Urusi na Ukraine: Je unyakuaji wa Urusi wa majimbo ya Ukraine una maana gani?

G

Chanzo cha picha, Getty Images

Ni vipi Urusi itaweza kuyanyakua majimbo manne iliyoyavamia, lakini tu kwa sehemu, wakati yamo katika eneo la vita ?.

Vladimir Putin amesaini tayari makubaliano ya kunyakua majimbo yaliyovamiwa , baada ya kutangaza kwamba Urusi haitawahi kamwe kuyaacha na itayalinda kwa njia zote.

Rais wa Urusi anakabiliwa na wakati mgumu. Ni mwezi wake wa saba wa kupoteza kasi ya vita kwani upinzani mkubwa wa Ukraine wa kukabiliana na Urusi , umezuia kuchukuliwa kwa majimbo yake mawili ya Luhansk na Donetsk, ambayo awali ilikuwa imeyachukua.

Katika majimbo manne yaliyo chini ya uvamizi wa Urusi, Putin aliendesha kile, alichokiita kura ya maoni, iliyolaaniwa na jamii ya kimataifa, ambayo iliyataja kama maigizo na wakati mwingine kuwahusisha wanajeshi wenye silaha waliokwenda mlango kwa mlango kukusanya kura.

 Kwa kunyakuwa majimbo manne ya mashariki pamoja na Zaporizhzhia na Kherson kusini mwa nchi, ataweza kutuma vikosi vingine vipya vya watu walioingizwa jeshini katika eneo la vita ambalo Moscow inasema lina ukubwa wa zaidi ya kilomita 1,000. 

Lakini pia anaweza kuyatisha mataifa ya Magharibi iwapo yanaendelea kuipatia silaha Ukraine kwa makombora yaliyotumiwa dhidi ya kile alichosema ni eneo la Urusi.

 Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres alilaani kunyakuliwa kwa majimbo ya Ukraine jambo ambalo alisema ni kuongeza hatari zaidi “Umamuzi wowote wa kushitaki…hautakuwa na thamani ya kisheria na unafaa kulaaniwa. Hauwezi kuendana na mfumo wa kimataifa wa sheria ; unakwenda kinyume na kila kitu ambacho kinapaswa kukubaliwa na jamii ya kimataifa; unakiuka malengo na kanuni za Umoja wa Mataifa.

Ni sawa na Crimea?

Anachokifanya katika majimbo manne aliyoyanyakua Bw Putini kinaonekana kama nakala ya kaboni ya kile alichokifanya Machi 2014, aliponyakua jimbo la Ukraine, kuitishwa kura ya maoni kulalaaniwa pakubwa na jamii ya kimataifa , lakini aliendelea na unyakuzi huo, kupitia mchakato halisi wa kikatiba uliopelekea kupigwa kwa kura ya ya bunge la Urusi, ambalo liliunga mkono unyakuzi huo.

G

Chanzo cha picha, KREMLIN HANDOUT

Maelezo ya picha, Baada ya kusaini mikataba ya unyakuzi wa majimbo , Vladimir Putinalijiunga na wanajeshi na wanaume wengine wanne ambao Urusi iliwapa uongozi wa majimbo ya Ukraine yaliyovamiwa
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Tofauti na unyakuzi wa sasa, Crimea ilitwaliwa kwa umwagaji mgogo wa damu na ikawa chini ya udhibiti kamili wa Urusi.

 Kwa viwango mbali mbali, maeneo manne ambayo yananyakuliwa na Urusi kwa sehemu bado yako mikononi mwa Waukraine. Yote kwa pamoja yanawakilisha15% ya eneo la taifa la Ukraine.

 Majimbo mawili ya mashariki kwa sehemu yamekuwa yakishikiliwa na wanamgambo wanaotaka kujitenga na Ukraine wanaoungwa mkono na Urusi tangu mwaka 2014 , lakini baada ya miezi saba ya vita ni 60% ya Donetsk ambayo Urusi inaweza kudai kuwa yake, na Luhansk iko katikati ya mapigano makuu ya Waukraine.

Vikosi vya Urusi vinaweza vinakaribia kupoteza mji muhimu wa mkakati wa vita wa Lyman.

Mji mkuu wa jimbo wa Zaporizhzhia uko chini ya udhibiti wa Ukraine, ingawa uko katika eneo linaloweza kushambuliwa na makombora ya Urusi, na vikosi vya Ukraine viko kilomita chache kutoka mji wa Kherson.

Unawezaje kunyakua majimbo manne ambayo hata hauwezi kuyadhibiti?, bila shaka kiongozi wa Urusi aliharakisha kufanya hivyo, kujitangazia kura za maoni bila taarifa.

 Katika hotuba yake ya unyakuzi, Rais Putin alitoa wito wa usitishaji wa mapigano na Urusi, na kufufua mazungumzo, lakini alieleza wazi kuwa hakutakuwa na urejeshaji wa wa maeneo yaliyonyakuliwa kwa Ukraine. Sehemu kubwa ya hotuba yake ilikuwa imejaa hasira dhidi ya nchi za Magharibi.

 Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alisema Ikumaa kwamba shambulio lolote dhidi yae neo lililonyakuliwa litachukuliwa kama kitendo cha uchokozi.

Nini kitabadilika?

Haijawa wazi bado. Hata Bw Peskov hakuweza kufafanua ni wapi Urusi itachora mipaka yake katika eneo lililovamiwa la kusini mwa Ukraine. 

Alisema, hatahivyo, kwamba Urusi italichukulia jimbo lote la Donetsk kama sehemu ya Urusi. Kwa sehemu hizo ambazo bado haziko chini ya uvamizi, alisema zinapaswa "kukombolewa".

Ukraine inajibu vipi?

Rais Volodymyr Zelensky alijibu hatua ya unyakuzi wa Urusi kwa kutoa wito kwa wajumbe wa NATO kuongeza kasi.

Hii inaonyesha mabadiliko kuanzia mwanzo wa vita, ambapo alitangaza kwamba ataacha kushinikiza wajumbe wa muungano huo wa kujihami wan chi za Magharibi wa nchi 30, kutokana na hofu ya makabiliano na Urusi.

Anafahamu , hatahivyo kuwa atatakiwa kuzishawishi nchi zote wajumbe wa muungano huo zikubali, jambo ambalo huenda lisikubaliwe na Uturiki. Pia amebainisha wazi kwamba unyakuzi hautaipatia Kremlin kile inachokitumaini: "Ukraine haiwezi na haitaweza kuvumia majaribio ya kuchukua sehemu yae neo letu."

Je ni vipi wakati huu ni hatari?

Hakuna yeyote kusema kweli anayefahamu nini kinachoendelea akilini mwa kiongozi wa Urusi, lakini maneno yake ya chuki dhidi ya Magharibi yamefikia kiwango kipya. 

Ni wazi kwamba anataka Magharibi waelewe kuwa Moscow inayaangalia mashambulio katika maeneo yaliyotwaliwa na Urusi kuwa kama uvamizi dhidi ya Urusi yenyewe.

Lakini hali ni mbaya kiasi gani katika uwanja wa mapigano na zaidi yake?

 Rais Putin tayari ametishia kutumia njia zote alizonazo kulinda eneo la Urusi, ikiwa ni pamoja na kutumia silaha za nyuklia. "Sio uongo," alisema. Na waziri wake wa ulinzi anasema Urusi inapigana na Magharibi hata zaidi ya Ukraine.

 Kiongozi wa Ukraine alipuuzilia mbali tisho la nyuklia, alilotaja kama "simulizi la kudumu la maafisa wa Urusi na wanaofanya propaganda". 

Na Paul Stronski anaamini kuwa ‘’kauli za ushawishi za Urusi za mara kwa mara’’ zinalenga kuzuia nchi za Magharibi hata kuiunga mkono Ukraine, licha ya kwamba zinaonekana kuazimia kupinga tisho hilo.

 Ijumaa, msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alisema kauli za hivi karibuni kuhusu nyuklia zilikuwa za kukosa uwajibikaji : "Tunatoa wito kwa kila mmoja kuwa na tabia ya uwajibikaji''