Sheria za vita ni zipi na zinatekelezwaje?

tt

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Mashirika ya Haki za Binaadamu ndio watetezi wakuu wa sheria ya vita

Vita vya Israel na Gaza sio vita vya kwanza duniani ambapo pande zote mbili zinashutumiana kwa kukiuka sheria ya vita. Kila mzozo mkubwa wa vita unapotokea, shutuma za kukiuka sheria za kimataifa zinazohusiana na vita huwa ni sehemu ya propaganda za pande zinazopigana.

Shutuma kama vile kuua raia, kuua watoto, kutumia silaha zinazokatazwa, au mauaji ya halaiki na uhalifu wa kivita ni kbaadhi ya shutuma za mara kwa mara zinazotolewa wakati wa vita.

Lakini je, ni kweli kuna sheria iliyoandikwa kuhusu vita ambayo kila mtu lazima afuate? Sheria hii ilitungwa wapi? Nani aliidhinisha? Maudhui yake ni nini? Na inatekelezwa vipi?

Sheria ya vita ni nini?

tt

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Katazo la kuuwa raia wasio na hatia lilikuwa jambo muhimu kwa wanaharakati wa haki za binaadamu mwanzoni mwa karene ya 20

Sheria ya vita ni sehemu ya sheria ya kimataifa. Hii ni mikataba ya kimataifa ambapo sheria zinazohusiana kupigana na kutumia silaha huamuliwa.

Hakuna mikataba ya kudumu ya sheria za vita. Mikataba hubadilika kulingana na muda na kuchukua sura tofauti kulingana na mageuzi ya jamii ya wanadamu.

Sheria ya vita si kama katiba ya baadhi ya nchi, ambayo imekusanywa utaratibu wa uhakika, wawazi na inaweza kuongezwa na kupunguzwa vifungu vyake.

Chochote kinachosemwa katika makubaliano mbalimbali ya sheria za kimataifa na ikiwa utekelezaji wake ni muhimu wakati wa vita, inachukuliwa kuwa sheria ya vita.

Sheria ya vita ilianzia wapi?

FDC

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Wanadamu wana historia ya kuamua sheria za mapigano. Lakini kabla ya enzi ya sasa, hakuna mamlaka ambayo iliweka sheria ambazo kila nchi ilipaswa kuzifuata.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kuanzia katikati ya karne ya 19, nchi za Ulaya zilifikia uamuzi kwamba wana nguvu hiyo kwa kuzingatia mikataba waliyotia saini kati yao kama "sheria za kimataifa"

Kuanzia katikati ya karne hii, nchi hizi zilifikia makubaliano juu ya sheria za baharini, ambayo ni msingi wa kwanza ya "sheria ya vita. Sheria hizi ziliongezeka hatua kwa hatua katika karne ya 20, na baadhi zinaendelea kutumika hadi leo.

Baada ya vita vyote viwili vya dunia, sheria hizi zikawa maarufu zaidi ili kupunguza kiwango cha maafa ya binadamu na mauaji ya watu wengi.

Maendeleo na mageuzi katika sheria ya vita yameendelea hadi leo, na kila wakati mkataba mpya wa kimataifa unapoidhinishwa kuhusu matumizi ya silaha mpya au zana za kisasa, maelezo yake yanaongezwa katika sheria ya vita.

Mashirika ya hisani kama vile Msalaba Mwekundu/Hilali Nyekundu ni wahimizaji wakuu wa kufutwa sheria hizi. Hujaribu kusaidia utekelezaji wa sheria hizi kwa kuchapisha taarifa sahihi na za kuaminika - sanjari na kuwakosoa wale wanaozikiuka.

Mafanikio na Ukosoaji

FD

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Baada ya vita vya pili vya dunia kuisha viongozi wa Nazi walishitakiwa kwa kuvunja sheria ya vita na sheria nyingine za kimataifa

Utekelezaji wa sheria ya vita una uhusiano wa moja kwa moja na kiasi cha habari kuhusu vita hivyo, pamoja na maoni ya umma juu ya vita hivyo.

Kando na hayo, wakosoaji wanasisitiza kuwa sheria ya vita inatekelezwa ndani ya mfumo wa "siasa zenye nguvu" na wavunjaji wa sheria hii wanaadhibiwa ikiwa maslahi ya nchi zenye nguvu, watawala wakuu, na miungano ya kimataifa yenye nguvu iko hatarini.

Bila kujali ukosoaji, mikataba mingi ambayo inaweza kuwa sehemu ya sheria ya vita imetoa suluhisho kwa kwa baadhi ya mambo. Mfano vikwazo na hata kuanzishwa mahakama ya kimataifa na kes kufunguliwa.

TYG

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Sehemu ya sheria hizi zinachochewa na hisia ya ubinadamu

Ipo Mahakama ya Kimataifa ya Haki ambayo inashughulikia malalamiko ya nchi dhidi ya nchi. Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu yenye mamlaka ya kushughulikia tuhuma za watu binafsi kama uhalifu wa kivita au mauaji ya kimbari.

Moja ya mfano wa Sheria ni matumizi ya silaha za uharibifu kama vile silaha za kemikali. Hata katika kesi kama vile vita ya Syria ambapo silaha za kemikali zilitumika. Wahusika wa kimataifa wote wanakubaliana kwamba aina hiyo ya silaha hazipaswi kutumika.

Suala hili linaonyesha wazi kwamba, mbali na ukosoaji, sehemu za sheria hizi zina uhalali wa kimataifa wa kimataifa na hakuna hata mmoja wa wahusika wa kimataifa anayehoji kanuni ya sheria ili kuzikiuka.

Mkataba wa Geneva ni nini?

FD

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Picha ya mji wa Bucha huko Ukraine baada ya mashambulizi ya Urusi

Katika mikataba ya kimataifa inayohusiana na sheria ya vita, kile kilichoidhinishwa huko Geneva mnamo 1948 kina umuhimu wa pekee.

Makubaliano haya yaliidhinishwa katika mikataba minne tofauti iliyofanyika Geneva mwaka wa 1948. Matendo ya nchi fulani wakati wa vita ndiyo yaliyozingatiwa kama msingi wa mkataba wenyewe. Mkusanyiko wa sheria hizi, ndio zinajuulikana kama Mkataba wa Geneva.

YTGH

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Mkutano wa 1948

Katika kusanyiko la kwanza, sheria zinazohusiana na jinsi ya kutibu waliojeruhiwa katika vita zilisainiwa. Katika mkataba wa pili, sheria zinazohusiana na majeruhi wa vita katika vita vya majini zilisahiniwa.

Katika mkataba wa tatu, suala la "wafungwa wa vita" lilichunguzwa na namna ya kukabiliana. Na katika Mkataba wa Nne, sehemu muhimu ya "Sheria ya Vita" zilisainiwa kuhusu hitaji la kuwalinda raia wakati wa vita.

Imetafsiriwa na Rashid Abdallah na kuhaririwa na Ambia Hirsi