Wanajeshi
wa Ukraine wamekaribishwa mjini Kherson na wakaazi waliojawa na furaha, baada
ya Urusi kusema kuwa imejiondoa kikamilifu katika mji huo muhimu wa kusini.
Video
ilionyesha wenyeji mitaani, wakipeperusha bendera ya taifa ya Ukraine na kuimba
huku wanajeshi wa Kyiv wakiwasili.
Wengine
waliimba nyimbo za kizalendo karibu na moto mkubwa wa kambi hadi usiku.
Kherson
ilikuwa mji mkuu wa kikanda pekee uliochukuliwa na Urusi baada ya uvamizi wa
Februari. Kurudi nyuma kumeonekana kama moja ya vikwazo vyake vikubwa vya vita.
Moscow
ilisema wafanyakazi 30,000 wametolewa nje ya eneo hilo - pamoja na vipande
karibu 5,000 vya vifaa vya kijeshi, silaha na mali nyingine.
Ikulu ya
White House ilisifu kile ilichokiita "ushindi wa ajabu", huku Rais wa
Ukraine Zelensky akiitaja "siku ya kihistoria".
Lakini
waziri wa mambo ya nje wa Ukraine alisema "vita vinaendelea".
Akizungumza nchini Cambodia kando ya mkutano wa kilele wa nchi za Asia, Dmytro
Kuleba alisema: "Tunashinda vita vya chinichini. Lakini vita
vinaendelea."
Taarifa
ya jioni siku ya Ijumaa kutoka upande wa Ukraine ilisema kuwa wanajeshi
walikuwa wamesonga mbele hadi ukingo wa magharibi wa mto Dnipro.
Picha
pia ziliibuka zikionyesha kuwa kivuko kikuu cha mto - Daraja la Antonivsky -
kilikuwa kimeporomoka kwa kiasi. Bado haijafahamika jinsi uharibifu huo
ulivyosababishwa.
Wanajeshi
wa Urusi walioikalia Kherson wanafikiriwa kuchukua nafasi mpya upande wa
mashariki wa mto.
Mkazi wa
Kherson alielezea hisia zake "zinazolemea" wakati watu walipoibuka
wakiimba na kucheza barabarani.
Alexei
Sandakov alifichua jina lake kamili kwa BBC, hapo awali alijiita
"Jimmy". Alisema Kherson alikuwa "huru sasa. Ni tofauti. Kila
mtu analia tangu asubuhi".
Aliongeza
kuwa "kila mtu alitaka kukumbatia" askari wa Kiukreni waliowasili.
Mabadiliko
ya udhibiti wa jiji hilo yalifuatia shambulio la haraka la Kiukreni katika
miezi ya hivi karibuni, ambapo Kyiv ilisema kuwa imeteka tena makazi 41 karibu
na Kherson.
Katika
hotuba yake ya jioni, Rais Zelensky alisema watu wa Kherson "walikuwa
wakisubiri" na "hawakukata tamaa juu ya Ukraine".
Aliongeza
kuwa wakaazi wamekuwa wakifanya kazi ya kuondoa "athari zozote za
wakaaji" kutoka barabarani, zikiwemo nembo za Kirusi.
Wakati
huo huo, msemaji wa Rais wa Urusi Vladimir Putin alikanusha hatua hiyo
iliwakilisha kushindwa kwa aibu.