Usaliti ndani ya ndoa: Simulizi kuhusu mwili uliokutwa kwenye jeneza

Chanzo cha picha, getty images
Onyo: Baadhi ya maelezo katika hadithi hii yanaweza kuwa ya kusumbua.
Ilikuwa miaka ya 1950. Treni iitwayo 'Indu Ceylon Express' ilikuwa imeondoka kutoka jimbo la India la Tamil Nadu. Ilikuwa Ikisafiri kutoka kituo cha Chennai Egmore hadi Dhanskudi na kutoka hapo kuelekea Thalaimanar nchini Sri Lanka.
Siku hizo, safari ya kutoka kituo cha Egmore cha Chennai hadi Dhanushkodi ilichukua saa 19. Baada ya kufika Dhanushkodi, watalii walikuwa wakishuka kwenye gari-moshi na kutoka hapo walipanda mashua hadi Thalaimanar nchini Sri Lanka.
Safari ilikuwa ya saa tatu na nusu na boti iliitwa 'Mail Express'.
Takribani miaka 70 iliyopita, mwili uliokatwa kichwa ulipatikana katika treni hii ambayo ilishtua kila mtu. Mauaji haya yametokeaje na ni sababu gani ya mauaji haya, mwili wa nani uliokatwa kichwa, haya ndiyo maswali yaliyoendelea kuipamba habari hiyo kwa siku nyingi.
Siri ya mwili uliokatwa kichwa kwenye jeneza

Chanzo cha picha, Getty images
Agosti 29, 1952 ndiyo siku ambayo treni ya haraka iliyoondoka Chennai saa 8 ilifika Manamadurai saa 10 alfajiri.
Abiria walilalamika kwamba moja ya makochi ya treni ilikuwa ikinuka. Baada ya hapo polisi wa reli walijulishwa kuhusu hilo.
Polisi walipoingia ndani ya bogi husika, walikuta sanduku likiwa limelala, ambalo lilikuwa likitoa uvundo. Polisi walipofungua sanduku hilo, walikuta mwili wa binadamu ukiwa umekatwa kichwa.
Mwili huo ulikuwa na soksi za kijani kibichi miguuni, lakini kwa kuwa mwili huo haukuweza kutambuliwa, ulipelekwa katika hospitali ya serikali ya mtaa ambako uchunguzi wa maiti ulifanyika.
Katika uchunguzi wa maiti, madaktari walihitimisha kuwa mwili huo ulikuwa wa mwanaume mwenye umri wa miaka 25.
Polisi walisema kwamba mwanaume huyo alitahiriwa, kuashiria kwamba alikuwa Muislamu, lakini hitimisho zote mbili zilithibitishwa kuwa si sahihi wakati kesi ya mauaji ilipotatuliwa.
Kichwa chake kilikutwa kwenye begi ufukweni
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Wakati polisi wa Manamadurai walikuwa wakijaribu kutambua mwili uliokatwa kichwa uliopatikana kwenye jeneza, mwanamke mmoja alikuwa akimtafuta mumewe na kubisha hodi kwenye mlango wa nyumba ya Devaki, mtu anayemfahamu. Badala ya Devaki, mumewe Prabhakar Maan alifungua mlango.
Mwanamke huyo alimwambia Prabhakar Maan, 'Mume wangu hajarudi nyumbani tangu jana. Watu walimwona akiwa na Devaki. Ndiyo maana nimekuja hapa.'
Prabhakar Maan alimwambia bibi huyo kwamba hakuna mtu kama huyo nyumbani kwake wala hajaja hapa.
Mume wa mwanamke aliyepotea alikuwa mfanyabiashara. Jina lake lilikuwa Alwinder na alikuwa hajarudi nyumbani tangu jana yake usiku. Kwa hiyo mke wake alikuwa akimtafuta kuanzia asubuhi. Bila kupata habari za mumewe, mwanamke huyo, pamoja na rafiki wa karibu wa Alwinder, walikwenda kituo cha polisi na kutoa ripoti ya kupotea.
Kwa mujibu wa mwanamke huyo, polisi waliamua kuanza uchunguzi kutoka kwenye nyumba ya Devki, lakini polisi walipofika nyumbani kwa Devki, nyumba yake ilikuwa imefungwa. Katika uchunguzi kutoka kwa majirani, ilifahamika kwamba Devaki na Prabhakar Maan walikuwa wamekwenda Mumbai.

