Ni kipi kinachowavuta Wahindi wengi kuhamia Australia?

Chanzo cha picha, MEDIALAB
Rohit Singh anazungumza kwa lafudhi ambayo ni tofauti kabisa na ya mama yake.
Yeye ni mhamiaji wa Kihindi wa kizazi cha pili anayeishi Mornington Peninsula, eneo la pwani ambalo ni takriban saa moja kwa safari ya kutumia gari kutoka Melbourne.
Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, amekuwa akiwasaidia wazazi wake kuendesha Avani, kiwanda cha divai walichoanzisha baada ya kuhamia Australia katika miaka ya 1990.
Bw Singh anasema kuwa katika muongo mmoja uliopita, jumuiya ya Asia Kusini huko Melbourne imeongezeka, kwa hivyo Avani ameanza kuandaa hafla za kuoanisha divai ambazo huangazia vyakula vya Kihindi - meen pollichathu (samaki waliookwa kutoka kusini mwa India) hutolewa kwa Pinot Gris; dal makhani (sahani ya dengu nyeusi iliyopikwa polepole na laini) na Pinot Noir.
Wapishi na wahudumu wa mikahawa ya majaribio haya ni miongoni mwa Wahindi zaidi ya 710,000 wanaoishi Australia, mojawapo ya "mataifa makubwa zaidi ya wahamiaji". Idadi yao imekuwa ikiongezeka kwa kasi katika miaka michache iliyopita - kulingana na sensa ya mwisho ya nchi hiyo, Wahindi sasa ni kundi la pili kwa ukubwa wa wahamiaji nchini Australia, wakiwa wamewapita Wachina na wa pili kwa Waingereza. Wimbi jipya la wahamiaji wa India kwa kiasi kikubwa limesukumwa na sekta ya teknolojia, kwani nchi ina mahitaji makubwa ya wafanyikazi wenye ujuzi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Aarti Betigeri, mwandishi wa habari ambaye kwa sasa anahariri historia kuhusu uzoefu wa Wahindi wanaokua Australia, anasema kwamba wazazi wake walipohamia huko katika miaka ya 1960, Wahindi hawakuwa sehemu kubwa ya umma. "Ilikuwa nadra kupata Mhindi mwingine mitaani," anasema.
Leo, mambo ni tofauti. "Wako katika kazi katika sekta zote, wanaendesha biashara zao na hata wanaingia kwenye siasa," anasema.
Serikali ya New South Wales iliyochaguliwa hivi majuzi ina wanasiasa wanne wenye asili ya India, akiwemo Daniel Mookhey, ambaye mwezi Machi alikua mwanasiasa wa kwanza mwenye asili ya India kuwa mweka hazina wa jimbo la Australia. Bado kuna safari ndefu, ingawa - Wahindi-Waaustralia, pamoja na wengine wenye nasaba isiyo ya Wazungu, bado hawajawakilishwa katika siasa, haswa katika ngazi ya shirikisho.
Mwezi Machi, Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese ziara yake ya kwanza nchini India tangu aingie madarakani, na wakuu hao walizungumzia ulinzi na usalama, uhusiano wa kiuchumi, na biashara baina ya nchi hizo.
"Mikutano ya mara kwa mara imeongeza uhusiano wa nchi mbili ambao haukuonekana siku za awali," Pradeep S Mehta, ambaye anafanya katika CUTS International, kikundi cha kimataifa cha utafiti wa sera za umma na utetezi.
Waangalizi wa mambo wanasema kuwa ushirikiano huu unaonekana kuwa wa manufaa kwa mataifa yote mawili, ambao pia ni sehemu ya kikundi cha nchi nne cha Quad wanaolenga kukabiliana na ushawishi wa China katika eneo la Indo-Pacific.

