DR Congo: Je taifa hili limelaaniwa na utajiri wake?

Muda wa kusoma: Dakika 6

Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) kumeshuhudiwa mzozo na ukosefu wa utulivu …Kwa muda usiokuwa chini ya miongo mitatu. Ila katika muongo mmoja uliopita, mapigano makali yamezuka mara kwa mara.

Japo eneo hilo linalojumuisha majimbo ya Ituri, Kivu kusini na Kivu Kaskazini yana jumla ya makundi ya wapiganaji zaidi ya 129, kundi la waasi la M23, ambalo ndilo kuu lililobuniwa baada ya makubaliano ya Machi 23 ya kutafuta amani imekuwa na historia ya machafuko.

Kundi la M23 lilipata umaarufu kwa mara ya kwanza mwaka 2012 kwa kuuteka mji mkuu wa Goma kwa muda mfupi. Baada ya makubaliano ya amani mwaka 2013, wapiganaji wengi wa M23 walijumuishwa katika jeshi la taifa.

Kundi hilo lilianza tena mapigano mwishoni mwa 2021, likisema DRC imeshindwa kuheshimu ahadi ya kuwajumuisha wapiganaji wake katika jeshi, miongoni mwa malalamishi mengine.

Vita, ukoloni, utumwa, ufisadi - Haya yote yamebadilisha taifa hili ambalo licha ya kuwa miongoni mwa mataifa tajiri zaidi duniani, sasa limekuwa masikini zaidi.

Lakini ni nini haswa kinachosababisha vita visivyoisha katika sehemu inayoonekana kubarikiwa na kila aina ya madini? ,anaandika mwanahistoria Dan Shaw

Maamuzi yaliofanywa karne ya 15

Mwishoni mwa Karne ya 15 himaya inayojulikana kama Ufalme wa Congo ilitawala sehemu ya magharibi ya Congo, na sehemu za majimbo mengine ya kisasa kama vile Angola.

Na wakati Wafanyabiashara wa Ureno walipowasili kutoka Ulaya katika miaka ya 1480, waligundua kuwa walikuwa wameingia kwenye nchi yenye utajiri mkubwa wa asili, tajiri wa rasilimali .

Walifanya kila wawezalo kuharibu nguvu yoyote ya kisiasa au kiasili ilioweza kupunguza masilahi yao ya utumwa au biashara.

Pesa na silaha za kisasa zilitumwa kwa waasi,ambapo majeshi ya Congo yalishindwa, wafalme waliuawa, wasomi walichinjwa na kujitenga kulihimizwa.

Kufikia karne ya 16, ufalme huo uliokuwa na nguvu ulikuwa umegawanyika vipande vipande katika hali isiyo na kiongozi, huku vita vya wenyewe kwa wenyewe vikiripotiwa.

Watumwa, wahasiriwa wa mapigano haya, walichukuliwa na kusafirishwa hadi Marekani. Takriban watu milioni nne walipelekwa kwa nguvu kwenye mdomo Mto Congo.

Meli za Uingereza zilitumika kufanya biashara hiyo huku miji ya Uingereza na wafanyabiashara wake wakitajirika kwa rasilimali za Congo ambazo hawakuziona .

Ushirikiano wa kwanza na Wazungu ndio uliokuwa chapa cha madhila wanayopitia raia wa Congo hadi sasa.

Maendeleo yamedumazwa, serikali zimekuwa dhaifu na utawala wa sheria haupo.

Hii haikusababishwa na Wacongo wenyewe bali maslahi ya wenye nguvu kuharibu, kukandamiza na kuzuia serikali yoyote yenye nguvu, imara na halal kushamiri

Utajiri wa DR Congo

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inachukuliwa kuwa nchi tajiri zaidi duniani kwa maliasili.

Madini mengi ghafi hayajatumika na yanadaiwa kuwa`na thamani ya hadi takriban $24 trilioni. Amana hizi ni pamoja na akiba kubwa zaidi ya madini ya coltan na kiasi kikubwa cha madini ya kobalti.

Hatajivyo kutokana na urahisi wa uchimbaji wa rasilimali hizo taifa hilo limelaaniwa kabisa na utajiri wake wa madini hayo.