Chanzo cha picha, getty images
Jirani aliwaambia polisi kwamba Prabhakar Mann alionekana akielekea ufukweni akiwa na begi siku iliyotangulia. Polisi kisha walitafuta ufuo wa Raipuram kwa siku chache.
Siku ya tatu baada ya Alwinder kutoweka, wakazi wa eneo hilo walilalamika kwa polisi kuhusu harufu mbaya kutoka kwenye begi lililokuwa kwenye ufuo wa Raipuram.
Polisi walipata kichwa kikiwa kimefungwa kwenye shati la kahawia kutoka kwenye begi wakati wakichunguza eneo hilo. Hali ya kichwa kilichokutwa kwenye begi kilikuwa kimeoza. Habari zilipotoka kwenye magazeti siku iliyofuata, kulikuwa na ghasia huko Chennai.
Kichwa kilichokatwa kilipelekwa katika Chuo cha Matibabu cha Madras kwa uchunguzi. Wakati huo huo, mwili uliokatwa kichwa pia ulitumwa kutoka Manamadurai hadi Chennai. Kesi hizi zote mbili zilichunguzwa na profesa mashuhuri wa mahakama CP Gopalakrishan.
Baada ya uchunguzi wa kitaalamu, walisema umri wa maiti unaweza kuwa miaka 42 hadi 45.
Kichwa kilichokutwa Chennai kilikuwa na matundu mawili sikioni, kilipooneshwa mke wa Sir Alwinderji, mara moja alisema kuwa kichwa hiki ni cha mumewe baada ya kuona tundu la sikio na muundo wa meno.

Chanzo cha picha, THE MADRAS POLICE JOURNAL, 1955
Alwinder alikuwa nani?
Alwinder pengine alikuwa na umri wa miaka 42 alipouawa mwaka wa 1952. Alifanya kazi kama afisa wa kitengo kidogo katika ofisi ya jeshi lakini alistaafu jeshi baada ya Vita vya Pili vya Dunia.
Baada ya kustaafu, alianzisha biashara yake ndogo katika jiji la Chennai. Mwanzoni, alianza kuuza vitu vya plastiki pamoja na rafiki yake Kunam Chetty. Rafiki yake alikuwa akiuza kalamu huko Chennai. Alwinder alianzisha duka lake dogo katika kipindi hiki.
Kando na hayo, pia walikuwa wakiuza sare kwa wateja kwa awamu. Wakati huo wazo la kutoa sari au vitu kwa awamu lilikuwa jipya hivyo walipata faida nzuri katika biashara.
Ingawa Alwinder alikuwa na watoto wawili, uchunguzi wa polisi ulibaini kuwa walikuwa na uhusiano wa kimapenzi na walikuwa kwenye uhusiano wa nje ya ndoa. Kando na hayo, Alwinder alikuwa akitumia dawa za kulevya.
Usiku mmoja wakati Alwinder hakurudi nyumbani, mke wake alikwenda dukani na kuulizia kuhusu mume wake. Ambapo aliambiwa kwamba alikuwa amekwenda kukutana na Devaki.
Devaki na Prabhakar walipanga mauaji
Devaki alikuwa asili ya Kerala na baada ya kumaliza elimu yake ya chuo kikuu, alianza kufanya kazi katika taasisi ya ukuzaji lugha huko Chennai.
Devki na Alvinder walikutana katika duka la vifaa vya kuandikia. Utangulizi mnamo Agosti 1951 uligeuka kuwa upendo. Wakati huo Devaki hakuwa ameolewa lakini Alvindar alikuwa ameoa.
Alvinder alikuwa na uhusiano wa kimapenzi nje ya ndoa na Devaki. Hii iliendelea kwa siku chache na mnamo 1952, Devaki aliolewa na Prabhakaran Mann. Prabhakar Mann hapo awali alikuwa akifanya kazi katika kampuni ya bima ya binafsi. Baadaye akawa mhariri wa jarida liitwalo 'Sava Tantra'.
Wakati Prabhakarman alipokuwa akifanya kazi kwa bidii ili kukuza jarida lake, Devaki alimpeleka kwenye duka la Alvinder. Devaki anamwambia Prabhakar kwamba Alvinder anaweza kuleta tangazo la jarida hilo.
Kulingana na afisa wa polisi M Sangaravelo, aliyechunguza kesi hiyo, Alvinder alikuwa akimsumbua Devaki hata baada ya kufunga ndoa. Kwa hivyo Devaki aliamua 'kumuondoa Alvinder'.

