Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kwa nini Ukraine imekuwa na mafanikio makubwa dhidi ya Urusi na inakabiliwa na changamoto gani?
Usifurahie sana mafanikio makubwa dhidi ya wanajeshi wa Urusi ambayo Ukraine imepata, afisa mwandamizi wa Marekani alisema awali, wakati ambapo Urusi nayo inaendelea kusonga mbele huko Donbas.
Uwezo wa Ukraine umeshangaza na kuwa hatua muhimu iliyopigwa katika vita hivi. Kwa mara ya kwanza waliilazimisha Urusi kujiondoa kutoka Kyiv, mji mkuu, na kisha kufanya mashambulizi huko Crimea, rasi chini ya utawala wa Urusi tangu 2014.
Hata hivyo, licha ya kuwepo kwa hali ya utulivu na gharama kubwa kwa jeshi lake, Urusi ilikuwa imepata mafanikio makubwa katika eneo hili. Sasa ni Ukraine ambayo inaendelea kusonga mbele katika eneo hilo na kurejesha maelfu ya kilomita ya eneo lililokuwa limetwaliwa na Urusi kwa siku kadhaa tu.
Makabiliano makubwa ya Ukraine yamekuwa katika eneo la mashariki karibu Kharkiv.
Taarifa za hivi karibuni za kijasusi kutoka Uingereza zinaonyesha kwamba maeneo yaliyokombolewa yanajumuisha zaidi ya kilometa 3,000, ingawa ni vigumu kutaja kutokana na vita vinavyoendelea na ugumu wa ufikiaji eneo hilo kwa waandishi wa habari walioko vitani.
Ukraine inadai kuwa imeteka miji muhimu kama vile Izyum na Kupiansk, vituo vyenye vifaa vya usafirishaji vilivyotumiwa na Urusi kusambaza majeshi yake katika eneo la Donbas.
Kupoteza huko pekee ni pigo kubwa kwa jeshi la Urusi.
Mambo ya msingi yaliyochangia mafanikio ya Ukraine
Kufanya mambo kwa kushtukiza imekuwa nguzo muhimu kwa Ukraine. Hiyo na matumizi ya kijanja ya silaha za Magharibi, ikiwa ni pamoja na makombora ya masafa marefu ya Uingereza na Marekani, ili kuharibu laini za usambazaji za Urusi na silaha. Wiki iliyopita, Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin alisema kuwa makombora ya masafa marefu yamepiga zaidi ya maeneo lengwa 400 muhimu kipindi hiki.
Kabla ya kuja kwa silaha hizi, Urusi daima ilikuwa inapata ushindi upate wake. Sasa mambo yanaonekana kubadilika, huku maafisa wa ujasusi wa Marekani wakisema kuwa Urusi inatafuta msaada wa Korea Kaskazini ili kunasa mamilioni ya makombora, na kuashiria kuwa hifadhi yake ya silaha imeisha katika miezi sita ya vita.
Matokeo ya silaha hizi za Magharibi na uamuzi wa Ukraine wa kurejesha eneo yamewalazimisha majeshi ya Urusi katika kile kinachoonekana kuwa kurudi nyuma.
Picha katika mitandao ya kijamii zinaonyesha vifaru, magari ya kivita na silaha kuachwa nyuma kwa haraka.
Cha kushangaza, maendeleo ya kijeshi eneo la mashariki yamekuwa kwa kasi zaidi kuliko mashambulizi yaliyotangazwa sana na Ukraine eneo la kusini kuelekea mji wa Kherson.
Ukraine ilikuwa imezungumzia mashambulizi hayo kwa muda mrefu kabla ya kuanza, na kusalia kimya kuhusu mipango yake kwa ajili ya mashariki. Sasa mambo yote yanaonekana kuwa ni sehemu ya mpango wake: Kubadilisha fikra wakati inaficha yale iliyokuwa ikiyaandaa eneo la mashariki.
Ni wazi kwamba Ukraine ilifanikiwa kupotosha Urusi. Kwa miezi michache iliyopita, Urusi imekuwa ikipeleka vikosi vya kijeshi kutoka mashariki kwa lengo la kujihami kusini mwa nchi hiyo. Kwa sasa wanajeshi wa pande zote mbili wako katika hatari.
Kwa nini maendeleo ya kijeshi ya Ukraine pia inamaanisha hatari?
Ukraine inapata ugumu kusonga mbele katika maeneo ya kusini katika kusini, ambapo wanaonekana wazi kabisa na kupambana zaidi katika maeneo ya wazi. Jeshi linalosonga mbele linahitaji wanajeshi zaidi na nguvu ya silaha ili kulishinda jeshi pinzani.
Hatari kwa Ukraine kwa sasa ni sawa na vile Urusi ilikabiliwa katika awamu za awali za vita katika suala la silaha, vifaa na wanajeshi. Faida ikiongezeka, maeneo ya usambazaji pia yanazidi kuwa katika hatari ambako kunaweza kusababisha mashambulizi kutoka kwa Urusi.
Pia kuna hatari kwamba vikosi hivyo ambavyo vimesonga kuendelea kutengeneza ulinzi uliojizunguka, na hilo linaweza kusababisha wao kuzingirwa.
Pamoja na matumaini makubwa, Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Oleksii Reznikov alionya kwamba majeshi yake ya mashariki yanaweza kuwa katika hatari zaidi ya kushambuliwa na Urusi. Kuchukua eneo haitoshi.
Jeshi pia linatakiwa kushikilia ardhi iliyokomboa. Mashambulizi mawili ya Ukraine bado yanasalia kuwa hatari na kuna uwezelano ikapata pigo. Hata hivyo, hii ni zaidi ya kufanya mashambulizi ya ardhini, hata kama hilo ndiyo lengo kuu.
Ukraine inatuma ishara kwa dunia kwamba ni kweli inaamini inaweza kushinda vita hivi na inatumia mafanikio yake kuomba silaha zaidi kutoka Magharibi.
Shambulizi hili linakuja wakati muhimu. Msimu wa baridi unakaribia katika eneo la Ulaya, wakati ambapo itakuwa vigumu kupigana na hapo mapenzi ya nchi za Magharibi yatakuwa katika majaribu.
Vita hivi viko mbali na kumalizika, lakini kwa mara nyingine tena Ukraine inaonyesha dunia uwezo wake wa kushinda changamoto zake.