Maji yasiyo na kikomo, kutoka mto wa pili kwa ukubwa duniani, Congo, hali nzuri ya hewa na udongo wenye rutuba mbali na madini kama vile shaba, dhahabu, almasi, urani, koltani na mafuta ni baadhi tu ya madini ambayo yanapaswa kuifanya kuwa moja ya nchi tajiri zaidi duniani.

Badala yake ni ulimwengu usio na matumaini.

Mfalme Leopold wa Ubelgiji

Mambo ya ndani ya Congo yalifunguliwa mwishoni mwa Karne ya 19 na mpelelezi mzaliwa wa Uingereza Henry Morton Stanley, ndoto zake za mahusiano ya biashara huria na jumuiya alizokutana nazo zilikatishwa na Mfalme maarufu wa Ubelgiji, Leopold, ambaye alianzisha ufalme mkubwa.

Umaarufu wa baiskeli ya marehemu Victoria iliwezeshwa na raba ya Kongo uliokusanywa na vibarua na watumwa.

Ili kufahamu hilo, wanaume wa Kongo walikusanywa na kikosi cha kikatili cha usalama kilichokuwa na afisa wa Ubelgiji, wake zao waliwekwa ndani ili kuhakikisha kwamba wanafuata sheria na walitendewa ukatili wakati wa utumwa wao. Kisha wanaume hao walilazimika kwenda msituni na kuvuna raba hiyo.

Kutotii au upinzani ulikabiliwa na adhabu ya papo hapo - kuchapwa viboko, kukatwa mikono, na kifo. Mamilioni waliangamia.

Viongozi wa kikabila wenye uwezo wa kupinga waliuawa, jamii ya kiasili iliharibiwa, mbali na kunyimwa elimu ifaayo.

Utamaduni wa utawala wa kikatili, wa kishenzi na wasomi wa Ubelgiji ambao hawakuwa na nia kabisa ya kuendeleza nchi au idadi ya watu uliundwa, na umedumu.

Katika hatua iliyopaswa kukomesha ukatili huo, Ubelgiji hatimaye ilitwaa Congo moja kwa moja, lakini matatizo katika koloni lake la zamani yalibakia.

Uchimbaji madini uliongezeka, wafanyikazi waliteseka katika hali mbaya, wakizalisha nyenzo ambazo zilichochea uzalishaji wa viwandani huko Yuropa na Marekani.

Vita vya pili vya dunia

Katika Vita vya Kwanza vya dunia, watu waliokuwa katika mstari wambele kutoka Magharibi na kwingineko walikufa, lakini ni madini ya Kongo ambayo yalisababisha mauaji hayo.

Maganda ya risasina makombora ya washirika yaliyopigwa Passchendaele yalikuwa na 75% ya shaba ya Congo.

Katika Vita vya dunia vya pili, madini ya uranium ya mabomu ya nyuklia yaliodondoshwa huko Hiroshima na Nagasaki yalitoka kwenye mgodi wa kusini-mashariki mwa Congo.

Uhuru wa Magharibi ulitetewa na rasilimali za Congo huku Wakongo weusi wakinyimwa haki ya kupiga kura, au kuunda vyama vya wafanyakazi na vyama vya kisiasa. Walinyimwa chochote zaidi ya elimu ya msingi zaidi.

Waliwekwa katika kiwango cha chini cha maendeleo ambacho kiliwafaa watawala na wamiliki wa migodi lakini walihakikisha uhuru ukifika hakuna wasomi wa nyumbani wanaoweza kuendesha nchi.

Kwa hivyo, uhuru wa 1960 ulikuwa mbaya sana.

Makundi ya nchi hiyo kubwa yalijaribu kujitenga mara moja, jeshi likawaasi maafisa wake wa Ubelgiji na baada ya wiki kadhaa wasomi wa Ubelgiji ambao waliendesha serikali walihama na kutoacha mtu yeyote mwenye ujuzi wa kuendesha serikali au uchumi.