Chanzo cha picha, getty images
Afisa aliandika makala ya kina kuhusu hili katika Jarida la Polisi la Madras mwaka wa 1955.
Aliandika kwamba Alvinder aliwahi kukutana na Prabhakar na kumwambia kwamba 'atakutana na afisa wa kampuni kubwa. Ikiwa Devaki pia atakuja nami, tunaweza kuomba tangazo kubwa la gazeti. Devaki kisha akahamia kwa Alwinder lakini nia ya Alwinder haikuwa nzuri.'
Wanampeleka Devaki hotelini kwa kisingizio cha kumtambulisha kwa mteja.
Baada ya kusikia kila kitu, Prabhakar anamuuliza Devaki 'Je, umewahi kuwa na uhusiano wa mapenzi na Alvinder?'
Devaki alijibu ndio, akisema kwamba wakati mwingine uhusiano huundwa chini ya shinikizo.
Kisha Prabhakaran alimhakikishia Devaki kulipiza kisasi na akapanga njama na Devaki kumuua Alvinder.
Alwinder aliitwa nyumbani na kuuawa

Chanzo cha picha, getty images
Tarehe 28 Agosti 1952, Devaki alikwenda kwenye duka la Alwinder na kumwomba arudi nyumbani. Kabla ya Alvinder kufika, Devaki anamtuma mtumishi wake mbali na nyumbani akiwa na pesa na kumuagiza arudi jioni.
Alwinder alipofika nyumbani kwa Devaki, wakati huo mumewe Prabhakar pia alikuwepo ndani ya nyumba hiyo lakini Alwinder hakujua kuhusu hilo. Prabhakar, pamoja na Devaki, muwalimuua Alvinder na kutenganisha kichwa chake na mwili.
Kisha mwili uliwekwa kwenye jeneza huku kichwa kikifungwa kwenye begi na kutupwa baharini huko Raipuram, lakini upesi mfuko huo ukasukumwa ufukweni na mawimbi.
Prabhakar alijaza mchanga kwenye begi na kuelea tena ndani ya maji, lakini wakati huo watu wengine walikuwa wamefika hapo na Prabhakar aliwaona na kukimbia.
Baada ya kurudi nyumbani, Devaki na Prabhakar wanaamua kuchukua mwili wa Alvinder hadi Kituo Kikuu cha Reli cha Chennai ili kuutupa. Walipofika pale wakiwa nahofu ya kuwepo kwa polisi, wakalichukua sanduku lenye mwili huo hadi kituo cha reli cha Egmore ambako waliliweka ndani ya treni.
Siku iliyofuata mke wa Alvinder anafika nyumbani kwa Devaki akiwatafuta, lakini kwa kuogopa kukamatwa na polisi, Devaki na Prabhakar mara moja walikimbilia Mumbai.
Haikuchukua muda mrefu kwa polisi kufichua mauaji ya Alvinder na mpango wa Devaki na Prabhakar. Sababu ilikuwa kwamba watu wengi walikuwa wamemwona Alvinder akiingia nyumbani kwa Prabhakar lakini hakuna mtu aliyemwona akirud.
Polisi wa Madras walikwenda Mumbai na kuwakamata Devaki na Prabhakar.
Wenzi hao walioshtakiwa walikuwa wakiishi na jamaa mmoja huko Mumbai. Alirudishwa Chennai kutoka Mumbai na kuhojiwa. Awali alikanusha shtaka la mauaji lakini kulikuwa na ushahidi mzito dhidi yake.
Dereva wa riksho aliyepeleka jeneza la Alwinder hadi kituo cha gari moshi na bawabu aliyeliweka kwenye treni walimtambua Prabhakar. Mfanyakazi wa Devaki Narayan pia alisema mambo mengi.
Uchunguzi wa kimahakama ulithibitisha kwamba yalikuwa mauaji ya kukusudia, lakini mtazamo wa hakimu kwa Alwinder ulikuwa mbaya sana.
Hivyo hakimu aliamua kutoa adhabu ndogo kwa wauaji Devaki na Prabhakar.
Mahakama ilimhukumu Prabhakar miaka saba na Devaki miaka miwili. Prabhakar na Devaki waliachiliwa baada ya kumaliza vifungo vyao katika miaka ya hamsini. Kisha akahamia Kerala alikozaliwa ambako alianzisha duka jipya.
Kesi hii ya mauaji inachukuliwa kuwa moja ya zilizo muhimu zaidi katika historia ya uchunguzi wa Polisi wa Tamil Nadu kwani sayansi ya uchunguzi ilichukua jukumu ambalo halijawahi kushuhudiwa katika kuthibitisha mauaji hayo.
Vitabu kadhaa viliandikwa baadaye kuhusu mauaji huko Tamil Nadu na mfululizo wa vipindi vya televisheni vilifanywa kwa mujibu wa kesi ya mwaka 1995.












