Tetesi za Soka Ulaya Alhamis: Man City, Liverpool zapigana vikumbo kwa Wirtz

s

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 2

Manchester City wamekutana na mshambuliaji wa Bayer Leverkusen Florian Wirtz, 22, kuhusu uhamisho katika majira ya joto. (Bild)

Hata hivyo, Liverpool pia wamewasiliana na Wirtz kuonyesha nia ya kumsajili kiungo huyo mshambuliaji katika majira haya ya joto. (Athletic)

Klabu za Ligi Kuu ya England zikiwemo Manchester City na Arsenal zinamnyatia mshambuliaji wa Real Madrid Rodrygo, 24, kufuatia ripoti za Mbrazil huyo kutoelewana na baadhi ya wafanyakazi wa klabu. (AS)

Real Madrid wako tayari kulipa pauni milioni 50 kumnunua beki wa kati wa Kihispania Dean Huijsen, 20, kutoka Bournemouth. (Sky Sports)

Dean Huijsen

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Dean Huijsen

Mshambuliaji wa Manchester United Joshua Zirkzee, 23, anasakwa na Inter Milan katika majira ya joto baada ya kiwango kibovu alichooshesha Mholanzi huyo msimu huu. (Corriere dello Sport)

Liverpool hawatakubali ada ya pauni 850,000 kutoka Real Madrid kumruhusu beki Trent Alexander-Arnold, 26, kuhamia klabu hiyo ya Uhispania mapema ili acheze michuano ya kombe la dunia kwa vilabu. (Sun)

Newcastle wamewapita Chelsea katika kinyang'anyiro cha kumsajili beki wa Kiingereza Marc Guehi, 24, kutoka Crystal Palace. (Teamtalk)

Bayern Munich wamekubaliana ada na Bayer Leverkusen kumsajili beki wa kati wa Ujerumani Jonathan Tah, 29. (Fabrizio Romano)

s

Chanzo cha picha, Getty Images

Barcelona wana nia ya kushindana na Arsenal katika kumsajili kipa wa Espanyol Joan Garcia, 24. (AS)

Barcelona wako tayari kuwaondoa hadi wachezaji nane wa kikosi cha kwanza katika majira haya ya joto ili kupata fedha za kusajili wachezaji wapya na kuboresha mikataba ya waliopo. (Mirror)

Barca wanataka kumsajili beki wa kati, beki wa pembeni na winga wa kumsaidia nyota wa Hispania mwenye umri wa miaka 17 Lamine Yamal. (Espn)

Xavi Simons wa RB Leipzig yuko tayari kuondoka klabuni hapo katika majira haya ya joto, licha ya kiungo huyo Mholanzi mwenye umri wa miaka 22 kusaini mkataba wa kudumu mwezi Januari. (Fabrizio Romano)

Bristol City wanataka kumbakisha mshambuliaji Nahki Wells, 34, msimu ujao baada ya kushindwa kufuzu kwa Ligi Kuu kupitia mchujo wa Championship. (Sky Sports)