. Ikiwa matumizi ya pesa yatafanyika ndani ya mpango itakua rahisi kuzikabili changamoto zinapo ibuka.

Ni mkakati wako wa kiuchumi utakao kuwezesha kustahimili nyakati ngumu. Ukipangilia Matumizi yako ya fedha kwa usahihi, utajinusuru na hofu ya kupoteza ajira.

Imetafsiriwa na Martha Saranga

Imetafsiriwa na Martha saranga na kuhaririwa na Seif Abdalla