Ufaransa V Morocco: Je nani kutinga fainali dhidi ya Argentina?

.

Chanzo cha picha, BBC Sport

Maelezo ya picha, Kylian Mbappe na Hakim Ziyech

Mashabiki wa Morocco ndio wamekuwa na kelele zaidi kwenye Kombe hili la Dunia lakini wanaweza kusaidia timu yao kushinda nusu fainali dhidi ya Ufaransa?

"Ningependa kuona Morocco ikifanikiwa, kwa sababu ya usaidizi wa ajabu wa timu hiyo," mtaalam wa soka wa BBC Sport Chris Sutton alisema.

"Mashabiki wa Argentina waliiburuza timu yao katika mechi - ilikuwa kama mchezo wa nyumbani kwao dhidi ya Uholanzi katika nane bora, na ikawa vivyo hivyo dhidi ya Croatia.

"Nikiwa na Morocco, pia nadhani itakuwa hadithi nzuri kwa timu ya Afrika kufanya hivyo. Mara nyingi sana kwenye michuano hii, tunapuuza timu kutoka nje ya Ulaya na Amerika Kusini, lakini Morocco imewafanya watu kuwa na fikra tofauti .

"Watakuwa chaguo langu la kimapenzi kutinga fainali, lakini sina uhakika sana kuhusu nafasi zao dhidi ya Ufaransa."

Sutton anatabiri matokeo ya kila mechi nchini Qatar.

Alichagua mshindi katika mechi mbili kati ya nne za robo fainali - akipata alama kamili katika ushindi wa Morocco dhidi ya Ureno na ushindi wa Ufaransa dhidi ya Uingereza - na mechi tano kati ya nane za 16 bora.

Hiyo ilitosha kudumisha kiwango chake cha mafanikio cha 55% katika dimba hilo, baada ya kuchagua matokeo sahihi katika michezo 26 kati ya 48 ya kundi.

Kabla ya Kombe la Dunia kuanza, Sutton alichagua timu 12 kati ya 16 zilizofuzu kwa hatua ya kwanza ya mtoano, ikiwa ni pamoja na Ufaransa, chaguo lake la kushinda michuano hiyo, na Uingereza, ambayo alisema kwa usahihi itatinga hadi nane bora.

Matokeo Nusu finali - Utabiri wa Sutton

Jumanne, 13 Dec

Argentina v Croatia 3-0 1-0

Jumatano, 14 Dec 

France v Morocco x-x 2-1

Argentina 3-0 Croatia : Utabiri wa Cris Sutton watimia

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Messi na Modric
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kama vile Diego Maradona alivyopata ushindi wa Argentina 1986 huko Mexico na mshambuliaji wa Brazil Ronaldo alipoandikisha hadithi ya ukombozi huko Yokohama katika ushindi wao wa 2002, hili litajulikana kama Kombe la Dunia la Messi ikiwa ataendeleza ushindi dhidi ya Ufaransa au Morocco katika fainali.

Kampeni ya Argentina nchini Qatar ilifunguliwa kwa fedheha ya kile ambacho bado ni mshtuko mkubwa zaidi wa Kombe la Dunia, waliposhindwa na Saudi Arabia.

Lakini namna bwana Messi na mwanafunzi wake Julian Alvarez walivyoiondoa Croatia katika ushindi wa 3-0 wa nusu fainali ilitoa onyo la kutisha kwamba wanafikia kilele ambacho mashabiki wao hawakudhania kwenye Uwanja wa Lusail

Kwa hivyo, yote yamerudi katika uwanja wa Lusail siku ya Jumapili ili kuona iwapo Argentina inaweza kushinda Kombe la Dunia la tatu katika fainali yao ya sita na ikiwa Messi aambaye ametajwa kuwa mchezaji bora zaidi kuwahi kutokea katika soka anaweza hatimaye kupata zawadi ambayo imekuwa ikimponyoka kwa muda mrefu.

Je Morocco itafurukuta mbele ya Ufaransa?

.
Maelezo ya picha, Bendera ya Ufaransa na Morocco

Mpango wa Morocco, kulinda lango lao na baadaye kushambulia kwa kasi, unaonekana kuwa rahisi lakini si rahisi kuutekeleza kama walivyofanya dhidi ya timu zilizokamilika.

Bao pekee waliloruhusu katika michezo mitano nchini Qatar ni bao la kujifunga wenyewe dhidi ya Canada katika hatua ya makundi. Pia wamekutana na Croatia, Ubelgiji, Uhispania na Ureno kwenye Kombe hili la Dunia na hakuna hata mmoja wao aliyenusurika.

Wasiwasi wangu ni kwamba majeraha na uchovu utawaathiri hapa. Romain Saiss alitolewa dhidi ya Ureno, huku kumekuwa na shaka juu ya utimamu wa beki mwenzake Nayef Aguerd na kiungo muhimu Sofyan Amrabat.

Morocco hushambulia kwa kasi ya hali ya juu na nina uhakika watapata fursa sawa katika mchezo huu.

Sioni ikifanikiwa wakati huu kwasababu watalazimika kusukumwa sana licha ya kwamba wanaonekana kuweza kuzuia .

Njia bora ya kuelezea Ufaransa ni kwamba watatafuta njia na ndivyo ninatarajia, huku Olivier Giroud akiwa na sauti nyingine kubwa katika matokeo.

Ufaransa hawachezi soka la kustaajabisha lakini ni wazuri kuwatazama kwa sababu wana wachezaji wengi wenye kuvutia macho, na wanaonekana kufanya vizuri na kuendeleza kiwango cha juu kwa muda mrefu.

Hivyo ndivyo walivyopitia robo-fainali yao - walikuwa wakatili zaidi kuliko England walipopata nafasi zao.

Ni ubora huo katika ushambuliaji ambao unapaswa kuleta mabadiliko katika mchezo huu pia. Ninaiunga mkono Ufaransa kufunga bao la kwanza na kupata ushindi.

Morocco watafunga, na watategemea kadiri ya ubora n uwezo wao, lakini ninahofia huu utakuwa mchezo ambao hawatauweza

Ningependa kukosolewa, kwa sababu timu hii ya Afrika imekuwa hadithi bora zaidi katika Kombe hili la Dunia, lakini pengine hapa ndipo wanapoaga.