Sayansi inasema unaweza kuwa na pacha wako usiyemjua

Twins

Chanzo cha picha, Getty Images

Akiwa mtoto, Jeffrey Craig alikuwa na ndoto ya kuwa na pacha wake.

"Ndoto zilikuwa za kawaida na kila wakati ni zilikuwa zinafanana.

Kulikuwa na taswira ya mtu mwingine kama mimi ambaye alikuwa akilala kitandani karibu nami.

Hakuwa mgeni: Nilijua ni kivuli changu ama pacha wa mie.Ilikuwa ya kushangaza kidogo, lakini sikuogopa - kwa kweli ilikuwa ya kutuliza."

Wakati wa utafiti wake kama profesa mshiriki katika Taasisi ya Utafiti ya Watoto ya Murdoch huko Australia, Craig aligundua "ugonjwa wa kutoweka kwa pacha," kwa maana ya kwamba pacha mmoja alikufa mapema wakati wa ujauzito.

Mabaki ya pacha yanaweza kubaki kwenye mfuko wa uzazi ama uterasi au tishu zinaweza kusambaratika, na seli humezwa na pacha mwingine au plasenta.

Kusoma juu ya hii, Craig alianza kujiuliza ikiwa ndoto hiyo ilikuwa ya maana zaidi."Nilianza kujiuliza ikiwa nilikuwa na kumbukumbu ya mbali ya kuchangia mfuko wa uzazi na pacha," alisema Craig, ambaye sasa ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Matibabu cha Deakin University na naibu mkurugenzi wa Twins Research Australia.

Twins

Chanzo cha picha, Getty Images

Utafiti wa hivi majuzi juu ya mapacha waliopotea, ambao Craig hakuhusika, lakini ulikaguliwa, unaweza kusaidia kutatua siri yake.

Timu ya kimataifa ya watafiti pacha imegundua njia ya kubaini kama mtu alikuwa ni pacha mmoja - ikiwa pacha wake wa pili bado yuko hai au amepotea kabla hajazaliwa.

Usahihi wa njia hiyo unaelezwa kuwa ni karibu asilimia 60 hadi 80.

Craig anadhani ni uboreshaji mkubwa katika eneo hili, na pia ana hamu ya kutaka kujua zaidi.

Iwapo watafiti wataweza kutengeneza mtihani wa kutegemewa wa kubaini watu waliopoteza pacha tumboni, "Ningeweza kupima dhana kwamba ndoto niliyoota, na ambayo mtu mwingine kama mie niliyelala naye karibu yangu, iliundwa kwa sababu nilianza maisha yangu kama pacha,” aliandika kwenye barua pepe.

Uwezekano kuwa una pacha wako ni mkubwa

twins

Chanzo cha picha, Getty Images

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Uwezekano kwamba wakati mmoja ulikuwa pacha ni Mkubwa kuliko watu wengi wanavyofikiria.Kiwango cha mapacha wanaozaliwa pamoja na wapo hai ni takriban asilimia 1.3 tu.

Lakini kama asilimia 12 ya mimba zote zinazotungwa kiasili zinaweza kuanza zikiwa za mapacha, kulingana na utafiti mmoja.

Katika takriban mimba moja kati ya nane kama hizo, mmoja wa mapacha hutoweka, na kusababisha kuzaliwa pacha mmoja, utafiti unapendekeza.

Kwa wale wanaotumia mkono wa kushoto, uwezekano ni mkubwa zaidi kwa sababu uwezekano kwamba mapacha watakuwa wa kushoto pia ni mkubwa zaidi.

Wakati asilimia tisa ya idadi ya watu kwa ujumla wanatumia mkono wa kushoto, asilimia 15 ya mapacha wanaofanana na asilimia 12 ya mapacha wasiofanana wanatumia mkono wa kushoto.

Kuwasaidia watu kugundua ikiwa walianza maisha wakiwa mapacha kunaweza kuwa na athari muhimu kwa afya zao, baadhi ya wataalam wanasema.Inaweza pia kuchangia uelewa mzuri wa mapacha wanaofanana na ukuaji wao wa mapema - vipengele vingi ambavyo bado vimegubikwa na siri.

Kuna dhana tofauti kwa nini pacha hupotea.

"Inaweza kuwa kuna tatizo katika fetusi moja, au labda mama hana nafasi ya kutosha," Segal anasema."Kwa maneno ya matibabu, inaitwa 'disappearing twin syndrome' kwa sababu kuna mapigo mawili ya moyo kwenye ultrasound inayofanywa mapema, lakini baadaye moja inaonekana kutoweka," anasema van Dongen."Hata hivyo, wale ambao wamepoteza mimba ya mapacha wanapendelea kuiita mimba mfu."Wakati mwingine mabaki ya pacha wa pili yanaonekana.