Ukraine: Wanajeshi ambao hawataondoka mstari wa mbele hadi vita viishe

dfvc

Chanzo cha picha, Mark Urban/BBC

Maelezo ya picha, Jimmy anaongoza kikosi cha 24
    • Author, Mark Urban
    • Nafasi, BBC

Maisha kwenye mstari wa mbele wa vita vya Ukraine sio rahisi, BBC ilikwenda kushuhudia.

Akiwa amesimama katikati ya magofu ya majengo, Jimmy, afisa wa Ukraine - amefanya kazi kwa miaka mingi katika jeshi, alitafakari kuhusu maisha yake na kusema, "kwa ninavyoona mimi ni mwenye bahati."

Jimmy (jina la lakabu) anaongoza kikosi cha 24 kiitwacho Mechanized Brigade, kina historia ndefu, ni sehemu ya jeshi la kawaida la Ukraine, linalopigana na Warusi toka 2014. Tangu uvamizi wa Februari 2022, kikosi hicho kimeongezeka zaidi ya mara tatu kwa ukubwa.

Mwezi Agosti tulitumia wiki mbili, kwenye kituo cha zamani cha viwanda vya sigara upande wa mashariki tukiwa na kikosi cha 24, kinachopigana huko Donbas. Ni kikosi cha mstari wa mbele kati ya Bakhmut na Horlivka.

Kabla ya vita, Brigedi ya 24 ilikuwa na wanajeshi 2,000, wakigawika katika makundi matatu. Ingawa jeshi la Ukraine ni mara chache hujadili idadi ya wapiganaji, kikosi hicho kwa sasa kimeogezeka na kuwa na zaidi ya wanajeshi 7,000, wakigawika katika makundi kadhaa - vikosi vitano vya askari wa miguu, vinne vya mizinga na kikosi cha vifaru.

Maisha ya Yuri

cxc

Chanzo cha picha, Mark Urban/BBC

Maelezo ya picha, Yurii na ndroni zake

Wakati vita vinaanza, askari wa zamani wa kawaida waliungwa mkono na maelfu ya watu wa kujitolea. Yurii, mfanyabiashara kutoka Kyiv ni mmoja ya raia waliojitolea kubeba silaha kupigana na Urusi.

Hapo awali alipewa bunduki na kuwa katika kikosi cha ardhini. Miezi michache baadaye, Yurii alihamishwa na kupelekwa katika kitengo cha droni cha kikosi hicho cha 24.

Akiwa ameketi kwenye meza katika uwanja wa michezo wa watoto karibu na mstari wa mbele, alituonyesha ndege mpya zisizo na rubani, na vifurushi vya vilipuzi, vikimruhusu yeye na wengine kuzirusha katika magari, majengo, au vizimba ambako Warusi wanajificha.

Yurii alielezea jinsi mama yake alivyokuwa na shaka juu ya kujiunga na jeshi, lakini mara tu alipoanza kuongoza ndege zisizo na rubani na kushambulia jeshi la Urusi, alibadilisha mawazo yake, na sasa anamuunga mkono.

Kwa masharti ya mkataba wao wa kujitolea – sawa na askari wa kawaida - hawawezi kuondoka mstari wa mbele na wanalazimika kuhudumu hadi vita viishe. Lakini wana haki ya likizo ya siku 10 tu kila mwaka.

Yurii anapata dola za kimarekani 3,195 tu kila mwezi. Malipo madogo kulinganisha na alichokuwa anakipata katika maisha yake ya uraiani – alipokuwa mfanyabiashara.

Yurii mwenye ndevu, aliniambia jinsi kikosi chao kinavyopaswa kuwa na ujuzi zaidi kuliko Warusi kwa sababu adui ana ndege zisizo na rubani nyingi zaidi. Mmoja wa maofisa alifichua kuwa Yurii anaendesha kitengo hiki.

Babu Hryb

zdzx

Chanzo cha picha, Mark Urban/BBC

Maelezo ya picha, Sajenti Hryb
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Pia tulikutana na sajenti Hryb (sio jina rasmi) - amepewa jukumu la kusimamia mizinga. Ana umri wa miaka 52. Amefanya kazi katika jeshi zaidi ya miaka 30 iliyopita. Anajua nini kuhusu vita vya kisasa?

Mizinga wanayotumia imetengenezwa miaka 40 iliyopita. Ni nani bora kujua namna ya kuitumia kuliko Babu Hryb? Uamuzi wake wa kujitolea haukuwa rahisi kwa familia yake. "Walilia kimya kimya," Hryb alielezea. "Walisema watanisubiri, na wananipenda."

