Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 19.10.2024
Newcastle wanataka kumsajili Marc Guehi Januari mwakani, Chelsea hawana nia ya kumuuza Cole Palmer na Manchester City kumenyana na Bayern Munich katika usajili wa Florian Wirtz.
Newcastle wako tayari kufanya kufufua mpango wa kumsajili beki wa England na Crystal Palace Marc Guehi, 24, mwezi Januari kwa takriban £80m. (Team Talk)
Chelsea haitakubali ofa ya kumuuza kiungo mshambuliaji Cole Palmer, 22, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza akihusishwa na kurejea katika klabu yake ya zamani ya Manchester City. (Football Insider)
Manchester City pia wanaonyesha nia ya kumnunua kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Florian Wirtz, 21, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Bayern Munich. (Sky Germany via Sky Sports)
Mabingwa wa Ufaransa Paris St-Germain na Real Madrid pia wanamtaka Wirtz, huku Leverkusen wakipendelea ofa kutoka nje ya Ujerumani. (Goal)
Manchester United wana nia ya kumuajiri kocha wa Sporting Lisbon Ruben Amorim, 39, ambaye ana kifungu cha kuondoka katika mkataba wake ambacho kitaanza kutumika mwaka wa 2025. (Florian Plettenberg)
Winga wa Bayern Munich Mjerumani Leroy Sane, 28, hana nia ya kuhamia Newcastle United. (CaughtOffside)
Nahodha wa Manchester United Bruno Fernandes alikuwa tayari kuondoka katika klabu hiyo msimu uliopita kabla ya Red devils kumpa kiungo huyo wa kati wa Ureno, 30, mkataba mpya wenye mafao "makubwa". (ESPN)
Mkufunzi wa Arsenal Mhispania Mikel Arteta, 42, anadokeza kuwa atakuwa tayari kuinoa England siku zijazo. (Guardian)
Wakufunzi Eddie Howe na Graham Potter waliohojiwa kuongoza timu ya taifa ya England kabla ya Thomas Tuchel kuteuliwa, jambo lililozua maswali kuhusu madai ya Chama cha Soka kwamba makocha 10 walishiriki katika mahojiano. (Telegraph - usajili unahitajika)
Tottenham wanamfuatilia kwa karibu winga wa Borussia Dortmund Muingereza Jamie Bynoe-Gittens mwenye umri wa miaka 20 wakiwa na mpango kumsajili. (Football Insider)
Liverpool wako tayari kumenyana na Borussia Dortmund kuwania saini ya kiungo wa wa Red Star Belgrade na Serbia Andrija Maksimovic, 17. (CaughtOffside)
Manchester City wamepiga hatua katika juhudi za kumsajili mshambuliaji wa Jamhuri ya Ireland wa chini ya umri wa miaka 17 Michael Noonan, 16, kutoka Athletic ya St Patrick. (Fabrizio Romano)
Winga wa New York City mwenye umri wa miaka 20 kutoka Argentina, Julian Fernandez angependa kuichezea Liverpool siku zijazo, licha ya klabu yake kumilikiwa na City Football Groupi, wamiliki wa Manchester City. (Express)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi