Fahamu kwa nini hivi karibuni utakuwa na pacha wako wa kidijitali

Chanzo cha picha, Getty Images
Wengi wetu tumeambiwa kwamba tunaye mtu mmoja anayefanana nasi duniani.
Lakini fikiria iwapo una uwezo wa kutengeneza pacha wako anayefanana na wewe kabisa lakini akiwa na maisha ya kidijitali.
Tunaishi katika wakati ambao kila kitu kinachopatikana katika dunia halisia kimeundwa katika ulimwengu wa kidijitali: Miji yetu, nyumba zetu, na hata sisi wenyewe.
Sawa na ulivyo ulimwengu wa kidijitali meterverse}, ambapo kuna avatar kama wewe , mapacha wa kidijitali wamekuwa teknolojia mpya iliosambaa.
Pacha dijitali ni kielelezo kamili cha kitu katika ulimwengu halisi, lakini kwa dhamira moja: kusaidia kuboresha, au kutoa maoni kwa toleo la maisha halisi.
Hapo awali, mapacha hawa walikuwa tu mifano ya kisasa ya 3D ya kompyuta.
Lakini akili bandia (AI) pamoja na Mtandao wa Mambo, ambao hutumia vitambuzi kuunganisha vipengele vya kimwili kwenye mtandao, inamaanisha kuwa sasa unaweza kuunda kitu kidijitali ambacho kinajifunza kila mara na kusaidia kuboresha mshirika wake halisi .
Mchambuzi wa teknolojia Rob Enderle anaamini kuwa tutakuwa na matoleo ya kwanza ya kufikiria mapacha wa kidijitali wa binadamu "kabla ya mwisho wa muongo."

Chanzo cha picha, Getty Images
Ujio wao utahitaji mawazo mengi na uzingatiaji wa kimaadili, kwa sababu mfano wetu wa kufikiri unaweza kuwa na manufaa makubwa kwa waajiri," anakumbuka.
"Itakuwaje ikiwa kampuni unayofanyia kazi itatengeneza pacha wako wa kidijitali na kusema 'hey, una pacha huyu wa kidijitali ambaye hatumlipi mshahara, kwa nini bado tunakuajiri?'
Enderle anaamini kuwa umiliki wa pacha hao wa kidijitali utakuwa mojawapo ya masuala muhimu ya enzi inayokuja ya mabadiliko makubwa.
Kumbukumbu za hadithi za kisayansi
Tayari tumeanza safari ya kuelekea kuunda mapacha wa binadamu, kwa kwa njia ya avatar waliotajwa hapo juu, lakini kwa sasa ni vigumu sana na ni wa zamani.
Kwa mfano, katika mfumo wa uhalisia wa Meta (Facebook) wa Horizon Worlds , unaweza kuipa avatar yako sura inayofanana na yako, lakini huwezi hata kuipatia miguu kwa sababu teknolojia iko katika hatua ya kwanza.
Sandra Wachter, mtafiti mkuu wa AI katika Chuo Kikuu cha Oxford, anaelewa mvuto wa kuunda mapacha wa kidijitali wa wanadamu: "Inakumbusha riwaya za kusisimua za uongo za sayansi, na hivi sasa ndio hatua iliopigwa."

Chanzo cha picha, sandra watcher
Anaongeza kuwa ikiwa mtu "atafaulu katika shule ya sheria, anaugua, au anafanya uhalifu itategemea bado 'swali la asili dhidi ya malezi' linalojadiliwa."
"Itategemea bahati nzuri na mbaya, kwa marafiki, familia, asili yako na hali ya kijamii na kiuchumi, na bila shaka juu ya chaguo lako binafsi," anasema.
Hata hivyo, anaeleza, AI bado si nzuri katika kutabiri haya "matukio
ya kipekee ya kijamii kutokana na utata wao wa asili."
"Kwa hivyo tuna safari ndefu hadi tuweze kuelewa na kuiga maisha ya mtu kutoka mwanzo hadi mwisho, tukichukulia kuwa inawezekana kila wakati."
Matumizi ya sasa
Badala yake, ni katika nyanja za muundo wa bidhaa, usambazaji, na upangaji miji ambapo utumiaji wa mapacha wa kidijitali kwa sasa ni wa kisasa zaidi na umeenea.
Katika mbio za magari ya Formula 1, timu za McLaren na Red Bull hutumia pacha wa kidijitali wa magari yao ya mashindano ya mbio.
Wakati huo huo, kampuni ya posta ya DHL inaunda ramani ya kidijitali ya ghala lake na msururu wa usambazaji wa afisi zake ili kuiwezesha kuwa na ufanisi zaidi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Na miji yetu inazidi kuigwa katika ulimwengu wa kidijitali; Shanghai na Singapore zina pacha wa kidijitali, waliundwa ili kusaidia kuboresha muundo na uendeshaji wa majengo, mifumo ya usafiri na mitaa.
Nchini Singapore, mojawapo ya kazi za pacha wake wa kidijitali ni kusaidia kutafuta njia mpya za watu kuzunguka na kuepuka maeneo ya uchafuzi wa mazingira. Maeneo mengine hutumia teknolojia inayopendekeza mahali pa kujenga miundombinu mipya, kama vile njia za treni za chini ya ardhi.
Miji mipya pia inajengwa katika eneo la Mashariki ya Kati wakati huo huo katika ulimwengu halisi wa kidijitali.
Kampuni ya programu ya Ufaransa ya Dassault Systèmes inasema imepokea maombi kutoka kwa maelfu ya makampuni kwa ajili ya teknolojia yake pacha ya kidijitali.
Kufikia sasa, kazi yake imejumuisha kutumia mapacha wa kidijitali kusaidia kampuni ya utunzaji wa nywele kubuni chupa za shampoo endelevu kidigitali, badala ya mifano isiyoisha ya maisha halisi. Hii inapunguza uharibifu.

Chanzo cha picha, Getty Images