Uongozi wa Mobutu

Kati ya kazi 5,000 za serikali kabla ya uhuru, tatu tu zilishikiliwa na WaCongo na hakukuwa hata na mwanasheria mmoja wa Congo, daktari, mwanauchumi au mhandisi.

Machafuko yalitishia kukumba eneo hilo. Watawala wa Vita Baridi walihamia kuzuia wengine kufaidika .

Akiwa ameingizwa katika matatizo hayo , kiongozi wa Congo, Patrice Lumumba, alipigwa vibaya na kuuawa na waasi wanaoungwa mkono na nchi za Magharibi. Mwanajeshi mwenye nguvu, Joseph-Desire Mobutu, ambaye miaka michache kabla alikuwa sajenti katika jeshi la polisi wa kikoloni, alichukua nafasi.

Mobutu akawa mbabe. Mnamo 1972 alibadilisha jina lake kuwa Mobutu Sese Seko Nkuku Ngbendu Wa Za ​​Banga, akimaanisha "shujaa mwenye nguvu zote ambaye, kwa sababu ya uvumilivu wake na nia yake isiyobadilika ya kushinda, anatoka kwenye ushindi hadi ushindi, akiacha moto katika hali yake".

Nchi za Magharibi zilimvumilia maadamu madini yalitiririka na Congo iliwekwa nje ya mzunguko wa Usovieti.

Yeye, familia yake na marafiki walifyonza mabilioni ya dola, jumba la dola milioni 100 lilijengwa katika msitu huko Gbadolite, huku uwanja wa ndege karibu na jumba hilo ukiundwa kuingiza ndege ya Concorde, ambayo ilikodishwa kwa safari za kufanya manunuzi mjini Paris.

Wapinzani waliteswa au kununuliwa, mawaziri waliiba bajeti nzima, serikali ilidharauliwa. Nchi za Magharibi ziliruhusu utawala wake kukopa mabilioni, ambayo yaliibiwa .

Mwaka 1997 muungano wa mataifa jirani ya Afrika, ukiongozwa na Rwanda - ambayo ilikuwa na hasira na Congo ya Mobutu ambayo ilikuwa ikiwalinda wengi wa wale waliohusika na mauaji ya halaiki ya 1994 - walivamia, baada ya kuamua kumuondoa Mobutu.

Mkimbizi wa Congo, Laurent Kabila, aliondolewa Afrika Mashariki ili kuwa mtu mashuhuri. Jeshi la Mobutu lililokuwa na njaa ya pesa lilivamia.

Mobutu aliondoka kwa mara ya mwisho kutoka kwenye msitu wake wa Versailles, ndege yake ikiwa imesheheni vitu vya thamani, askari ambao hakuwalipa walifyatua risasi kwenye ndege hiyo ilipokuwa ikiruka angani.

Rwanda ilikuwa imemshinda jirani yake kwa urahisi sana. Hata hivyo, mara baada ya kuwekwa uongozini, Kabila, kibaraka wa Rwanda, alikataa kufanya kama alivyoambiwa.

Kwa mara nyingine tena Rwanda ilivamia, lakini safari hii walizuiliwa tu na washirika wake wa zamani wa Kiafrika ambao sasa walishambuliana na kuitumbukiza Kongo katika vita vya kutisha.

Majeshi ya kigeni yalipambana ndani kabisa ya Congo huku taifa hilo likiporomoka kabisa na machafuko kuenea.

Mamia ya vikundi vilivyojihami vilifanya ukatili, mamilioni walikufa.

Tofauti za kikabila na lugha zilichochea vurugu, wakati udhibiti wa utajiri wa asili wa Congo uliongeza udharura wa kutisha kwenye mapigano.

Askari watoto walioandikishwa kwa nguvu walikusanya watumwa kuchimba madini kama vile coltan, sehemu kuu ya simu za rununu, huku wakiangamiza jamii za maadui, kuwabaka wanawake na kuwafukuza walionusurika msituni, kufa kwa njaa na magonjwa.

Mabilioni ya paundi yaliozalishwa na madini hayo hayakuleta chochote isipokuwa taabu na kifo kwa watu hasa wanaoishi juu yao, huku wakiwatajirisha wasomi wachache huko Congo na wafadhili wao wa kigeni.