Tetesi za soka Ulaya Jumatatu: Leroy Sane njia panda Bayern

Leroy Sane

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 2

Bayern Munich hawakusudii kuboresha ofa yao ya mkataba kwa winga wa Ujerumani, Leroy Sane, licha ya mawakala wapya wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 - ambaye mkataba wake unaisha msimu huu wa joto kuwasilisha pendekezo jipya kwa mabingwa hao wa Bundesliga. (Florian Plettenberg, Sky Sports Germany)

Mkurugenzi wa michezo wa Napoli, Giovanni Manna, anaendelea kukaa kimya kuhusu kumsajili kiungo wa Ubelgiji, Kevin de Bruyne, mwenye umri wa miaka 33, kwa uhamisho huru atakapoondoka Manchester City mwishoni mwa mkataba wake msimu huu wa joto. (Calciomercato)

Mshambuliaji wa Canada, Jonathan David, atakuwa mchezaji huru mkataba wake na Lille utakapomalizika msimu huu wa joto na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anasakwa na Napoli. (La Gazzetta dello Sport)

c

Chanzo cha picha, Getty Images

Bosi wa Bayer Leverkusen, Fernando Carro, anaamini kuna nafasi 50-50 kwa kiungo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 22, Florian Wirtz, ambaye amehusishwa na Bayern Munich, kuweza kusalia na klabu hiyo. (Sky Sports Germany)

Beki wa kati wa Arsenal, Jakub Kiwior, yupo kwenye rada za Juventus na Inter Milan huku beki huyo wa Poland mwenye umri wa miaka 25 akipima mustakabali wake wa muda mrefu. (Football Insider), external

Real Madrid wanafanya mazungumzo na Liverpool kuhusu kutoa takriban pauni milioni 1 ili beki wa England mwenye umri wa miaka 26, Trent Alexander-Arnold, ajiunge nao mapema kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia la Klabu. (Football Insider)

s

Chanzo cha picha, Getty Images

Meneja wa zamani wa Everton na Burnley, Sean Dyche, ni miongoni mwa makocha wanaowania kuchukua nafasi ya ukocha pale Leicester City, huku Foxes wakitarajiwa kuachana na kocha wao wa sasa, Ruud van Nistelrooy (Talksport).

Kiungo wa Brazil, Douglas Luiz, anasema anakumbuka sana alivyokuwa anacheza mara kwa mara Aston Villa wakati huu akihangaika kupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza Juventus, ambao walimsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kutoka klabu hiyo ya Midlands msimu uliopita wa joto. (Twitch, via Birmingham Mail),

Brighton ni miongoni mwa klabu kadhaa zinazotaka kumsajili beki mwenye umri wa miaka 21, Diego Coppola, ambaye anacheza katika klabu ya Serie A, Hellas Verona. (Fabrizio Romano)

AC Milan wanamtaka beki wa kati wa Feyenoord, David Hancko, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka Bayer Leverkusen na Juventus ambazo zinamtaka pia mchezaji huyo wa kimataifa wa Slovakia mwenye umri wa miaka 27. (Calciomercato)