Je, uchumi wa Israel umeathiriwa vipi na vita?

wesdx

Chanzo cha picha, Getty Images

    • Author, Jeremy Howell
    • Nafasi, BBC
  • Muda wa kusoma: Dakika 4

Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, Israel imetuma maelfu ya wanajeshi huko Gaza na kusini mwa Lebanon, imefanya maelfu ya mashambulizi ya angani dhidi ya maadui zake, na kutumia mamilioni ya dola kwenye mifumo yake ya ulinzi wa anga ili kuzuia makombora na ndege zisizo na rubani.

Serikali ya Israel inakadiria kuwa vita vyake dhidi ya Hamas na Hezbollah vimegharimu zaidi ya dola bilioni 60.

Pia unaweza kusoma

Gharama ya vita vya Israel

azx

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Waziri wa Fedha wa Israel Bezalel Smotrich anasema vita vya sasa vimeigharimu Israel zaidi ya dola bilioni 60

Ni vita vya muda mrefu zaidi na vya gharama kubwa zaidi katika historia ya Israel," Waziri wa Fedha wa Israel Bezalel Smotrich aliliambia Bunge la Israel, Knesset mwezi Septemba 2024.

Smotrich aliongeza kuwa gharama ya operesheni za kijeshi zinaweza kuwa kati ya dola bilioni 54 na bilioni 68 za Kimarekani.

Hapana shaka kuwa mashambulizi ya Israel dhidi ya Lebanon na uvamizi wake wa kijeshi kusini mwa nchi hiyo, mbali na makombora iliyorusha kukabiliana na mashambulizi ya anga kutoka Iran, yataongeza zaidi gharama ya vita hivyo.

Amr El-Garhi, mwanauchumi katika Chuo Kikuu cha Sheffield Hallam nchini Uingereza, anasema baada ya kupanuka kwa vita hivyo, huenda gharama ikapanda hadi dola bilioni 93 ikiwa vita vitaendelea hadi 2025.

Benki ya Israel iliongeza dhamana za serikali na kukopa ili kulipia vita. Iliongeza dola 8 bilioni katika mauzo ya dhamana mwezi Machi 2024.

Israeli huuza dhamana kwa wakopeshaji wa ndani na nje ya Israel, ikijumuisha Wayahudi wa nje ya Israel.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Takwimu za Benki ya Israel zinaonyesha kuwa wageni wamekuwa na nia ndogo ya kununua bondi za serikali ya Israel.

Benki hiyo inasema ilipata asilimia 8.4 pekee kutoka nje ya nchi, ikilinganishwa na asilimia 14.4 Septemba 2023, mwezi mmoja kabla ya kuzuka kwa mzozo wa Israel na Hamas.

“Kutokana na hali hiyo, viwango vya riba kwenye hati fungani za serikali vilipanda, ili kuwavutia zaidi wanunuzi wa kigeni,” anasema Profesa Manuel Traelenberg, mwanauchumi katika Chuo Kikuu cha Tel Aviv.

Dk. Tomer Fadlon wa Taasisi ya Mafunzo ya Usalama wa Taifa mjini Tel Aviv anasema hali jumla ya kifedha ya Israel iko vizuri.

Profesa Karnit Flug, mwanauchumi katika Taasisi ya Israel Democracy Institute na gavana wa zamani wa Benki ya Israel, anasema serikali huenda ikapunguza bajeti ya dola bilioni 9.9 na kukawa na ongezeko la kodi katika jaribio la kupunguza nakisi ya bajeti ya serikali.

Hata hivyo, Flug anaamini "baadhi ya hatua zilizopangwa zitakabiliwa na upinzani kutoka kwa vyama vya wafanyakazi na baadhi ya maafisa wa serikali.”

Wanauchumi wengi wanaishauri serikali ya Israel kuchapisha bajeti yake ya 2025 sasa, na kuweka mgao kwa sekta mbalimbali ili kukabiliana na ongezeko la matumizi ya kijeshi.

Profesa Esteban Klor wa Chuo Kikuu cha Hebrew University huko Jerusalem anasema: “Hakuna mipango ya kupunguza bajeti yoyote ili kufadhili gharama za vita. Hakuna mkakati wa kiuchumi kwa vita na mkakati wa kijeshi.

Kuna athari gani kwa uchumi wa Israel?

dx

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Gavana wa zamani wa Benki ya Israel Karnit Flug anasema serikali inaweza kuongeza ushuru ili kupunguza nakisi ya bajeti ya serikali.

Uchumi wa Israel ulikuwa unakua kwa kasi hadi Oktoba 2023, lakini ulipungua kukuwa baada ya kuzuka kwa vita. Katika mwaka huo mzima, Pato la Taifa kwa kila mtu lilipungua kwa asilimia 0.1, kulingana na Benki ya Dunia.

Benki ya Israel inatarajia kuwa ukuaji wa uchumi katika kipindi cha 2024 utaongezeka kwa asilimia 0.5 pekee. Na kuweka kando utabiri wa mwezi Julai, kwamba ukuaji wa uchumi 2024 ungekuwa wa asilimia 1.5.

Katika mwaka uliopita, kampuni nyingi nchini Israel zimekumbwa na uhaba wa wafanyakazi, na hivyo kupunguza kiwango cha biashara wanachoweza kufanya.

Sababu ya hilo ni kwamba vikosi vya Israel viliwaita wanajeshi wa akiba zaidi ya 360,000 mwanzoni mwa mzozo na Hamas.

Tangu wakati huo wengi wao wamerudi, lakini imewaita wengine wa akiba 15,000 kwa ajili ya operesheni ya sasa ya ardhini nchini Lebanon.

Serikali pia iliwazuia Wapalestina wapatao 220,000 kutoka Gaza na Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu kuvuka kuingia Israel kufanya kazi kwa sababu za kiusalama.

Hilo iliathiri sana sekta ya ujenzi, ambayo iliajiri Wapalestina wapatao 80,000, na kuwabadilisha na maelfu ya wafanyakazi kutoka nchi kama vile India, Sri Lanka na Uzbekistan.

Profesa Flug anasema kufuatia kudorora kwa uchumi wa Israel wakati wa vita, kuna "uwezekano wa uchumi kuimarika baada tu ya vita, kutokana na kuimarika kwa sekta ya teknolojia ya Israel, ambayo sasa ni ya tano kwa kukuza uchumi huo.

Lakini, "kwa sababu vita hivi vimekuwa vya muda mrefu zaidi kuliko vita vya hapo awali, na vimeathiri sehemu kubwa ya watu, hilo linaweza kufanya kuimarika kwake kuchukua muda mrefu," anasema Fluge.

Pia unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Rashid Abdallah na kuhaririwa na Seif Abdalla