Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 12.12.2023

Chelsea wako tayari kupokea maombi ya kumuuza kiungo wa Uingereza Conor Gallagher, 23, wakati dirisha la uhamisho litakapofunguliwa mwezi ujao ili kumtafutia fedha kocha Mauricio Pochettino, ambaye anaweza kumnunua mshambuliaji wa Brentford na England Ivan Toney, 27, au mhambuliaji wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen. (Mail)

Beki wa Ufaransa Axel Disasi na beki wa Uhispania Marc Cucurella ni miongoni mwa wachezaji saba ambao kocha wa Chelsea Mauricio Pochettino yuko tayari kuwauza Januari, licha ya Disasi, 25, kujiunga na The Blues msimu uliopita na Cucurella, 25, aliyegharimu zaidi ya £60m mwezi Agosti 2022. (Teamtalk)

Manchester United wanataka kubadilishana winga wa Uingereza Jadon Sancho, 23, na winga wa Barcelona wa Brazil Raphinha, 26. (Sport - kwa Kihispania)

Manchester United hawana nia ya kutumia chaguo la kuongeza muda mkataba wa mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, 28, utakapokamilika mwishoni mwa msimu huu. (Athletic)

Manchester United wako tayari kupokea maombi ya kuwauza kiungo wa kimataifa wa Brazil Casemiro, 31, mlinzi wa zamani wa Ufaransa Raphael Varane, 30, na kiungo wa Uholanzi Donny van de Beek, 26, mwezi Januari, pamoja na Martial na Sancho. (Guardian)

Iwapo Sancho ataondoka Manchester United mwezi Januari, mshambuliaji wa wa Ivory Coast Amad Diallo, 21, anaweza kuchukua nafasi yake katika kikosi chao cha kwanza baada ya kuuguza jeraha. (Football Insider)

West Ham United inasalia "asilimia 100" nyuma ya David Moyes, 60, licha ya kushindwa kwa mabao 5-0 ugenini na Fulham.(Telegraph).

Wawakilishi wa Bayern Munich walikuwa kwenye mchezo wa Jumapili kumfuatilia kiungo wa kati wa Fulham na Ureno Joao Palhinha, 28, ambaye nusura wamsajili msimu uliyopita. (90min)

Tottenham wamekubali mkataba mpya wa muda mrefu kwa beki wa Italia Destiny Udogie, 21. (Fabrizio Romano).

Everton wanataka kumrejesha mlinzi wa Uingereza Mason Holgate, 27, kutoka kwa mkopo wake wa muda Southampton kwa sababu hapati muda wa kucheza. (Sun)

Bournemouth wamempa Lloyd Kelly, 25, mkataba wa kitita kikubwa katika klabu hiyo katika jitihada za kumshawishi kusaini kandarasi mpya. (Teamtalk)

Brentford wako sokoni kutafuta mshambuliaji mwezi ujao hata kama Toney atasalia katika klabu hiyo, huku mchezaji wa kimataifa wa Marekani wa FC Cincinnati Brandon Vazquez, 25, akiwa miongoni mwa washambuliaji wanaowawania. (Telegraph - usajili unahitajika)

Kiungo wa kati wa Red Bull Salzburg Israel Oscar Gloukh, 19, yuko kwenye rada za Aston Villa kabla ya dirisha la usajili la Januari. (Football Insider)

Kiungo wa klabu ya Feyenoord na timu ya taifa ya Uholanzi Quinten Timber, 22, ndugu pacha wa beki wa Arsenal Jurrien, analengwa na Fulham. (Teamtalk)

Arsenal wamefanya mazungumzo ya kandarasi na mlinzi wa Uingereza Reuell Walters huku wakijaribu kuzuia nia ya kumnunua kinda huyo mwenye umri wa miaka 18 kutoka kwa klabu zingine za Ligi Kuu ya Uingereza na barani Ulaya. (Standard)

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi