Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kherson: Je ni pigo kwa Urusi au mtego kwa Ukraine?
Vyombo vya Habari ulimwenguni vinachambua taarifa ya Urusi kuondoa vikosi vyake kutoka Kherson. Wanaosoma taarifa hizo, wanasisitiza tahadhari katika ujumbe wanaotuma.
Huu kwa wepesi sio ushindi kwa Urusi, lakini ni mapema mno kujadili kuhusu Ukraine kunyakua udhibiti kamili wa Kherson. "Ushindi mkubwa kwa Kyiv, inayobadili mpangilio wa kijeshi usiku wa kuamkia majira ya baridi," imeandika Financial Times.
Gazeti hilo kama mengine mengi ya mataifa ya magharibi linakumbuka kwamba ni mpaka hivi karibuni mji mzima wa Kherson – eneo pekee la kati la Ukraine lililodhibitiwa na Urusi – ulikuwa umejaa picha zenye ujumbe kuwa Urusi ipo hapa daima, lakini ki uhalisia, ‘daima’ ilidumu kwa takriban miezi minane tu.
Gazeti hilo la FT limenukuu maoni ya wachambuzi na duru za ki intelijensia: wakati jeshi la Ukraine litakapoingia Kherson hatua hii itaipa jeshi la nchi hiyo fursa nzuri ya kuvishambulia vikosi vya Urusi.
Lakini ni mapema kusema kwamba hili haliwezi kuepukika na litadhoofisha jeshi la Urusi.
Kwa muda mrefu Urusi imekuwa ikijiimarisha katika ukingo wa mashariki wa Dnieper, na iwapo ukingo wa magharibi ni kwa ukubwa eneo tambarare, basi njia za maji na maeneo yenye unyevu yatasaidia kupaimarisha hapa. Mchambuzi wa masuala ya kijeshi Rob Lee anafahamisha kwamba kufikia kingo za Dnieper karibu na Kherson kutaipatia Ukraine uwezo wa kushambulia vituo vya reli, maghala na vituo vingine angalau katika eneo la kaskazini la Crimer lililotengwa mnamo 2014. Wachambuzi wa BBC wanataja kuwa maafisa Ukraine wanatahadhari pakubwa kuhusu kauli za uongozi wa jeshi la Urusi kuhusu kujiondoa kwa wanajeshi wake. Na jeshi la Ukraine linanuia kuitazama hali kwa makini wakati wanaingia mjini humo. BBC pia inataja muitikio kutoka maafisa wa mataifa ya magharibi kuhusu kuondoka kwa wanajeshi hao huko Kherson. Kwa jumla wamefurahi kwamba usaidizi wa silaha uliotolewa kwa Ukraine, unafua dafu.
Mchambuzi wa masuala ya kisiasa kutoka Uingereza, Mark Galeotti, ambaye ni mmoja wa wataalamu kuhusu Urusi amezungumza na BBC Radio 4.
Ameonya dhidi ya kukata shauri haraka lakini kwa maoni yake kuondoka kwa vikosi hivyo Kherson kunamaanisha kuwa iwapo Urusi ilikuwa ikifikiria kuhusu kushinda vita pekee, sasa imeanza pia kufikiria kuhusu vipi isishindwe. "Je ni mtego?" linauliza jarida la Economist. Lakini mwandishi anaandika kuwa duru katika taarifa hiyo zinathibitisha kuhusu kuondoka kwa vikosi.
Na mlipuko katika kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia maji cha Kakhovskaya, ambao kama vyombo vya habari viliripoti, huenda kilitegwa na wanajeshi wa Urusi kabla ya kuondoka, utasababisha hasara zaidi kwa Urusi yenyewe kuliko kwa Ukraine.
CNN linaieleza hali hiyo kuwa ni "Izara lakini iliyotabirika," Mchambuzi wa masuala ya kijeshi wa CNN Tim Lister anasema "Kwa kiwango hiki, haijulikani Ukrain itaitikiaje," Anaeleza kwamba vikosi vimepungua katika maeneo ya mbele ya vita katika eneo la kusini na ardhi inayowakabili mbele huenda imetegwa kwa mabomu. Lister anaamini kwamba kihikima, mbinu inayotumia Urusi inaeleweka, la muhimu kwa kamanda wa jeshi hilo la Urusi Sergei Surovikin, inaonekana ni kuimarisha maeneo ya ulinzi baada ya miezi kadhaa ya changamoto. Lakini kisiasa, kuondoka kwa wanajeshi hao ni ushindi mkubwa dhidi yao. Televisheni ya Al Jazeera pia inazungumzia athari hizo za kisiasa kwa Urusi. Imechambua ripoti za vyombo vya habari vinavyounga mkono serikali na vituo vya Telegram, baadhi yao vina maelfu au hata mamilioni ya watazamaji.
Watangazaji wanalazimika kuzungumza kuhusu ‘uamuzi mgumu’ au kutaja kwa uchungu kuwa Urusi inakabidhi maeneo ambayo hapo awali iliyadhibiti na kutangaza ni yake.