Je, mtu aliyehukumiwa kunyongwa akiwa na umri wa miaka 12 alitokaje baada ya miaka 28 jela?

Miaka 25 iliyopita, mvulana alihukumiwa kifo kwa kuchukuliwa kuwa na miaka 18 katika kesi ya mauaji.
Kuthibitisha kwamba alikuwa mvulana mdogo wakati wa kesi hiyo ni jambo lililoshindikana na mahakama ya Juu ilibatilisha hukumu yake mwezi Machi.
Mwandishi wa BBC Saudhik Biswas alisafiri hadi kijiji cha Jalapsar katika jimbo la Rajasthan kukutana na mwanamume huyo, ambaye sasa ana umri wa miaka 41.
Imepita wiki kadhaa sasa tangu Niranram Chetanram Chaudhary aachiliwe baada ya kufutiliwa mbali kwa hukumu ya kifo dhidi yake katika gereza moja katika mji wa Nagpur, magharibi mwa India.
Ametumia miaka 28, miezi sita na siku 23 za maisha yake akisoma vitabu chini ya ulinzi mkali katika seli ya futi 12 kwa 10 na kujaribu kuthibitisha kwamba alihukumiwa kabla ya kutimiza miaka 18.
Jumla ya siku 10,431.
Niranaram alihukumiwa kifo kwa kuua watu saba, ikiwa ni pamoja na wanawake watano na watoto wawili, huko Pune mwaka 1994.
Pia alikamatwa pamoja na wanaume wawili kutoka kijiji chake huko Rajasthan.
Alihukumiwa kifo mnamo 1998, akidhani alikuwa na umri wa miaka 20.
Katika kesi hiyo, Mahakama ya Juu ya India mwezi Machi ilihitimisha kesi ya Niranaram ya miaka 30, ambayo ilihusisha mahakama tatu, kusikilizwa mara nyingi, ukataji wa rufaa, maombi ya rehema, vipimo vya kuthibitisha umri na utafutaji wa karatasi zake za tarehe ya kuzaliwa.
Majaji waliamua kuwa Niranaram alikuwa na umri wa miaka 12 na miezi 6 pekee wakati wa uhalifu huo na kwamba alikuwa mtoto mdogo.
Kulingana na sheria za India, adhabu ya kifo haiwezi kutolewa kwa vijana wadogo badala yake (Wanakabiliwa na kifungo cha juu zaidi cha miaka mitatu jela.)
Je, iliwezekanaje kutokea kwa ukiukwaji mkubwa kama huo wa haki hadi kumhukumu kijana kifo?

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Wakati Niranaram alikamatwa, kwa sababu ambazo haziko wazi kabisa, polisi walikuwa wameandika vibaya umri na jina lake.
Jina lake lilitajwa kimakosa kama Narayan katika barua iliyoandaliwa na polisi wakati wa kukamatwa kwake.
Hakuna anayejua wakati umri usio sahihi ulirekodiwa.
"Rekodi zinazohusiana na kukamatwa kwake ni za zamani sana. Nyaraka za awali za kesi hiyo hata hazijafika katika Mahakama ya Juu," alisema Shreya Rastogi, wa mpango wa haki ya jinai katika Chuo Kikuu cha Sheria cha Kitaifa cha Delhi.
Cha kushangaza katika kesi hiyo ni makosa katika tarehe yake ya kuzaliwa na ombi la mtoto huyo mdogo halikuzungumzia na mahakama, waendesha mashtaka na wakili wapinzani hadi 2018.
Niranaramn ni mmoja wa watu wengi kutoka vijijini India ambao hawajui tarehe yao ya kuzaliwa kwa uwazi na hivyo hawapati cheti cha kuzaliwa.
Rejesta ya zamani katika shule yake ya kijijini iliorodhesha tarehe yake ya kuzaliwa kuwa 1 Februari 1982. Hii hatimaye ilimuokoa.
"Mfumo mzima umefeli -- waendesha mashtaka, mawakili wapinzani, mahakama, wapelelezi... tumeshindwa kuthibitisha umri wake wakati wa tukio," Rastogi alisema.
Wiki iliyopita, tuliendesha gari kupitia eneo lenye joto na mchanga mwingi, miti iliyochakaa hadi kijiji chenye nyumba 600 na watu 3,000 huko Bikaner, Rajasthan.
Alizaliwa kwa baba mkulima, Niranaram amerudi kuishi na familia yake kubwa ya kaka 4, wake zao na watoto.
"Kwa nini hii ilinitokea?

Kijiji hicho kilionekana kuwa na mafanikio licha ya mashamba yaliyoenea kwenye milima.
"Kwa nini hii ilinitokea? Nilipoteza sehemu muhimu ya maisha yangu kwa sababu ya kosa rahisi, "Niranaram, mrefu na macho yaliyoingia ndani, alisema.
Anahoji nani atafidia haya yote. Serikali haikutoa fidia yoyote kwa kosa hilo.
Mnamo 1998, wakati Niranaram na washtakiwa wengine walihukumiwa kifungo cha maisha, mahakama ilisema kesi hiyo ilikuwa nadra.
Mnamo Agosti 26, 1994, watu saba wa familia moja walipatikana wamekufa katika jaribio la wizi katika nyumba moja huko Pune.
Kulingana na familia ya mwathiriwa, mmoja wa washtakiwa alikuwa akifanya kazi katika duka moja linalomilikiwa na familia iliyouawa.
Aliacha kufanya kazi wiki moja kabla ya mauaji.
(Mwanamume huyo baadaye aliachiliwa kwa sababu alisaidia katika uendeshaji wa mashtaka.)
Familia ya marehemu haikuwafahamu washtakiwa wengine wawili, akiwemo Niranaram.
"Kulikuwa na haja gani ya kuwaua wote ikiwa nia yao ilikuwa kupora?" Sanjay Rathi, mmoja wa familia ya mwathiriwa, aliambia vyombo vya habari vya Indian Express mnamo 2015.

Niranaram alisema kuwa alitorokanyumbani baada tu ya kumaliza darasa la tatu katika shule ya mtaani.
Alipoulizwa na BBC kwa nini alitoroka nyumbani, alisema, “Sikumbuki kabisa.
Sikumbuki hata nilikutana na nani. Nilitoroka nyumbani na kufika Pune.
Nilipata kazi katika duka la kushona nguo huko.
" Familia yake pia haikumbuki kwa nini Niranaram aliondoka nyumbani.
Alipoulizwa analipi la kusema kuhusu mauaji hayo, alisema, "Sikumbuki chochote kuhusu uhalifu huo.
"Sijua kwanini polisi walinichukua, nakumbuka walinipiga baada ya kukamatwa, nilipowauliza kwa nini wananipiga, walisema kuna kitu kimetokea Marathi, sikujua chochote wakati huo," alijibu.
Je, ulikiri kufanya makosa?

“Sikumbuki. Lakini polisi waliniambia nitie sahihi karatasi nyingi. Tulikuwa wadogo sana. Nilifikiri nilinaswa katika jambo lisilo la haki.”
Kwa hiyo nilipomuuliza kama anakanusha kutuhumiwa kufanya uhalifu, mimi sikatai wala kukubali uhalifu huo.
Ninaweza kusema zaidi katika suala hili ikiwa kumbukumbu zangu ni sahihi.
Lakini Niranaram akajibu kuwa sikumbuki chochote.
Wakati ikiachiliwa huru mwezi uliopita, Mahakama ya Juu ilikuwa na mashaka kama mvulana wa miaka 12 angeweza kufanya uhalifu huo wa kutisha.
"Wakati hii inatushtua, hatuwezi kutumia uvumi kama huo kuficha mchakato wetu wa hukumu. Hatuna ujuzi wa saikolojia ya watoto au uhalifu wa kutilia maanani jambo hili...,” majaji walisema.
"Sikumbuki chochote kuhusu gereza hilo isipokuwa wafungwa wenzake na maafisa waliomdhulumu," Niranaram alituambia huku akiketi sakafuni.
Ingawa alikaa kwa muda katika Jela ya Pune, bado anaweza kukumbuka siku zake kama mfungwa nambari 7322 katika Jela ya Nagpur.
'Sikuweza kufanya urafiki na wafungwa wenzangu kwa sababu niliogopa sana.
Nilipambana na upweke kwa kuzingatia masomo yangu,’’ anasema.
Ana shahada ya uzamili katika sosholojia na anajiandaa kusomea shahada ya sayansi ya siasa baada ya kuachiliwa kutoka gerezani.
Alitaka kutembelea India yote mara tu alipoachiliwa kutoka gerezani.
Kwa hili alichukua kozi ya miezi 6 inayohusiana na utalii. Pia alizingatia kusoma mawazo ya Gandhi na kusema, "Vitabu ni rafiki yako mkubwa unapokuwa jela."
Niranaram alisema kwamba mawasiliano yake pekee na ulimwengu wa nje ilikuwa kupitia magazeti kadhaa ya Kiingereza.
Aliyasoma kuanzia mwanzo hadi mwisho.
Baada ya kuona picha ya mwigizaji wa Hollywood Vin Diesel kwenye gazeti, naye pia akaamua kunyoa nywele zake.
Pia alisoma habari kuhusu vita vya Ukraine. "Hii inaonyesha kwamba dunia ya leo inakabiliwa na ukosefu wa uongozi unaokubalika na wote kujadili suluhu kati ya nchi hizo mbili," alikuwa amebainisha katika barua kwa Rastogi akiwa gerezani.

Usiku wa kabla ya mtoto wake kurudi nyumbani baada ya siku ndefu, mama yake Niranaram, ambaye alikuwa amevuka miaka 70, alikuwa akisherehekea.
Lakini Anni Devi alikuwa anatiririkwa na machozi alipomwona mwanawe usoni - hakufikiria kile wengine walikuwa wakisema
Baba yake Niranaram aliaga dunia mwaka wa 2019.)
"Tulitazamana. Mama yangu amebadilika sana, "Niranaram alisema.
Niranaram, ambaye aliachiliwa kutoka gerezani mwezi Machi, alianza kutambua "ni kiasi gani India imebadilika".
“Kuna aina mpya za magari barabarani. Watu wanavaa nguo za kifahari.
Barabara ziko katika hali nzuri sana.
Nchi hii imebadilika sana,” alisema huku akitabasamu.
"Wakati mwingine ninahisi kama mgeni katika nyumba yangu mwenyewe,'' anasema. Kuzungumza na watu hadharani kunanitisha. Nimezoea kuwa katika seli ndogo gerezani. Upweke huo mkubwa haukufanyi uwe na uhusiano wa kawaida na jamii. Inabidi niwe makini".
Niranaram alisema kwamba anapaswa kujifunza jinsi ya kuishi kama mtu huru.
"Sijui jinsi ya kutangamana na watu. Hasa wanawake, anasema, kabisa.
"Nafikiri mara mbili kabla ya kuzungumza na wengine," alisema.
Hata hivyo, alisema kwamba anataka kuanza maisha mapya.
Familia yake imempa Niranaram smart phone. Anajifunza jinsi ya kuitumia.
Watoto wa kaka zake wamemfungulia Niranaram akaunti za Facebook na WhatsApp.
Niranaram anasema anataka kusomea sheria na kujihusisha na huduma za kijamii, pia alisema kwamba anataka kuwasaidia wafungwa ambao wanapitia hali kama yake.












