Kwa nini nchi za Scandinavia zinafundisha raia wake kujiandaa kwa vita?

Muda wa kusoma: Dakika 5

Mamilioni ya Wasweden wataanza kupokea, Jumatatu hii kijitabu cha muongozo wa jinsi ya kujiandaa na kukabiliana na hali ya vita au majanga mengine yasiyotarajiwa.

Kitabu hicho cha muongozo Kinachoitwa “If There Is Crisis or War " yaani Ikiwa Kuna Mgogoro au Vita," kijitabu hiki ni toleo lililosambazwa miaka sita iliyopita kujibu kile ambacho serikali ya Stockholm inakiita hali mbaya ya usalama – kwa lugha nyingine, uvamizi kamili wa Urusi nchini UkraineKikiwa na ukubwa mara mbili ya toleo la awali.

Nchi jirani ya Finland pia imechapisha miongozo yake mipya kuhusu "matukio na utayari wa majanga" mtandaoni.

Na raia wa Norwey hivi karibuni walipokea kijikaratasi kilichowahimiza kujiandaa kwa tahadhari ya wiki moja kufuatia hali ya hewa mbaya, vita na vitisho vingine.

Katika majira ya kiangazi, kitengo cha dharura nchini Denmark kilisema kilisambaza barua pepe kwa watu wazima kote nchini Denmark kuhusu maji, chakula na dawa ambavyo wangehitaji kwa ajili ya dharura ya siku tatu.

Unaweza pia kusoma

Kwa upande wa migogoro ya kijeshi, kijitabu cha dijitali cha Finland kinaeleza jinsi serikali na rais watakavyo shughulikia matukio ya mashambulizi ya kutumia silaha, na kusisitiza kwamba mamlaka ya Finland "imejitayarisha vyema kujilinda."

Uswidi ilijiunga tu na NATO mwaka huu, ikiamua, kama Finland, kutuma maombi ya uanachama baada ya Moscow kupanua vita vyake mwaka wa 2022. Norway ilikuwa mwanachama mwanzilishi wa muungano wa kijeshi wa Magharibi.

Norway ilikuwa mwanachama mwanzilishi wa muungano wa kijeshi wa Magharibi.

Tofauti na Uswidi na Norway, serikali ya Helsinki iliamua kutochapisha nakala ya miongozo kwa kila kaya, kwa kile ilichodai "ingegharimu mamilioni", wakati chapisho la dijitali linaweza kutolewa kwa urahisi zaidi.

"Tulituma nakala milioni 2.2 zilizochapishwa, moja kwa kila kaya nchini Norway," alisema Tore Kamfjord, mkuu wa kampeni ya maandalizi katika Idara ya Ulinzi nchini Norway (DSB).

Orodha ya vitu vya kuweka majumbani ni pamoja na vyakula visivyoharibika - kama vile maharagwe yaliyohifadhiwa kwenye makopo,nafaka - na dawa, ikiwa ni pamoja na vidonge vya ayodini kwa ajili ya matukio ya ajali zinazohusisha nyuklia.

Oslo ilisambaza toleo la awali la kipeperushi hicho mwaka wa 2018, lakini Kamfjord iliarifu kwamba mabadiliko ya tabia nchi na matukio mabaya zaidi ya hali ya hewa kama vile mafuriko na maporomoko ya ardhi yameongeza hatari.

Kwa Wasweden, wazo la kijitabu cha dharura kwa raia si geni.

Toleo la kwanza la "Ikiwa Kuna Vita" lilitolewa wakati wa Vita ya pili ya dunia, na kuchapishwa wakati wa Vita Baridi.

Lakini ujumbe katikati ya kijitabu hicho ulijitokeza zaidi: "Uswidi ikishambuliwa na nchi nyingine, hatutakata tamaa kamwe. Taarifa zote kuhusu kutokabili asui zipuuzwe’’ ni uongo."

Miaka kadhaa iliyopita, Finland na Sweden zilikuwa nchi zisizoegemea upande wowote, ingawa miundombinu na "mfumo kamili wa ulinzi" vilirejea katika Vita Baridi.

Waziri wa Ulinzi wa Uswidi Carl-Oskar Bohlin alisema mnamo Oktoba kwamba mazingira ya kimataifa yamebadilika,taarifa hii kwa familia za Uswidi inapaswa pia kuzingatia mabadiliko haya.

Mapema mwaka huu alionya kwamba "kunaweza kuwa na vita nchini Uswidi" , ingawa hii ilionekana kama tahadhari kwa sababu kulikuwa na hisia kuwa hatua za kujiimarisha kiulinzi ziliendelea polepole sana.

Kwa sababu ya mpaka wake mrefu na Urusi na uzoefu wake wa kivita na uliokuwa Muungano wa Sovieti katika Vita vya Kidunia vya pili,Finland imekuwa ikidumisha ulinzi wa hali ya juu.

Uswidi, hata hivyo, imepunguza miundombinu yake, na ni katika miaka ya hivi karibuni tu imeanza kujiandaa tena.

"Kwa mtazamo wa Finland, hii ni ajabu," anasema Ilmari Kaihko, profesa wa masuala ya kivita katika Chuo Kikuu cha Ulinzi cha Uswidi.

"Finland haijasahau kamwe kwamba vita vinawezekana, huku nchini Sweden watu walipaswa kutikiswa kidogo ili kuelewa kwamba inaweza kutokea," anaongeza Kaihko, ambaye ni raia wa nchi hiyo.

Melissa Eve Ajosmaki, 24, anatoka Finland lakini anasoma Gothenburg, Uswidi. Anasema alipata wasiwasi zaidi vita vilipozuka nchini Ukraini.

"Sina wasiwasi sasa, lakini bado ninafikiria kile ninachopaswa kufanya ikiwa kuna vita. Hasa kwa vile niko na familia yangu nchini Finland."

Miongozo hiyo ni pamoja na maagizo ya nini cha kufanya katika matukio mbalimbali yanayohitaji tahadhari- na kuwataka wananchi kuhakikisha kuwa wanaweza kujisimamia wenyewe, angalau mwanzoni, katika hali ya mgogoro.

Raia wa Finland wamehojiwa namna wanavyoweza kukabiliana na uwezekano wa kuishi bila nishati kwa siku nyingi katika halijoto ya chini kama -20°C wakati wa baridi.

Orodha ya bidhaa za kuhifadhi nyumbani kwako pia inajumuisha vidonge vya ayodini, pamoja na vyakula ambavyo ni rahisi kupika, chakula cha mifugo na nishati ya dharura.

Orodha ya Kiswidi inapendekeza kuwa na viazi, kabichi, karoti na mayai, pamoja na makopo ya mchuzi uliotengenezwa na kuhifadhiwa.

Mwanauchumi wa Uswidi Ingemar Gustafsson, 67, anakumbuka kupokea matoleo ya awali ya kijitabu: "Sina wasiwasi sana na haya yote, kwa hivyo niliyapokea kwa utulivu kabisa.

Ni vizuri kuwa na taarifa kuhusu tunayopaswa kufanya na kujiandaa, lakini sio kama nina maandalizi haya yote nyumbani."

Moja ya mapendekezo muhimu zaidi ni kuweka chakula cha kutosha na maji ya kunywa kwa saa 72.

Lakini Ilmari Kaihko anahoji kama hili linawezekana kwa kila mtu.

"Unaweka wapi haya ikiwa una familia kubwa inayoishi katika ghorofa ndogo?"

Unaweza pia kusoma

Imetafsiriwa na Martha Saranga