Nyuma ya tamko hili la "kwa kadiri vita vitakavyo dumu." Mamia kwa maelfu ya familia za Ukraine zinahangaika, zikiwa na matumaini sanjari na hofu wakati vita vinapofikisha miezi 18 na havionekani kukoma hivi punde.

Katika kituo cha matibabu huko Lviv cha askari walio na majeraha makubwa. Nilipata simulizi za akasri walio pona na kuwaambia wake zao wanataka kurudi tena mstari wa mbele wa vita.

Kati ya wanaume ambao tuliwarekodi wakifunzwa huko Yavoriv na maeneo mengine yaliyokaribu na mstari wa mbele - wengi wako katika miaka yao ya 40, na wachache kabisa katika miaka yao ya 50. Maafisa walituambia kuhusu changamoto kubwa ya kuwaajiri vijana katika brigedi mbalimbali.

Maafisa kadhaa waliokuwa wakisimamia vituo vya kuandikisha wapiganaji wapya walitimuliwa mwezi Agosti. Maelfu ya wanaume walikuwa wakihonga ili wasiandikishwe au wasafirishwe nje ya nchi ili kukwepa kuingia jeshini.

Miongoni mwa wale wanaojitolea kwa hiari - wengi ambao wamepoteza kazi zao katika mgogoro wa kiuchumi unaoambatana na vita na kuvutiwa na malipo yanayotokana na kuwa mstari wa mbele.

"Unapaswa kusubiri"

dszxc

Chanzo cha picha, Mark Urban/BBC

Maelezo ya picha, Natalia alijaribu kumzuia ndugu yake asiende vitani bila mafanikio a

Kuhusu majaribio ya kuvunja ngome za Urusi msimu huu wa joto, ili kukomboa ardhi iliyokaliwa. "Mafanikio ya haraka hayawezekani," Jimmy alituambia. "Tunajitayarisha kwa vita vya muda mrefu."

Afisa mwingine - mwongoza kikosi, alilinganisha mzozo huo na vita vya Vietnam, akimaanisha kuwa unaweza kudumu miaka mingi.

Kadiri mapigano yanavyoendelea, ndivyo hasara inavyoongezeka. Majeruhi ni suala la nyeti sana nchini Ukraine. Ni kinyume cha sheria kuchapisha takwimu. Lakini Pentagon ilikadiria Waukraine 70,000 wameuawa katika vita hivyo, wengi wao wanajeshi.

Kulingana na uchunguzi wetu kupitia mitandao ya kijamii na ripoti za vyombo ya habari, makadirio yetu yanayonyesha Brigedi ya 24 imepoteza wapiganaji takribani 400. 120 kati yao walikufa wakati wa mapigano kati ya 2014 na mwanzoni mwa 2022, waliobaki ni tangu uvamizi wa Urusi.

Pia mada nyingine nyeti ni kujua idadi ya wafungwa wa vita waliokamatwa na Urusi, kwani ubadilishaji wa wafungwa umekuwa wa kiwango kidogo sana.

Mke wa mfungwa mmoja wa vita alituambia ni wanaume 22 tu kutoka Brigedi ya 24 wamerudi hadi sasa na idara zote za serikali alizoziandikia zilimpa mrejesho sawa: "Unapaswa kusubiri."

Nje kidogo ya jiji la Lviv, tulimfuata Natalia Nezhura katika makaburi alipokuwa akiweka maua mapya kwenye kaburi la ndugu yake Andrii. "Nilijaribu kila kitu kumzuia kwenda mstari wa mbele," alielezea.

Alificha karatasi za wito wa Andrii, hilo liliposhindwa alimtafutia kazi ya kutoa mafunzo ya silaha katika kituo cha mafunzo cha Yavoriv, "lakini mwishowe wavulana wengi katika kituo hicho walipelekwa mstari wa mbele".

Andrii aliuawa mapema mwaka huu, wakati Brigedi ya 24 ilipokuwa ikipambana Bakhmut. Mazungumzo yetu yalifanyika katikati ya bendera zinazopepea za wanajeshi waliouwawa. Tulihesabu makaburi zaidi ya 2,000.

Nilipomuuliza jinsi vita hivyo vitaishaje, Natalia alijibu: “Nataka tu Warusi wote wafe, ninawachukia kwa moyo na roho yangu yote,” akaongeza, “unawezaje kuzungumzia amani wakati waliwaua watu wetu wengi?"