Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka: Arsenal waanza mazungumzo na Cunha
Arsenal waanza mazungumzo ya kumnunua Matheus Cunha, mustakabali wa Julen Lopetegui West Ham uko mashakani, huku Harry Maguire akiwaniwa na klabu kadhaa za Ligi ya Premia.
Arsenal wamefanya mazungumzo ya awali na mshambuliaji wa Wolves wa Brazil Matheus Cunha, 25. (Caught Offside), nje.
Beki wa Uholanzi Virgil van Dijk amepokea ofa ya mkataba kutoka kwa Liverpool lakini haiendani na matarajio ya mchezaji huyo wa miaka 33. (Athletic - usajili unahitajika)
Mustakabali wa Julen Lopetegui kama kocha mkuu wa West Ham uko kwenye mizani. (Sky Sports)
Edin Terzic, Roger Schmidt, Sergio Conceicao na Massimiliano Allegri ni miongoni mwa wakufunzi wanaowaniwa na West Ham. (Telegraph - usajili unahitajika)
West Ham pia inavutiwa na kocha wa zamani wa Brighton na Chelsea Graham Potter. (Times - usajili unahitajika)
Rodri ameiomba Manchester City kumnunua mchezaji mwenza wa kimataifa na winga wa Athletic Bilbao Nico Williams, 22. (Metro)
Beki wa Uingereza Harry Maguire, 31, anawaniwa klabu kadhaa za Ligi Kuu ya England huku mushtakabili wake katika klabu ya Manchester United ukiwa haujulikani. (Football Insider)
Kocha wa Paris St-Germain Luis Enrique hataki klabu hiyo ya Ufaransa kumleta mshambuliaji wa Sporting na Sweden Viktor Gyokeres, 26, ambaye amekuwa akihusishwa na Manchester City na Manchester United. (Foot Mercato)
Newcastle United inawafuatilia winga wa Bournemouth na Ghana Antoine Semenyo, 24, na mshambuliaji wa Brentford wa Cameroon Bryan Mbuemo, 25. (The i News - usajili unahitajika)
Arsenal na Liverpool wanamfuatilia winga wa LA Galaxy mwenye umri wa miaka 23 kutoka Brazil Gabriel Pec. (Caught Offside)
Hull City wanatazamia kumteua mkufunzi wa Reading Ruben Selles kama kocha wao mpya, huku Alex Neil na Slavisa Jokanovic wakiwa miongoni mwa wengine wanaowania nafasi hiyo. (Telegraph - usajili unahitajika)
Klabu za EPL zinamfuatilia mshambuliaji wa Celtic wa miaka 18 Daniel Cummings. (Mail- usajili unahitajika)
Crystal Palace wanatazamiwa kumsajili mshambuliaji wa Australia Rylan Brownlie mwenye umri wa miaka 17 kwa uhamisho wa bure. (Football Insider)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi