Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ndege ya kijeshi ya Urusi iliyoanguka ya Ilyushin 76, ni nini kinachojulikana kufikia sasa?
Ndege ya kijeshi ya Urusi ya Ilyushin 76 imeanguka katika eneo la Belgorod mwendo wa saa 11:00 kwa saa za huko, Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema.
Sababu za ajali hiyo hazijatangazwa rasmi; inawezekana kulikuwa na wafungwa wa Ukraine kwenye ndege hiyo. Wafanyikazi wakuu wa Ukraine waliozungumza na BBC walisema kuwa bado hakuna habari kwa ukamilifu zilizotolewa.
Ndani ya ndege hiyo ya Il-76 iliyoanguka kulikuwa na wanajeshi 65 waliotekwa wa Kikosi cha Wanajeshi wa Ukraine waliosafirishwa hadi mkoa wa Belgorod kwa ajili ya mabadilishano, wafanyikazi sita wa ndege hiyo na watu watatu waliokuwa wameandamana nao, Wizara ya Ulinzi ya Urusi inadai.
Idara hiyo haikubainisha ikiwa kuna watu walionusurika katika ajali hiyo ya ndege, lakini gavana wa eneo la Belgorod, Vyacheslav Gladkov, baadaye alisema katika kituo cha telegram: "Kila mtu aliyekuwemo amefariki."
Hapo awali, mtandao wa telegramu na wanablogu wa kijeshi waliripoti kuhusu ajali ya Il-76 katika wilaya ya Korochansky eneo la Belgorod, wakiweka video ambayo inadaiwa inaonyesha ndege hiyo ikianguka na kulipuka ardhini.
Wakati huo huo, vyombo vya habari vya Ukraine vilidai hapo awali, vikinukuu chanzo katika Kikosi cha Wanajeshi cha Ukraine, kwamba "hii ni kazi yao." Nukuu hii ilitolewa na Ukrayinska Pravda na RBC-Ukraine. Kulingana na vyanzo hivyo, Il-76 iliyoanguka haikuwa ikisafirisha wafungwa, lakini "labda" makombora ya mfumo wa ulinzi wa anga wa S-300.
Baadaye, ujumbe huo ulihaririwa, na kuondoa maneno kuhusu "kazi" ya jeshi la Ukraine. Wizara ya Ulinzi ya Ukraine bado haiwezi kuthibitisha kwamba ndege hiyo ilishambuliwa na Wanajeshi wa Ukraine, kwa kuwa "bado wanakusanya taarifa," kulingana na kituo cha matangazo cha Suspilne.
Idhaa ya BBC ya Ukraine iliomba Jenerali wa Wafanyakazi wa Ukraine, Wizara ya Ulinzi na Kurugenzi Kuu ya Ujasusi wa Kijeshi kutoa maoni. Hata hivyo, wafanyikazi wakuu walisema kuwa hadi sasa hakuna habari rasmi na kwamba kila kitu bado kinafuatiliwa.
Urusi ilikataa kutoa maoni juu ya ripoti ya Wizara ya Ulinzi. "Hii ni habari mpya kabisa. Sasa tutashughulika nayo," Katibu wa Habari wa Rais wa Urusi Dmitry Peskov alisema.
Ndege ya Il-76 ilianguka kilomita tano hadi sita kutoka kijiji cha Yablonevo, hakukuwa na uharibifu wowote chini, mkuu wa kanisa la mtaa aliiambia TASS.
Uchambuzi wa ajali ya ndege ya Il-76 na mwandishi wa BBC Pavel Aksenov
Mtandao wa telegram wa Urusi unadai kuwa ndege ya Il-76, iliyoanguka katika eneo la Belgorod, ilidunguliwa na walinzi wa anga wa Ukraine. Uthibitisho wa habari hii unaweza kuwa video inayoonyesha ushahidi wa kombora au wakati ambapo ndege ilishambuliwa.
Lakini hakuna video kama hiyo, na kwa msingi wa video iliyowekwa mtandaoni ni vigumu kufikia hitimisho la wazi juu ya sababu za ajali ya ndege hiyo - ni sekunde zake za mwisho tu zilirekodiwa, na ndege yenyewe haionekani vizuri.
