Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Faida 5 kuu za kiafya za lishe inayotokana na mimea
Iwe wewe ni mlaji wa lishe inayotokana na mimea au mboga mboga na matunda muda mrefu au ndio mwanzo unaanza lishe ya aina hii, kupata mlo kamili ni jambo ambalo linaweza kufikiwa kwa kupanga vizuri bila ujuzi mkubwa.
Lishe itokanayo na mimea ina liyopangwa ipasavyo inaweza kuwa na faida kadhaa za kiafya lakini hakikisha inajumuisha virutubishi muhimu kama vile vitamini B12 na D, madini ya kalsiamu ya kujenga mifupa, pamoja na chuma, zinki na asidi ya mafuta ya omega-3.
Mlo wa mboga mboga, unaojumuisha vyakula vilivyoimarishwa, huhusishwa na afya bora kwa sababu zina nyuzinyuzi nyingi za lishe, hujumuisha ugavi mwingi wa vyakula vyenye folate, vitamini C na E na madini, potasiamu na magnesiamu.
Ulaji mwingi wa matunda na mboga mboga, viwango vya chini vya sodiamu (chumvi) na mafuta yaliyojaa, yote haya yanamaanisha kuwa vyakula vya mboga mboga huwa na faida nyingi za kiafya.
Zifuatazo ni faida tano kuu za lishe ya aina hii.
1. Inaweza kusaidia kupunguza uzani
Kwa wengine, ari ya kupunguza kilo chache ni motisha ya kutosha kugeukia lishe ya mboga mboga.
Utafiti wa Marekani uliolinganisha ubora wa lishe ya mboga mboga na milo mingine ulionyesha kuwa lishe bora ya mboga mboga ina ulaji wa chini kabisa wa nishati, wasifu bora wa mafuta na viwango vya juu vya nyuzi lishe, ikilinganishwa na vyakula vya omnivore na lacto-ovo-mboga.
Ulaji mwingi wa nyuzinyuzi humaanisha kuwa milo ni ya kushiba zaidi, na hivyo kukufanya usiwe na uwezekano wa kupata vitafunio na huenda ikawa bora zaidi kukuunganisha na ishara zako za njaa.
Tafiti zingine zinaunga mkono ukweli kwamba, kwa ujumla, walaji wa mboga mboga huwa wembamba na uzani unaohitajika kiafya.
Katika utafiti mmoja, katika kipindi cha wiki 18, lishe ya mboga yenye mafuta kidogo ilisaidia washiriki kupoteza kilo 4.2 zaidi ya wale walio kwenye lishe ya kudhibiti.
Faida ya ziada ni kwamba mlo wa mboga mboga kwa kawaida ina kiwango cha chini cha mafuta isiyohitajikahivyo basi hakuna haja ya kufanya ya kudhibiti kiwango cha kalori.
2. Afya ya moyo
Kufurahia mlo uliojaa vyakula ambavyo ni rafiki wa mboga mboga kama vile nafaka, kunde, matunda na mboga, kunahusishwa na hatari ndogo ya ugonjwa wa moyo ikiwa ni pamoja na kiharusi.
3. Inaweza kusaidia kusawazisha sukari mwilini
Kuzingatia lishe ya mboga mboga kunaweza kusaidia wale walio na shida ya sukari mwilini.
Watu wanaotumia lishe ya mboga mboga hujipunguzia hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari aina ya 2.
Kujumuisha nafaka katika lishe husaidia kuleta utulivu wa sukari ya damu kwa sababu nafaka husaidia kusaga chakula polepole, kama kizuizi cha mwili.
Kujumuisha nafaka katika lishe husaidia kuleta utulivu wa sukari ya damu kwa sababu nafaka husaidia kusaga chakula polepole, kama kizuizi cha mwili.
Ikiwa unataka kufikia faida za sukari ya damu kutokana na lishe ya mboga mboga, hakikisha unajumuisha nafaka nyingi kwenye milo yako.
4. Huweza kupunguza hatari ya baadhi ya saratani
Magonjwa ya saratani yanatarajiwa kuongezeka katika miongo michache ijayo.
Ongezeko hili likifikiriwa kwa sehemu fulani, linatokana na mambo na mtindo wa maisha ikiwa ni pamoja na unene, kutofanya mazoezi na lishe.
Kula vyakula vingi vinavyotokana na mimea ikiwa ni pamoja na kunde, matunda na mboga mboga na kupunguza ulaji wako wa nyama nyekundu au iliyosindikwa imeonekana kupunguza hatari ya saratani.
Utafiti unaochunguza athari za lishe inayotokana na mimea unaonekana kunyesha kuwa na matokeo bora zaidi kwa saratani zote za hatari hupatikana kutoka kwa lishe bora ya mboga mboga.
5. Inaweza kuwa na manufaa kwa afya ya utumbo
Mfumo wa utumbo inategemea jamii ya vijidudu (bakteria, chachu na virusi) ambavyo vinaishi kwenye njia ya utumbo.
Uelewa wetu wa jumuiya hii muhimu ya viumbe hai unaendelea na sasa tunajua kwamba unaathiri jinsi tunavyofikiri, kuhisi na jinsi tulivyo na afya njema.
Utafiti unapendekeza kwamba kwa kubadilisha vyakula tunavyokula, tunaweza haraka sana na kwa mafanikio kubadilisha mifumo yetu ya utumbo kuwa bora.