Ilani ya Faragha ya Chaneli ya WhatsApp ya BBC Swahili

Muda wa kusoma: Dakika 2

Imani yako ni muhimu sana kwetu. Hii inamaanisha kuwa BBC imejitolea kulinda faragha na usalama wa data yako ya kibinafsi. Ni muhimu kwamba usome ilani hii ili ufahamu jinsi na kwa nini tunatumia data kama hiyo ya kibinafsi. Notisi hii ya faragha inaeleza jinsi tunavyokusanya na kutumia data ya kibinafsi kukuhusu wakati na baada ya uhusiano wako nasi, kwa mujibu wa sheria ya ulinzi wa data.

BBC itakusanya data gani ya kibinafsi na jinsi tunavyoitumia

BBC itakusanya na kuchakata maelezo ya kibinafsi ambayo umechagua kutoa ili kutumia kama sehemu ya kujiunga na kufuata idhaa na jamii zetu. Taarifa hii inaweza kujumuisha baadhi au data zote zifuatazo zilizoorodheshwa hapa chini.

Data ya kibinafsi

Data ya kibinafsi ambayo inaweza kukusanywa itakuwa:

  • Akaunti/jina katika wasifu wako wa WhatsApp
  • Nambari yako ya mawasiliano, kama vile nambari ya simu
  • Picha inayoonyeshwa

Kutegemea hali ya picha yako inayoonyeshwa na mipangilio yako ya faragha, inawezekana kwamba BBC pia itakusanya na kuchakata taarifa nyeti, zinazojulikana pia kama data ya aina maalum ambayo utachagua kufichua. Hii inaweza kujumuisha kwa mfano:

  • Rangi au kabila lako
  • Taarifa za afya yako
  • Imani yako ya kidini au kifalsafa
  • Mwelekeo wako kuhusiana na masuala ya mapenzi
  • Maoni ya kisiasa

Kuweka mipangilio ya picha ya onyesho la WhatsApp iwe ya faragha

Tafadhali kumbuka ikiwa utaruhusu kila mtu kuona picha yako inayoonyeshwa kwenye akaunti yako ya WhatsApp, BBC inaweza kuona habari hii pia. Unahimizwa kubadilisha mipangilio yako ya faragha kuwa ‘anwani pekee’ ili kupunguza maelezo ya kibinafsi unayoshiriki kupitia WhatsApp nasi.

Mdhibiti wa Data ni nani?

BBC ni mdhibiti huru wa data na taarifa zozote za kibinafsi tulizopewa na wewe ambazo zimehifadhiwa kwenye vifaa na mifumo ya BBC.

WhatsApp ni "mdhibiti data" anayejitegemea wa data yoyote unayotuma kupitia programu. Tafadhali fahamu kuwa pia uko chini ya Sera ya Faragha ya WhatsApp na Sheria na Masharti. WhatsApp inaweza kushiriki data yako ndani ya Kampuni za Meta.

Kila mdhibiti anaamua ni kiwango kipi kuchakata maelezo yako ya kibinafsi yale yanatumiwa, na njia ambazo yanachakatwa. Kwa kuepusha shaka, taarifa zako za kibinafsi zitakusanywa na kuchakatwa na BBC kwa madhumuni yaliyoainishwa katika notisi hii ya faragha, ambayo inajiunga na kufuata Idhaa ya BBC ya WhatsApp. Kila mdhibiti ana wajibu wa kutii, na kuonyesha utiifu wa sheria ya ulinzi wa data.

Msingi ya kisheria au halali ya kuchakata data yako ya kibinafsi

Tunategemea idhini /rukhsa ya kutumia data ya kibinafsi kukuhusu. Hii ni kwa sababu umeamua kikamilifu kujijumuisha katika matangazo yetu ya Vituo vya WhatsApp. Iwapo ungependa kuacha kupokea matangazo haya unaweza kuondoa idhini yako wakati wowote kwa kujiondoa kwenye kituo.

Kushiriki maelezo yako

BBC haitashiriki data yako ya kibinafsi na washirika wengine bila idhini yako.

Kuhifadhi taarifa zako

BBC itachakata data yako ya kibinafsi kwa kipindi ambacho ni muhimu kutimiza madhumuni yaliyoainishwa katika notisi hii ya faragha.

Haki zako na habari zaidi

Una haki chini ya sheria ya kulinda data ya Uingereza. Unaweza kuomba nakala ya data ambayo BBC huhifadhi kukuhusu, ambayo inajumuisha data ya Akaunti yako ya BBC na data iliyofafanuliwa hapo juu mradi tu tunashikilia data hizi.

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia barua pepe yetu dataprotection.officer@bbc.co.uk. Ikiwa una maswali au ungependa kupata maelezo zaidi kuhusu haki zako, tafadhali tembelea Sera ya Faragha na Vidakuzi ya BBC katika http://www.bbc.co.uk/privacy.

Ikiwa una wasiwasi kuhusu jinsi BBC imeshughulikia taarifa zako za kibinafsi, unaweza kueleza wasiwasi wako kwa mamlaka ya usimamizi nchini Uingereza, Ofisi ya Kamishna wa Habari (ICO) https://ico.org.uk/.

Kusasisha notisi hii ya faragha

Tutarekebisha notisi ya faragha ikiwa kuna mabadiliko makubwa ya jinsi tunavyotumia data yako ya kibinafsi.