Video inaonyesha jinsi ndege hiyo inavyoelekea ardhini. Wakati fulani, kipande kikubwa kinaanguka, baada ya hapo, labda pengine, moto unaoneka kutapakaa katika eneo la upande wa kushoto.
Huu hauwezi kuwa ushahidi wa wazi kwamba ndege ilitunguliwa, wala haiwezi kutumiwa kukanusha utokeaji wa tukio hilo.
Mahali ambapo ndege hiyo ilianguka iko umbali wa kilomita 90 kutoka mpaka wa Ukraine. Hii inaweza kuruhusu Ukraine kutumia mifumo ya makombora ya masafa ya kati ya kukinga ndege.
Kwa mfano, mifumo ya ulinzi wa anga ya Patriot au Buk inaweza kuangusha ndege kwa umbali kama huo. Mfumo wa IRIS-T SLM, ambao unahudumu na Kikosi cha Wanajeshi cha Ukraine, ina uwezo wa kufika umbali wa kilomita 40 na haiwezi kushambulia kwa umbali kama huo.
Siku 10 kabla ya ajali ya Il-76 juu ya Bahari ya Azov, ndege ya A-50, ambayo ilijengwa kwa msingi wa ndege ya Il-76, ilipigwa risasi huku ndege ya Il-22 pia ikiharibiwa vibaya.
Kulingana na habari za kituo kimoja, alipigwa risasi na jeshi la Ukraine. Ndege zote mbili zilipatikana takriban kilomita 150 kutoka eneo la karibu linalodhibitiwa na Kikosi cha Wanajeshi wa Ukraine. Kwa hivyo kinadharia uwezekano kama huo upo.
Ikiwa Ukraine, kama wachambuzi wa Urusi wanavyodai, ilitumia mfumo wa ulinzi wa anga wa Patriot, basi umbali wa makombora yake ya PAC 2 ni kilomita 160.
Vile vile, thamani na jukumu lake katika ulinzi wa vitu ambavyo ni muhimu kimkakati ni kubwa sana.
Haijulikani ikiwa Ukraine wangeweza kuhatarisha silaha muhimu kama hiyo kuharibu ndege wakati wanaweza kuiangusha.
Wakati wa kujadili uwezekano wa uhamishaji wa silaha za Magharibi kwenda Ukraine, haswa, makombora kama ilivyoripotiwa kwenye vyombo vya habari, Marekani ilionyesha hofu kwamba Vikosi vya Wanajeshi vya Ukraine vitazitumia dhidi ya malengo nchini Urusi. Hata hivyo, hakujawa na uthibitisho rasmi.
Uhusiano kati ya wafungwa na ndege ya Il-76
Na, Mwandishi wa BBC Svyatoslav Khomenko.
Hakuna kitu cha ajabu katika ukweli kwamba anga inaweza kutumika kufanya mabadilishano ya wafungwa.
Ndiyo, katika video za kubadilishana wafungwa kwa kawaida tunaona wafungwa wanasafirishwa hadi mahali pa mikutano kwa basi.
Lakini ikiwa tunazungumza juu ya wafungwa ambao, kwa muda wa miezi kadhaa au hata miaka wakiwa wamezuiliwa, walihamishwa hadi katika kizuizi kilicho eneo la mbali kabisa la Urusi, basi lazima kwa namna fulani waletwe karibu na mpaka.
Zaidi ya hayo ubadilishanaji wa aina hii mara nyingi lazima uwe wa haraka iwezekanavyo: mazungumzo juu ya kubadilishana ni magumu na yanayobadilika badilika, na inawezekana kabisa kwamba ni lazima kumtoa mtu kutoka Tyumen kwenda Belgorod, hadi kwenye mpaka katika mkoa wa Kharkov, mara moja.
Katika mahojiano na jamaa za wanajeshi wa Ukraine waliobadilishana hapo awali, ni rahisi kupata marejeleo ya ukweli kwamba ndege zilitumiwa kusafirisha wafungwa hadi eneo la kubadilishana.
Imefasiriwa na Asha Juma