Afya: Je, vyakula vya kuongeza hamu ya tendo vinafanya kazi kweli?

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES
- Author, Jessica Brown
- Nafasi, BBC
Chokoleti, stroberi, chaza; huelezwa ni vyakula vinavyoweza kuongeza hamu yetu ya kufanya mapenzi na kuboresha ufanyaji wa tendo lenyewe. Lakini kuna ukweli wowote kwenye madai hayo?
Kwa wale ambao wana matatizo na ufanyaji wa mapenzi, ni kweli vyakula fulani vinaweza kusaidia kwa njia sawa na dawa na Viagra.
Jamii mbalimbali katika historia zimetafuta vyakula ambavyo vinaweza kuongeza hamu ya kufanya mapenzi au kuboresha utendaji wa ngono.
“Hata hivyo, watu walio na matatizo katika ufanyaji wao wa mapenzi ndio huona mabadiliko wanapokula hivi vyakula,” anasema Lauri Wright, msemaji wa Chuo cha Nutrition and Dietetics, kutoka Marekani. “Mtu asiye na matatizo hawezi kuona mabadiliko yoyote.”
Chakula kimoja ambacho kinaaminika kwa muda mrefu kuongeza hamu ya ngono ni chokoleti. Utafiti unaonyesha umeonyesha kuwa kakao pia linaweza kuongeza hamu.
Kula chokoleti kunaweza kuongeza hamu ya ngono kwa kuchochea utengenezaji serotonini na kemikali ya dopamini ya nyurotransmita, ambazo pia huchangia katika mwitikio wetu wa ngono.
End of Pia unaweza kusoma
Mtindo wa maisha na lishe

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES
Michael Krychman, mtaalamu na mshauri wa masuala ya kujamiiana kutoka kliniki ya Sexual Health and Survivorship Medicine, Marekani anasema "tunachojua ni kwamba, watu wanaofanya mazoezi, kula lishe bora na kupunguza msongo wa mawazo, vitu hivi vyote huboresha maisha ya ngono."
“Mlo wetu unaweza kufanya kazi kama kichochezi kutupa manufaa kama vile mtiririko mzuri wa damu, kuongezeka homoni au kuongeza hamu,” anasema Wright.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
“Jambo la msingi kuzingatia ni samaki, nyama isiyo na mafuta, karanga, matunda, mboga mboga na nafaka, huasaidia kazi ya neva na kusaidia mtiririko wa damu na homoni," anasema Wright.
"Hamu ni ya kimwili na ya kisaikolojia. Ukweli kwamba hamu ya kufanya ngono ina mambo mengi. Dawa au chakula vinaweza kufanya kazi,” anasema Nan Wise , mtaalamu wa saikolojia na masuala ya kujamiina katika Chuo Kikuu cha Rutgers huko New Jersey.
“Uzoefu wetu pia unaweza kuchangia kujua ni vyakula gani vinavyoongeza hamu ya ngono kwa mtu mmoja mmoja,” anasema Jean-Christophe Billeter, profesa wa tabia za kijamii na kujamiiana katika Chuo Kikuu cha Groningen nchini Uholanzi.
"Ubongo unakuwa na waya wa kutengeneza kumbukumbu tunapopata mafanikio ya tendo la ndoa, kulingana na hali itakavyotokea katika mazingira ambayo mtu alifanya ngono, hii itakua ni kitu cha kuamsha hamu ya kufanya mapenzi katika siku za usoni."
Kuna utafiti unapendekeza kuwa mawazo chanya yanahusishwa na kuongezeka kwa msisimko wa ngono, na lishe iliyo na yakula vingi vya mimea.
Chakula na Mvuto

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES
Inawezekana chakula chochote kinaweza kuwa na sifa za kuongeza hamu. Kwa maana kwamba, ikiwa mtu ana njaa na hakuna chakula, hamu yake ya ngono itapungua.
Kimsingi, wanadamu wana hamu ya kufanya ngono ili kuzaliana, na tunahitaji kuwa na uzito mzuri na kuwa na lishe ambayo hutoa virutubisho sahihi ili kufanya hivyo," Billeter anasema.
Kuna ushahidi kwamba chakula kilionekana mara kwa mara katika matendo ya ngono ya Karne ya 17 kwa sababu hiyo hiyo, ili kusaidia wanandoa kwa raundi inayofuata.
Pia kuna ushahidi kwamba tunakula vyakula vinavyotufanya tuonekane tunavutia kwa watu wa jinsia tofauti. Fikiria ndege fulani, madume wana rangi nyingi zaidi kwa sababu majike wanavutiwa nazo, na wanapata rangi hii kwa kula vyakula fulani.
Hiyo ipo kwa wanadamu, pia. Hapo awali, wanawake walionekana kuwa wa kuvutia zaidi wakiwa wanene, kunenepa wakati hakukuwa na chakula kingi kuliashiria mwanamke ni mzuri katika kuzaliana," anasema Bileter.
"Buibui hukamata nzi ili kuwasilisha kwa majike ili kujamiiana, wakati nyenje huzalisha jeli ili kuwashawishi majike kujamiiana nao," anasema Abbott.
Wazo la vyakula vya kuongeza hamu limedumu kwa muda mrefu kwa sababu watu daima huvutiwa na dhana ya maisha marefu ya ujana na uzazi.
Imetafsiriwa na Rashid Abdallah