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Wakati uhusiano kati ya India na Australia ulianza mamilioni ya miaka - bara kuu liitwalo Gondwana liliwahi kuunganisha mataifa hayo mawili ya siku hizi - historia ya Wahindi kuhamia nchini humo inaangaliwa zaidi. Wahamiaji wa awali walifika Australia katika miaka ya 1800 kama vibarua au watumishi wa raia wa Uingereza waliokuwa wakihama kutoka India.
Katika miaka ya 1900, idadi kubwa ya Wahindi walianza kuhama na idadi yao iliongezeka sana baada ya sera ya White Australia - sheria ya kibaguzi ambayo ilizuia uhamiaji wa wasio wazungu - ilitupiliwa mbali mnamo 1973.
"Hata wakati huo, Australia ilisalia kuchagua aina ya wahamiaji iliowakaribisha; ni wahamiaji wenye ujuzi tu, kama vile wafanyakazi wa teknolojia, madaktari, wauguzi na wasomi waliokaribishwa, na hilo pia kwa kiwango kidogo sana," anasema Jayant Bapat, mtafiti ambaye ameshiriki. -aliandika kitabu juu ya diaspora ya Wahindi huko Australia.
Mbadiliko halisi yalikuja mwaka wa 2006, wakati serikali inayoongozwa na John Howard ilipofungua milango ya Australia kwa wanafunzi wa Kihindi na kuanzisha hatua za sera ambazo zilifanya iwe rahisi kwao kupata makazi ya kudumu.
"Wanafunzi wa India bado wanaunda sehemu kubwa sana ya wahamiaji wa muda. Baada ya kupata digrii zao, wengi wao wanaruhusiwa kuishi Australia," Bw Bapat asema.

Chanzo cha picha, Getty Images
Lakini kulikuwa na mvutano pia. Mwishoni mwa miaka ya 2000, idadi ya mashambulizi ya vurugu dhidi ya wanafunzi wa Kihindi huko Sydney na Melbourne yaligonga vichwa vya habari duniani kote.
Idadi ya wahamiaji wa India waliingia barabarani wakipinga, India ilijibu vikali na serikali ya Australia ikachukua hatua kushughulikia hali hiyo. Matukio ya upotovu ya vurugu bado yanaripotiwa mara kwa mara.
Wafunga mkono wanasema kuwa wahamiaji kutoka nchi za Asia na Kusini mwa Asia huleta tamaduni nyingi zinazohitajika kwa jamii ya Australia na wamesaidia uchumi kukua. Lakini baadhi ya wanasiasa wa upinzani wamekosoa sera za uhamiaji za Australia, wakisema kuwa wahamiaji wenye mishahara ya chini huchukua kazi na kuchangia uhaba.

Chanzo cha picha, MEDIALAB
Baadhi ya jamii ya Wahindi wanasema kwamba wanajaribu kuifanya Australia kuwa jumuishi zaidi kwa kuwaelimisha watu kuhusu utamaduni na urithi wao.
Divya Saxena, 24, ambaye amekulia Sydney, anataka kufanya dansi za asili za Kihindi kama Kathak na Bharatnatyam zienezwe zaidi nchini Australia.
Anasema kuwa Sydney Ina jumuiya inayostawi ya wabunifu wa Australia wenye asili ya kihindi kama yeye ambao wanajitahidi "kuvunja imani potofu" karibu na jumuiya ya Asia Kusini na kusaidiana biashara.
Bi Saxena hivi majuzi aliandaa utaratibu wa densi wa Rowi Singh, mshawishi wa urembo kutoka Australia mwenye asilia ya Kihindi ambaye hubuni mwonekano mzuri uliochochewa na urithi wake wa Asia Kusini
"Kizazi cha wazazi wetu kilianza hapa; lengo lao lilikuwa kushikilia kazi thabiti ili waweze kuwapa watoto wao maisha bora. Kwa hivyo waliweka vichwa vyao pamoja na kujaribu kuchanganyika. Lakini watu wa kizazi changu hawakubali kubeba mzigo kama huo," Bi Saxena anasema.
"Tuko huru kufuata matamanio yetu, na wengi wetu tunajaribu kuifanya Australia kuwa mahali bora zaidi kwa vizazi vijavyo."












